Mwinjilisti amvaa Rais Magufuli, amuonya

Mwinjilisti amvaa Rais Magufuli, amuonya

Mamlaka unayopaswa kutii bila
shuruti ni ile iliyoko ndani
ya Sheria /katiba !

Na hiyo ndiyo anapaswa kuitumia!

Hata yeye anasema tufuate sheria !
 
Ujumbe mzur ila gazeti alilotumia!
Nashaur atumie gazet lisilo na mlengwa wa Kisiasa
 
Labda Magufuli atasikiliza ushauri wake kwa kuwa umetolewa na miongoni mwa watumishi wa Mungu ambao kila Mara Rais haachi kuomba maombi kutoka kwao.
 
Hitler aliwateketeza wayahudi milion zaid ya saba. Miongoni mwao makanisa makubwa enzi hizo hayakusema kitu chochote... miaka ya hivi karibuni Vatican eti wanajuta kwanini walikuwa wanaangaliatu huku wanadamu wanateketea.
Mwinjilisiti Mungu akubariki kwa kunena.
Mungu ibariki Tanzania
 
M
Anashaurika??
Je, ni kweli kwamba hadi kufikia kutoa kauli hzo hakuwa na washauri??
Ok... Labda kateleza au aliyasema hayo bila ya washauri wake kujua na wakati huo halipo ktk hotuba yake..... Je , baada ya one mistake hakuna marekebisho??.. ???.....

Nionavyo mimi, rais wetu anayo hulka ya kuzungumzia hadharani mambo mengi amabayo anakuwa hajawashirikisha washauri na kwa kufanya hivyo makosa hayaepukiki. Aidha Rais wetu pia anayo hulka ya kuzungumzia mambo ambayo kwa nafasi yake hastahili kuzungumzia kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amewazuia wasaidizi wake kupata maoni kutoka kwa wadau na wananchi kwa ujumla. Tuzidi kumuombea Mungu amponye na udhaifu huu.
 
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Kusupa amesema, kauli za Rais Magufuli ikiwemo ile kusema watakaoandamana ‘watakiona’ na kusema, ‘mimi sijaribiwi’ ni kauli zinazothibitsha namna rais huyo anavyokosa unyenyekevu wa kiuongozi.

Bora apewe za uso. Rev. Kasupa is a genuine person. Mchango wake pamoja na wa akina Mapalala, Makani, Mtei, Mtikila, Abdulrahman Babu,Marando, ... ktk harakati ya vyama vingi kila mtu anaujua. Ndiyo maana hawezi kukaa kimya wakati JPM anaturudisha nyuma miaka 50.
 
Huyu jamaa naona kaamua kutumiwa na Chadema
 
kwanza nampongeza sana Mtumishi Huyu wa Mungu. Kwa kuona Mbali na kutoa rai yake kwa Mh Rais.

Mimi nadhani ifikie maala kwamba serikali chini ya Rais Magufuli, ifikirie kuketi meza moja na viongozi wa vyama shindani na kubaliana juu ya mfumo mzuri wa kufanya siasa ndani ya nchi yetu.

Hii itasaidia sana kujenga umoja na mshikamano wa watanzania na udugu.

Haipendezi wewe kama Baba kula Chakula Mwenyewe huku watoto wakinungunika kwa kukosa lishe sawa na Baba yao.

Ifikie maala serikali ifungulie mikutano kwa vyama shindani na ipange utaratibu Mzuri kuusu Maanadamano Au kukubaliana kutokuwepo maandamano na kuruhusu Mikutano ya Kisiasa.

Hata mimi natoa wito kwa unyenyekevu kwa Mh Rais kwamba swala hili la Mikutano Au Kufanya siasa kwa vyama shindani kungetafutiwa muhafaka wa kitaifa kuliko kutumia nguvu.
 
Mchungaji gani asiyejua mamlaka iliyopo inatambuli mpaka kwa MUNGU?hajielewi huyo,wala kwenye uzi huu sirudi tena
Ushauri wake ni nzuri Mkuu, sisi tuna mfumo wa malt party system, kila chama chenye usajili wa kudumu kina fursa zote sawa na chama Tawala. Rais hana mamlaka ya kuvunja katiba na sheria alizoapa kzilinda na kuzisimamia, tena na kumtanguliza MUNGU AMSAIDIE KWA KUSHIKA BIBLIA. Taifa LA MUNGU ni mashahidi sote tulimsikia siku ile ya ALHAMISI ALIPOAPISHWA. TUZIDISHE MAOMBI ndio njia pekee tena Mh JPM kila siku anatuomba tumwombee naamini uwezo wa kutuepusha na kikombe hiki upo ndani ya uwezo wake, Mimi nasali BABA YETU X 100 KWA AJILI YAKE KILA SIKU.
 
