Mwinyi katuachia laana!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,701
Ni wakati sasa watanzania tumuombe rais huyu mstaafu afute kauli yake kuwa: "SISI NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU", maana kila mashindano tunaharibu. Yule mzee katulaani!
 
Unategemea nini unapokuwa na wachezaji wavuta bangi? Utavuna bangi!!!
 
Mkuu wala tusimsingizie babu wa watu, tatizo letu ni usimba na yanga na pia maandalizi kiongozi.

Tunajisahau na kudhani tumeshapiga hatua tunajiweka class ambayo hatuko, tuache siasa ifanyike juhudi kuinua kiwango cha michezo, kwa sasa ni kama tunabahatisha kiongozi. Timu imejaa wavuta bangi, wasio na adabu, makocha wetu wamejaa siasa na kulalamika tu badala ya kutafuta njia za kubobea kwenye fani unategemea nini hapo.

Ushauri wa bure tu, tusahau habari za mashindano kwa sasa, serekali au sijui wadau watengeneze timu kwa miaka 3 au zaidi ndio tuanze kushindana, kwa sasa ni kupoteza muda na hela bure tu
 
Me nahisi ile laana ndio inatufanya tujisahau...
 
Mlikuwa mnataka kocha mzawa mkapewa Jamuhuri Kiwelu, kocha gani anashinda Magome Mapipa, Delaxe bar anakunywa bia tu, hiyo mipango au mbinu za ushindi atazifanya muda gani?
 
Ni wakati sasa watanzania tumuombe rais huyu mstaafu afute kauli yake kuwa: "SISI NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU", maana kila mashindano tunaharibu. Yule mzee katulaani!
Mzee Mwinyi alizungumzia uhalisia wa timu yetu. Hata ww pengine ungesema vivyo hivyo au zaidi yake. JK alijitahidi kadri yake, ikiwemo kumgharamia kocha na kuwaenzi wachezaji kwa hali na mali lakini wapi! Tatizo bado lipo, ina maana halijapata dawa? Hatuna wachezaji? Tatizo ni nini?
 
Kujua tatizo ni nini inahitajika mjadala wa kitaifa!
 
Ni wakati sasa watanzania tumuombe rais huyu mstaafu afute kauli yake kuwa: "SISI NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU", maana kila mashindano tunaharibu. Yule mzee katulaani!

Pengine ni kwa kujua historia yetu ndo akatoa hiyo kauli. Unadhani mtu akisema TZ ni nchi ya ufisadi atakuwa amekosea? wala hahitaji kuondoa hiyo kauli yake, yuko sahihi na ukweli ndo huo. Ataendelea kuwa sahihi mpaka tutakapoondoa siasa kwenye mambo yanayohitaji utaalamu na umakini!
 
Mlikuwa mnataka kocha mzawa mkapewa Jamuhuri Kiwelu, kocha gani anashinda Magome Mapipa, Delaxe bar anakunywa bia tu, hiyo mipango au mbinu za ushindi atazifanya muda gani?

Tatizo la Julio maneno mengi kuliko vitendo!
 
Pengine ni kwa kujua historia yetu ndo akatoa hiyo kauli. Unadhani mtu akisema TZ ni nchi ya ufisadi atakuwa amekosea? wala hahitaji kuondoa hiyo kauli yake, yuko sahihi na ukweli ndo huo. Ataendelea kuwa sahihi mpaka tutakapoondoa siasa kwenye mambo yanayohitaji utaalamu na umakini!

Kwa kweli sisi tumetawaliwa sana na siasa, kila kitu siasa inachukua nafasi kuliko utaalamu!
 
Tusilaumu makocha na wachezaji wa mpira. Kiukweli Tanzania kila kitu tunakuwa wa kusua sua tu. Angalia uchumi, utendaji kazi n.k. Nadhani sisi tunawezea sana suala la ngono.
 
Ahahahaah!! Tumlaumu sasa nani??
 
Nafikiri tatizo si mwinyi ila hao tunaowapa timu! Nilibahatika kusafiri na julio kwenda mwz pumba alizotoa nilisikitika!
 
Nikahoji uwezo wake wa kiakili! Kama anashindwa kupambanua mambo ya kawaida tu! Coastal wata baki kweli mwaka huu?
 
kila timu inapocheza, wataalam wanaagiza watanzania wasiache sara na dua, hii ni akili matope.
Je wale wengine hawafanyi vivyo hivyo kama sisi.
Maandiko yanasema unavuna unachopanda, si vinginevyo.
Hata tukicheza hovyo tunahitaji kushinda, hii ni ajabu kwelikweli!
 
Back
Top Bottom