Mwijaku ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Machawa wa Rais Samia kwa Mkoa wa Dar es Salaam

PureView zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
9,088
29,847
Mwijaku ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Chawa wa Mama Mkoa wa Dar es Salaam.

IMG_6605.jpeg

Mtanzania maarufu wa Kituo Cha Redio kongwe nchini Clouds FM Mwemba Burton almaarufu kama Mwijaku ametangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chawa wa Mama Mkoa wa Dar Es Salaam.

Katibu wa Chawa wa Mama Taifa Neema Karume amesema kuwa uteuzi huo umekuja baada ya Mwijaku kukidhi vigezo vya kuwa na nguvu ya uhamasishaji katika masuala ya Chama na Serikali na jamii nzima kwa ujumla.

Uteuzi huo umefanyika Aprili Mosi mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam.

"Tunamkaribisha sana ili tuungane kwa pamoja kuyasema yale yote mazuri anayoyafanya Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan hakika mama amefanya makubwa hatuna budi kumuunga mkono katika juhudi zake zote" amesema Katibu wa Chawa wa mama Taifa Neema Karume.

Katibu huyo wa Chawa Taifa Neema ameongeza kwa kusema kuwa kundi la Chawa wa Mama linaundwa na watu kutoka kada mbalimbali nchi nzima huku akiyataja baadhi yao makundi hayo kuwa ni Madereva wa Bodaboda, Madereva Taxi, Mabasi ya Abiria, Mama Lishe ,Wakulima, Wafugaji, Wafanyabiashara wakubwa na Wamachinga, Wasusi, Wavuvi, Wanasiasa, Wanafunzi wa Vyuo, Waalimu, Wakurugenzi katika taasisi mbalimbali Wafanyakazi wa Serikali na Taasisi binafsi na Watanzani waliopo nje ya nchi ( DIASPORA).

Neema amesema kuwa lengo la kundi la Chawa wa Mama ni kuhakikisha wanakuwa Mabalozi wazuri ndani na nje ya nchi kwakuyasemea mazuri yanayotekelezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 wanaweka historia kwa Rais Dkt. Samia Hassan kuliongoza taifa katika awamu ya saba.

Chanzo: Haki Ngowi
 
Japo mdudu chawa siyo mzuri mpaka kwenye afya sababu anaishi mazingira machafu, ila hilo jina ndiyo zuri sana kwa hao wahusika, sisi tunaoliona baya ni hatujui kwa nini kwao ni zuri.

a) Chawa ananyonya damu; hawa machawa wanajitengenezea njia ya kutunyonya watanzania kwa mgongo wa kumsifia mama kwa mazuri.

b) Issue ya kumsifia mama ina kitengo maalum na wala wana ccm hawahitaji wadudu wachafu kufanya hiyo kazi, ila wao wameona fulsa mpya ya kula ndiyo maana wamebuni huu ulaji.

Yetu macho, masikio, mengine tupo hapa tunaendelea kujifunza tabia ya mwanadamu!.
 
Daah hizi mambo bhana
Yaan Rais yupo vizuri ila hawa wa pembeni ni kama wanadharirisha taasisi ya Urais
Sasa chawa tafsiri yake ni uchafu na hukaa humo na kuzaliana
Aiseh it carries negative perception
Neno paa lina maana zaidi ya moja halikadhalika neno paka, hiyo ni mifano michache tu hivyo hata neno chawa linaweza kurasimishwa katika hii maana inayotumika sasa na vijana.
Pamoja na kufafanua hivyo lakini hizo tabia za uchawa(kujipendekeza) sikubaliani nazo.
 
Mwijaku ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Chawa wa Mama Mkoa wa Dar es Salaam.

View attachment 2576622

Mtanzania maarufu wa Kituo Cha Redio kongwe nchini Clouds FM Mwemba Burton almaarufu kama Mwijaku ametangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chawa wa Mama Mkoa wa Dar Es Salaam.

Katibu wa Chawa wa Mama Taifa Neema Karume amesema kuwa uteuzi huo umekuja baada ya Mwijaku kukidhi vigezo vya kuwa na nguvu ya uhamasishaji katika masuala ya Chama na Serikali na jamii nzima kwa ujumla.

Uteuzi huo umefanyika Aprili Mosi mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam.

"Tunamkaribisha sana ili tuungane kwa pamoja kuyasema yale yote mazuri anayoyafanya Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan hakika mama amefanya makubwa hatuna budi kumuunga mkono katika juhudi zake zote" amesema Katibu wa Chawa wa mama Taifa Neema Karume.

Katibu huyo wa Chawa Taifa Neema ameongeza kwa kusema kuwa kundi la Chawa wa Mama linaundwa na watu kutoka kada mbalimbali nchi nzima huku akiyataja baadhi yao makundi hayo kuwa ni Madereva wa Bodaboda, Madereva Taxi, Mabasi ya Abiria, Mama Lishe ,Wakulima, Wafugaji, Wafanyabiashara wakubwa na Wamachinga, Wasusi, Wavuvi, Wanasiasa, Wanafunzi wa Vyuo, Waalimu, Wakurugenzi katika taasisi mbalimbali Wafanyakazi wa Serikali na Taasisi binafsi na Watanzani waliopo nje ya nchi ( DIASPORA).

Neema amesema kuwa lengo la kundi la Chawa wa Mama ni kuhakikisha wanakuwa Mabalozi wazuri ndani na nje ya nchi kwakuyasemea mazuri yanayotekelezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 wanaweka historia kwa Rais Dkt. Samia Hassan kuliongoza taifa katika awamu ya saba.

Chanzo: Haki Ngowi
Hii nchi vituko mingi sana
 
Back
Top Bottom