Mwinjilisti amvaa Rais Magufuli, amuonya

Mwinjilisti amvaa Rais Magufuli, amuonya

Muda wa siasa ulishaisha.. Uchaguzi ukishamalizika, kinachofuata ni kazi tu.. Mbona sijaona mikutano ya siasa ikiendelea katika nchi ya uingereza, marekani, Norway, Japan, Rwanda, Sweden, uswis, Canada, baada ya uchaguzi kuisha..

Wanaopenda siasa, wanataka kutuchelewesha.. Ni bora wahame katika nchi yetu
 
Kamara Kusupa, Mwinjilisti wa makanisa ya kipentekoste hapa nchini, amesema marufuku ya mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya upinzani iliyotangazwa na Rais John Magufuli itavuruga amani ya nchi.

Kusupa ambaye ni miongoni mwa watu walioshiriki katika harakati za kuishinikiza serikali kurejesha mfumo wa vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990, amemuandikia barua Rais Magufuli yenye kichwa cha habari; “Msimamo wako utachochea maasi”.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Kusupa amesema, kauli za Rais Magufuli ikiwemo ile kusema watakaoandamana ‘watakiona’ na kusema, ‘mimi sijaribiwi’ ni kauli zinazothibitsha namna rais huyo anavyokosa unyenyekevu wa kiuongozi.

“Ukiwa binadamu huna namna ya kuepuka majaribu, asiyejaribiwa ni Mungu pekee. Ndio maana hata mwokozi wetu Yesu alijaribiwa na pia alitufundisha kwamba tunaposali tumwombe Mungu atuepushe na majaribu.

Mheshimmiwa rais haki inayokuwezesha kuzunguka Manyoni, Singida, Nzega na Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha ukifanya mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi waliokuchagua, ni haki hiyo moja ndiyo waliyonayo Lowasa, Mbowe na wanasiasa wengine,” amesema.

Amemtaka Rais Magufuli, asiwaoneshe watanzania kwamba haki ya mwenyekiti wa CCM taifa inaanzia pale zilipoishia haki za wanasiasa wa vyama vingine kwani kufanya hivyo ni kuchochea maasi.

“Rais Magufuli anapaswa kuhakikisha, taifa halizalisahi wakimbizi kama yalivyotokea maafa ya tarehe 27 Januari, 2001 baada ya Chama Cha CUF kuandaa maandamano na Serikali kuyasambaratisha na kuchochea vurugu zilizozalisha wakimbizi, waliokimbilia nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,” amesema Kusupa.

Chanzo: Mwanahalisi

Baada ya kulalamika juu ya viongozi wa dini kutoingilia ukuta Catholic ipo kimya bakwata kimya Kkkt kimya mmeona muanze kuokoteza wainjilist ili waje wawasaidie
 
MUNGU husikiliza watu wake wanataka nini,juzi hapa mmetoka kusema Rais wa kucheka cheka na wa safari hatumtaki,mala oooh hii nchi inahitaji kiongozi mkali ndo itakaa sawa,MUNGU amejibu mlichotaka tena mnarudi kulalamika.nyie ni watu gani?

Kiongozi tuliye naye si malaika. Kama kuna mahali anafanya ndivyo sivyo, lazima watu wenye mapenzi mema na nchi yao wapaze sauti, wasikike. Wengine kama wewe unaweza kunyamaza au kushangilia kila kitu afanyacho, hiyo ni haki yako na unalindwa na sheria
 
Huyo mwinjilisti sio ndio kati ya wale walio kwenda kwa Lowasa kumtembelea...
 
Aliwasemea washika bunduki lakini yeye kama binadamu anaweza kujatibiwa.
 
