Kama kweli ungemjua MUNGU vzr usingesema maneno dhaifu,kuna nyakati MUNGU amenyanyua watu wakorofi kwa makusudi maalumu juu ya jamii au juu ya kikosi cha vita.kusema na kudhani MUNGU hua anawateua wapole na wakarimu pekee umejidanganya.
Biblia imejaa mifano lukuki ya watawala ambao pale tu walipofanya tofauti na mpango wa Mungu, aliwaadhibu mara moja. Mungu alimsifia sana Mfalme Daudi kwa sababu hata kama alianguka mara nyingi, alitubu mara moja.
Daudi alikuwa hataki hata kuwagusa "maadui wake", namzungumzia Mfalme Sauli. Huyu alipanga kumuua Daudi mara nyingi, lakini hata pale Daudi alipopewa na Mungu nafasi ya kumdhuru Sauli, alimwachia kwa kuheshimu kwamba "huyu ni mpakwa mafuta wa Mungu".
Lakini Mungu alimwadhibu Daudi pale alipomnyanyasa na mwisho kumuua Uria. Pia alimwadhibu pale alipoamua kufanya sensa kinyume cha maagizo ya Mungu. mara zote hizo Daudi alitubu. kuna ile ishu ya Shimei ambaye alimlaani Mfalme Daudi pale alipokuwa anamkimbia mwanae mwenyewe wa kumzaa, Absalom [2Sam.16:5-13]. Makamanda wa Daudi walitaka kumuulia mbali, bali Daudi akasema mwacheni, pengine katumwa na Mungu huyu, na mimi kwa kuvumilia pengine Mungu atanisamehe maovu yangu.
Ni kweli, Mungu alimwita mfalme mpagani na katili sana, Nebukadreza, "mtumishi wangu" [Yeremia 27:6] lakini kumbuka Mungu alishasema mwanzo kwamba pale atakapotumia taifa ovu kuadhibu taifa teule, hao taifa ovu wawe makini sana kutambua kwamba wasingeweza kufanya lolote kwa taifa teule, pasipo kuwezeshwa na Mungu.
lakini kwa upumbavu wao, watajiona wamefanya hayo kwa nguvu zao wenyewe, na hapo ndipo Mungu atakapowaadhibu na wao [Kumb. 32:21-36].
Kwa hiyo hata kama Mungu huwatumia pia watawala waovu ili kuadhibu taifa lake, bado hao watawala waovu imewapasa kuifuata sheria ya Mungu. imewapasa kumtambua, wafanye tu kile alichokusudia Yeye alipoamua kuwatumia, pamoja na uovu wao. hapo tu ndipo nao watakuwa salama.