Safi, viongozi wengine wa dini wasiwe wanafiki

ni wachache wanakuwa naujasiri wa kuongea ile kweli inayopingana na haki...

tatizo hao watetez au wana harakati bado wanapata misukosuko badala ya mawazo yao kufanyiwa kazi. mf. lisu, gwajima na wengne....

Nakushukuru angalau kiongozi wa dini umejitokeza na kusema neno la kuitakia nchi yetu mema bila unafiki wa CCT, TEC etc!

wale maaskofu wa eskrow sijui watakuwa upande gani na waumini wao...

" watanzania niombeni, hii kazi ya urais ni ngumu sana, najuta kwanin nilichukua fomu"

Sasa em jaribu kufanya maombi hapo ulipo, utamuombea kwa lipi na lipi hutaliombea ..?!

Unyenyekevu ni muhim sana, hasa wa kufuata taratibu na sheria ..!!


nikitathimini ya iptl, lugumi, na ufisadi mwngne wa wana ccm... labda bakwata ndio watakuwa tayari kufanya maombi!!
 
Huyu jamaa naona kaamua kutumiwa na Chadema
Hebu fikiri tena jibu lako. Wewe ni mchonganishi na amani kwako ni sawa na malaria. Ulikuwepo walipokuwa wanamtuma? Usipende sana kuuonyesha udhaifu wako wa fikra hapa kwani wakwezo wanapita humu. Utajaabika ushindwe hata kuchutamisha ubongo wako!?
 
Hebu fikiri tena jibu lako. Wewe ni mchonganishi na amani kwako ni sawa na malaria. Ulikuwepo walipokuwa wanamtuma? Usipende sana kuuonyesha udhaifu wako wa fikra hapa kwani wakwezo wanapita humu. Utajaabika ushindwe hata kuchutamisha ubongo wako!?
Watu wengne humu usiwajibu! Just ignore them
 
KAMARA Kusupa, Mwinjilisti wa makanisa ya kipentekoste hapa nchini, amesema marurufuku ya mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya upinzani iliyotangazwa na Rais John Magufuli itavuruga amani ya nchi, anaandika Pendo Omary.

Kusupa ambaye ni miongoni mwa watu walioshiriki katika harakati za kuishinikiza serikali kurejesha mfumo wa vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990, amemuandikia barua Rais Magufuli yenye kichwa cha habari; “Msimamo wako utachochea maasi”.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Kusupa amesema, kauli za Rais Magufuli ikiwemo ile kusema watakaoandamana ‘watakiona’ na kusema, ‘mimi sijaribiwi’ ni kauli zinazothibitsha namna rais huyo anavyokosa unyenyekevu wa kiuongozi.

“Ukiwa binadamu huna namna ya kuepuka majaribu, asiyejaribiwa ni Mungu pekee. Ndio maana hata mwokozi wetu Yesu alijaribiwa na pia alitufundisha kwamba tunaposali tumwombe Mungu atuepushe na majaribu.

Mheshimmiwa rais haki inayokuwezesha kuzunguka Manyoni, Singida, Nzega na Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha ukifanya mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi waliokuchagua, ni haki hiyo moja ndiyo waliyonayo Lowasa, Mbowe na wanasiasa wengine,” amesema.

Amemtaka Rais Magufuli, asiwaoneshe watanzania kwamba haki ya mwenyekiti wa CCM taifa inaanzia pale zilipoishia haki za wanasiasa wa vyama vingine kwani kufanya hivyo ni kuchochea maasi.

“Rais Magufuli anapaswa kuhakikisha, taifa halizalisahi wakimbizi kama yalivyotokea maafa ya tarehe 27 Januari, 2001 baada ya Chama Cha CUF kuandaa maandamano na Serikali kuyasambaratisha na kuchochea vurugu zilizozalisha wakimbizi, waliokimbilia nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,” amesema Kusupa.


Chanzo: Mwanahalisi
sie yetu macho
 
Back
Top Bottom