Kiongozi tuliye naye si malaika. Kama kuna mahali anafanya ndivyo sivyo, lazima watu wenye mapenzi mema na nchi yao wapaze sauti, wasikike. Wengine kama wewe unaweza kunyamaza au kushangilia kila kitu afanyacho, hiyo ni haki yako na unalindwa na sheria
Mwenye mapenzi mema na afanye kazi kwa bidii kukuza uchumi,siyo tantalila zisizo na maana,tukipinga mnadhani kila mtu ni ccm.waliyokua wanatutetea wamewrong kupita maelezo na ile gia ya angani na mwenye akili nzuri anatambua hlo,ila mpo msiyojua,kila mnachoambiwa na wachumia tumbo unakiamini na mnapiga kelele,hakuna muda wa siasa kuna muda wa kazi tu sasa hv,leteni nyuzi za kubadilishana mawazo namna ya kukuza uchumi wetu na siyo kila siku kukosoa tu hata penye hamna.uongozi uko sawa tatizo ni waTanzania kua wazito kuelewa na kuwa na mapenzi na vyama.mnaowaamini wamecheza karata ambayo hata mtoto mdogo angeweza kuwaelewa,na waliyowah kuyapigia kelele ndo RAIS wetu wa nchi anashughulika nayo pia,sasa hv mtatuambia nini tuwasikilize?eti UKUTA!!!!!MWEH..wewe ndo kaa kimya rafiki
 
Ni wakati WA kufanya kazi tusubiri siasa mpaka 2020 Full stop
 
Nakushukuru angalau kiongozi wa dini umejitokeza na kusema neno la kuitakia nchi yetu mema bila unafiki wa CCT, TEC etc!

Mwinjilisti Kamala Kusupa, nimemkubali. Juzi nilimsikia akihojiwa na StarTv kwenye kipindi kinachosimamiwa na Dotto Bulendu wakishirikiana na Angalieni Mpendu. Kusupa ni mtu mkweli, mnyenyekevu, mwenye hofu ya Mungu na anayemtakia mema Rais na nchi hii.
Huu ndiyo uongozi wa Kidini unaotakiwa na si sawa na viongozi wengine wa kidini wamejaa unafiki wa KUMSIFIA RAIS KWA KUVUNJA KATIBA huku wakiwaponda wapinzani kwa kutaka kufanya maandamano!!!

Mimi nimesikitika sana kwa kuona viongozi wengi wa dini wanakuwa wanafiki kwa kujikomba kwa Rais na kujidai kumwombea ilhali ANAVUNJA KATIBA. Biblia inasema MUNGU HASIKIII MAOMBI YA MNAFIKI hata siku moja. HAIWEZEKANI RAIS AVUNJE KATIBA KWA KUZUIA MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA NA MAANDAMANO KWA KUANDAA POLISI ILI KUZUIA MIKUTANO KWA MABOMU NA RISASI ZA MOTO. KATU MUNGU HAWAWEZI KUBARIKI UPUUZI KAMA HUO.

Hii inanikumbusha ile hadithi ya Mfalme aliyekuwa amedanganywa kwa kuvalishwa VAZI HEWA LISILOONEKANA HUKU AKIAMINI AMEVAA. Watu waliokuwa karibu naye wakiwa wamejaa unafiki WALIANZA KUMSIFIA NA KUMPONGEZA ATI KAPENDEZA ILHALI WAKIJUA MFALME YUKO UCHI WA MNYAMA!!! Ndipo akatokea mtoto mdogo akawaambia MBONA MIMI NAONA MFALME YUKO UCHI JAMANI, HIYO NGUO ALIYOVAA IKO WAPI????Ndipo watu wakawa kama wameshtuliwa toka usingizini wakaanza kusema, 'OH KWELI MFALME YUKO UCHI, ilibidi waungwana wamstili kwa kanzu ili kuondoa aibu.

Hadithi hiyo haina tofauti anachofanya Rais Magufuli kwa sasa. Watu wa Serikali na Chama chake cha CCM walio karibu naye HAWATAKI KUMWAMBIA UKWELI KUWA ANAVUNJA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KWA KUZUIA MIKUTANO NA MAANDAMANO YA VYAMA VYA SIASA KWA KISINGIZIO CHA ''HAPA KAZI TU''. Huu ni unafiki uliopitiliza na matokeo yake ni damu kumwagika. Kama Watanzania kwenye nchi yao Huru wameamua kuandamana na kufanya mikutano kama Katiba na sheria inavyowaruhusu wewe unawazuia kwa kutumia sheria na Katiba ipi? Hapa ndipo penye tatizo, ina maana Rais badala ya kuzuia vurugu kwa kuwaambia Polisi waruhusu Mikutano na Maandamano na wahakikishe wanatoa ulinzi wa uhakika yeye ndiyo anakuwa wa kwanza kuwaamurisha Polisi kuwa atakaye andamana ATAKIONA CHA MTEMA KUNI.........!!!!!!Hii ni kauli ambayo haikutakiwa kabisa kutoka kwenye kinywa cha Rais anayejua unyeti na uzito wa Ofisi ya Rais. Vinginevyo huyo Rais hajui nini maana ya kuwa Mkuu wa nchi......!!!!

