Mwinjilisti amvaa Rais Magufuli, amuonya

Mwinjilisti amvaa Rais Magufuli, amuonya

Mchungaji gani asiyejua mamlaka iliyopo inatambuli mpaka kwa MUNGU?hajielewi huyo,wala kwenye uzi huu sirudi tena

Tumeambiwa katika biblia kutii mamlaka iliyopo, LAKINI ni mamlaka halali tuu kwa maana hata shetani ana mamlaka lakini mamlaka ya haki, hivyo hatupasi kuitii mamlaka isiyotenda haki!!!?
 
Rais wa Tanzania HANA nguvu ya kuzuia watu kufanya kazi zao za kisiasa
Hata Sept 1 CHADEMA wakiwa ngangari watafanikiwa
CHADEMA ya Dr Slaa wangefanikiwa
Sina uhakika na CHADEMA hii ya Lowassa ambayo ni kama tu CCM B
 
Watumishi kama hawa wanaona kweli na kuikemea hadharani ni wachache sana wengi hasa bakwata wanaweka njaaa zao mbele lakini damu ya watu ipo mikononi mwao na uzao wao
BAKWATA ni taasisi ya serikali
Hata kuhudumiwa sasa wanahudumiw ana serikali ikiwemo matibabu ya viongozi wao nje ya nchi
WAPUUZWE
 
Mimi namuunga mkono rais kwenye mambo mengi kama kutumbua majipu,kuyazuia majipu,kukusanya kodi n.k
Simuungi mkono kabisa kwenye uoga wake wa kisiasa dhidi ya wanasiasa wenzake!!Hilo tu ndio linanikera sana
 
Mimi namuunga mkono rais kwenye mambo mengi kama kutumbua majipu,kuyazuia majipu,kukusanya kodi n.k
Simuungi mkono kabisa kwenye uoga wake wa kisiasa dhidi ya wanasiasa wenzake!!Hilo tu ndio linanikera sana
Hata katika hilo linaloitwa kutumbua majipu, kuwe na staha. Siyo ile ya Makonda-nitumbue, tumbuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Rais hafanyi hivyo, kuna taratibu zake.
 
Tunakurupuka,tunatengeneza matatizo,baadaye tunayatatua alafu tunajisifu kwa wananchi hizi akili za ccm
 
Mchungaji gani asiyejua mamlaka iliyopo inatambuli mpaka kwa MUNGU?hajielewi huyo,wala kwenye uzi huu sirudi tena
Tatizo ni kwamba je, huyo mwenye mamlaka anatambua kwamba Mamlaka hiyo aliyonayo imetoka kwa Mungu? Maana tatizo ndio huwa liko hapo. Huwa tunakuwa wepesi kunukuu huo waraka kwa Warumi kwamba mamlaka yote inatoka kwa Mungu, tunasahau wajibu wa utawala kwa Mungu ambaye ndio asili ya Mamlaka yote. Kama mtawala anatambua kwamba mamlaka aliyonayo imetoka kwa Mungu, basi atafuata haki, maana Mungu ni mwenye Haki. hatawabagua watu wake, maana anawatawala kwa niaba ya Mungu mwenyewe. ajiulize kwamba je, kama angekuwa ndio Mungu mwenyewe anatawala, angewabagua watu wake hivyo? Aliwakemea waisraeli wasiwabague hata wageni, sembuse waisraeli wenzao?
 
Ujumbe mzur ila gazeti alilotumia!
Nashaur atumie gazet lisilo na mlengwa wa Kisiasa
Tatizo ni kwamba hayo magazeti unayoyaamini, mengi yanaogopa kuandika habari kama hizo. inahitaji uwe na akili kama ya mwendawazimu hivi kuikosoa serikali siku hizi. Hizi siyo enzi za JK ati.
 
Kauli hii naifananisha na ya mchungaji kakobe alipomuandikia barua Rais mstaafu wa awamu ya nne kuhusu masuala fulani na kama hatakubali ushauri wake uchaguzi wa 2015 ungekuwa mgumu kwa chama, na ndivyo ilivyokuwa.
 
kiongozi huyu wa dini ameona mbali, na yaelekea anajuwa kwamba kumuombea pekee rais hakutakuwa na maana iwapo hatafuata misingi ya utawala bora.
 
M


Nionavyo mimi, rais wetu anayo hulka ya kuzungumzia hadharani mambo mengi amabayo anakuwa hajawashirikisha washauri na kwa kufanya hivyo makosa hayaepukiki. Aidha Rais wetu pia anayo hulka ya kuzungumzia mambo ambayo kwa nafasi yake hastahili kuzungumzia kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amewazuia wasaidizi wake kupata maoni kutoka kwa wadau na wananchi kwa ujumla. Tuzidi kumuombea Mungu amponye na udhaifu huu.
Mungu kweli amsaidie alitambue hilo, lasivo hilijambo litatugharimu.
 
Back
Top Bottom