Rais amayejua majukumu yake, unyeti wa Ofisi ya Rais na mzigo alioubeba wa kusimamia HAKI NA USTAWI WA WATANZANIA TAKRIBANI MILIONI 50 HAWEZI KUTOA LUGHA KAMA HIYO. Baba wa Taifa enzi za uhai wake aliwahi kutamka kuwa IKULU NI MZIGO, IKULU SI MAHALI PA KUKIMBILIA unless mtu hajui nini maana ya kuwa Rais. Katika nchi za wenzetu Rais anathamini uhai wa kila raia wake na ikitokea hata Mwannachi mmoja kapoteza uhai inakuwa ni maumivu kwa Rais kwanini hakusaidia kuokoa uhai wa raia huyo!

Leo Rais wetu anaandaa JESHI LA POLISI kupambana na Raia wasio na hatia kisa wameamua kutumia haki yao kikatiba kuandamana na kufanya mikutano tu!!! Lazima Watanzania tuache unafiki na tumwambia Rais ukweli kuwa hajavaa nguo, yuko uchi na hapendezi na hivo lazima avalishwe nguo za kumstiri aibu yake.
 
Mwinjilisti Kamala Kusupa, nimemkubali. Juzi nilimsikia akihojiwa na StarTv kwenye kipindi kinachosimamiwa na Dotto Bulendu wakishirikiana na Angalieni Mpendu. Kusupa ni mtu mkweli, mnyenyekevu, mwenye hofu ya Mungu na anayemtakia mema Rais na nchi hii.
Huu ndiyo uongozi wa Kidini unaotakiwa na si sawa na viongozi wengine wa kidini wamejaa unafiki wa KUMSIFIA RAIS KWA KUVUNJA KATIBA huku wakiwaponda wapinzani kwa kutaka kufanya maandamano!!!

Mimi nimesikitika sana kwa kuona viongozi wengi wa dini wanakuwa wanafiki kwa kujikomba kwa Rais na kujidai kumwombea ilhali ANAVUNJA KATIBA. Biblia inasema MUNGU HASIKIII MAOMBI YA MNAFIKI hata siku moja. HAIWEZEKANI RAIS AVUNJE KATIBA AZUIE MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA NA MAANDAMANO KWA KUANDAA POLISI KUZUIA MIKUTANO KWA MABOMU NA RISASI ZA MOTO. KATU MUNGU HAWAWEZI KUBARIKI UPUUZI KAMA HUO.

Hii inanikumbusha ile hadithi ya Mfalme aliyekuwa ameambiwa atembee Uchi kwa kuvalishwa VAZI HEWA LISILOONEKANA HUKU AKIUAMINI AMEVAA. Watu waliokuwa naye karibu wakiwa wamejaa unafiki WALIANZA KUMSIFIA NA KUMPNGEZA KWA JINSI ALIVYOPENDEZA ILHALI MFALMEYUKO UCHI WA MNYAMA!!! Ndipo akatokea mtoto mdogo akawaambia MBONA MIMI NAONA MFALME YUKO UCHI, HIYO NGUO ALIYOVAA IKO WAPI????Ndipo watu wakawa kama wameshtuliwa toka usingizini wakaanza kusema, 'OH KWELI MFALME YUKO UCHI, ilibidi waungwana wamstili kwa kanzu na ili kuondoa aibu.

Hadithi hiyo haina tofauti anachofanya Rais Magufuli kwa sasa. Watu wa Serikali na Chama chake cha CCM walio karibu naye HAWATAKI KUMWAMBIA UKWELI KUWA ANAVUNJA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KWA KUZUIA MIKUTANO NA MAANDAMANO YA VYAMA VYA SIASA KWA KISINGIZIO CHA ''HAPA KAZI TU''. Huu ni unafiki uliopitiliza na matokeo yake ni damu kumwagika. Kama Watanzania kwenye nchi yao Huru wameamua kuandamana kama Katiba na sheria inavyowaruhusu wewe unawazuia kwa kwa kutumia sheria na Katiba ipi? Hapa ndipo kuna tatizo, ina maana Rais badala ya kuzuia vurugu kwa kuwaambia Polisi waruhusu na kutoa Ulinzi kwenye Mikutano na Maandamano yeye ndiyo anakuwa kuwaamurisha Polisi atakaye aandamana ATAKIONA CHA MTEMA KUNI.........!!!!!!Hii kweli ni inaweza kuwa kauli ya Rais anayejua unyeti na uzito wa Ofisi ya Rais????
Natilia shaka sana......!!!!

Rais amayejua majukumu yake, unyeti wa Ofisi ya Rais na mzigo alioubeba wa kusimamia HAKI NA USTAWI WA WATANZANIA TAKRIBANI MILIONI 50 HAWEZI KUTOA LUGHA KAMA HIYO. Baba wa Taifa enzi za uhai wake aliwahi kutamka kuwa IKULU NI MZIGO, IKULU SI MAHALI PA KUKIMBILIA unless mtu hajui nini maana ya kuwa Rais. Katika nchi za wenzetu Rais anathamini uhai wa kila raia wake na ikitokea hata Mwannachi mmoja kapoteza uhai inakuwa ni maumivu kwa Rais kwanini hakusaidia kuokoa uhai wa raia huyo!

Leo Rais wetu anaandaa JESHI LA POLISI kupambana na Raia wasio na hatia kisa wameamua kutumia haki yao kikatiba kuandamana na kufanya mikutano tu!!! Lazima Watanzania tuaxhe unafiki na tumwambia Rais ukweli kuwa hajavaa,hapendezi na yuko uchi hivo lazima avalishwe nguo za kumstiri aibu yake.
CCT, BAKWATA na TEC walaaniwe na shetani! Wanafiki, wanaogopa kusema ukweli. Eti wanamuombea, labda kwa shetani!
 
Daima damu y watanzania itakuw juu ya kichwa chake mwenyew mtawal mbaya
 
Hilo gazeti lifungiwe. Hayo matamshi hakuyatoa mwinjilist ( Fuatilieni video clip). Ni maneno ya mjanjamjanja mmoja mwenye nia ya kumchafua mwinjilist aliyetoa ushauri mzuri na wenye hekima.
Narudia.;- Gazeti lichunguzwe, hatua stahiki za kisheria zichukue mkondo wake
 
Mwenye mapenzi mema na afanye kazi kwa bidii kukuza uchumi,siyo tantalila zisizo na maana,tukipinga mnadhani kila mtu ni ccm.waliyokua wanatutetea wamewrong kupita maelezo na ile gia ya angani na mwenye akili nzuri anatambua hlo,ila mpo msiyojua,kila mnachoambiwa na wachumia tumbo unakiamini na mnapiga kelele,hakuna muda wa siasa kuna muda wa kazi tu sasa hv,leteni nyuzi za kubadilishana mawazo namna ya kukuza uchumi wetu na siyo kila siku kukosoa tu hata penye hamna.uongozi uko sawa tatizo ni waTanzania kua wazito kuelewa na kuwa na mapenzi na vyama.mnaowaamini wamecheza karata ambayo hata mtoto mdogo angeweza kuwaelewa,na waliyowah kuyapigia kelele ndo RAIS wetu wa nchi anashughulika nayo pia,sasa hv mtatuambia nini tuwasikilize?eti UKUTA!!!!!MWEH..wewe ndo kaa kimya rafiki

Hivi ulikusudia kusema nini? Kabla ya ku-post maoni yako, jaribu kusoma tena na tena. Pili jaribu kuelewa post ya mwenzako kabla ya kujibu.
 
Kama kuna mtu atajiita "Kiongozi wa dini" halafu haioni na kuitenda haki basi huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu. Kiongozi wa dini ni mwangalizi wa haki na Usawa na anapaswa Kunena juu hayo kila sekunde ya Uhai wake.
 
Mchungaji gani asiyejua mamlaka iliyopo inatambuli mpaka kwa MUNGU?hajielewi huyo,wala kwenye uzi huu sirudi tena
Tatizo la uzezeta ni kubwa kuliko tunavyofikiri..... hata huyu .....anaona amechambua hoja ya mchungaji!
 
Tatizo la uzezeta ni kubwa kuliko tunavyofikiri..... hata huyu .....anaona amechambua hoja ya mchungaji!
Tatizo la watu waliozaliwa na mtindio wa ubongo ni kubwa kuliko tunavyofikiri.....hata huyu....anajiona anajua na hajui kitu
 
Back
Top Bottom