Mwigulu umedhalilisha Taaluma ya Ualimu

Mwigulu umedhalilisha Taaluma ya Ualimu

Kukusaidia Bw Makalla ni kwamba hao anaowataja Mwigulu, wanaweza ku instruct na sio kufundisha. Level ya Primary na sekondari ni total teaching na siyo instructing, hivyo mwanasheria au mhandisi hawawezi kamwe kufundisha. Hapo baba ni mpaka ujue kitu kinaitwa pedagogy of education, philosophy of education, curriculum and education, educational evaluation, standardization of marks, etc

Bila kusahau Foundation of Education Development (FED)
 
Lecturer ni instructor siyo teacher plse tofautisha.Nadhani tunakuwa wavivu mno wa kujisumbua kujua mambo.
tatizo hapa kwetu kwa kiswahili tunarahisisha kuwaita malecturer waalimu, hatuoni hiyo tofauti......
kwa maoni yangu mwalimu ni zaidi ya lecturer, nawaheshimu sana walimu
 
Wana jf tunaweka chuki tunapochambua hoja ya mwigulu. Hili wazo ni mhimu sana kwani amesema kuliko kusubiri walimu mpsks wamalize ndio waajiriwe ni bora kuwachukuwa wataalam ambao wapo tu hawana kazi. Lipi bora mwsnsfunzi kujisomea hesabu au kufundishwa na mhandisi. Acheni kuwaza kizamani na chuki ndani

Mbona wapo wengi tuu ambao hawajaajiriwa?
 
Walimu wenyewe washaacha kazi zamaani,
wamebaki na ajira tuu.

saivi walimu wanapongezana kufali kwa hile asilimia 90, ukifika shure story na kusaini out good day subilia asilimia 99 saivi
 
kutokana na maelezo yako unamaanisha hao watalipwa zaid ya walimu coz elimu yao ni quality kuliko ya walimu au na hiyo itakua n serikali ya jk au ya nan?
...endapo mishahara ya walimu ingekuwa mizuri, leo hii wale wanaopata marks za juu ndio wangekuwa wanakwenda Ualimu, ila kwa sababu mishahara ya Walimu ni duni ndio maana sasa watu wanaoenda Ualimu ni wale wenye marks za chini, solution hapa ni kwanza kuwaondoa walimu vilaza wasio na uwezo, kama Mwalimu wa hesabu niliyemshuhudia anayewafundisha Wanafunzi -2 - -6 = -8; baada ya kuondoa hawa, maslahi ya Walimu yapandishwe, ili likifanyika automatically watu wenye sifa stahiki wataenda Ualimu...
 
Hivi chuo cha Ma-lecturers kiko wapi vile?

wew mtu nikwambie basi kwani hujui ni sababu gani inafanya vyuo vikuu kua na Autonomy zao!? ni kwasababu hakuna pakupatia mwongozo wa kielimu juu ya hapo! Kungekua na vyuo vyenye kufundishia ma_Lecturer, basi ingetoa hata sababu ya kua na National Exam kama certificate na Diploma!
 
Sha Makala
Lipi bora mwsnsfunzi kujisomea hesabu au kufundishwa na mhandisi. Acheni kuwaza kizamani na chuki ndani

Mkuu, moja ya sababu ya kufeli kidato cha nne ni upuuzi kama huu wa kudhani kwamba kila mtu anaweza kufundisha. Unakumbuka walimu wa "voda fasta?" Kwa taarifa yako bado wapo mashuleni huko sekondari na wanafanya kazi nzuri tu ya kufelisha wanafunzi, kuwafundisha "u-check bob" na upuuzi mwingi tu kwa sababu hawana taaluma ya kufundisha (pedagogy). Afu serikali inaunda tume!
 
Mwigulu Taaluma ya Ualimu ni Taaluma kama Taaluma zingine,Unaposema kila Mtu mwenye Shahada ana uwezo wa kufundisha unakosea tena sana.Kuna kitu kwenye ualimu kinaitwa Pedagogy of Teaching.

Kufundisha ni Taaluma unayotakiwa usomee,mtu kama injinia asiye jua hata moja kuhusu Preparation of Teaching,Teaching Aids,Leason Plan,Scheme of work atafundisha vipi?,we unafikiri kufundisha ni kujua tu kilichopo kwenye Vitabu?,We mbunge unamasiala sana wewe.
Alaa kumbe! Ndo maana wanawadharau walimu. Wanadhani ni biashara ya kila mtu. Foolish.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hata hawa ni walimu

ndugu, lecturer sio mwalimu, lecturer anaelekeza tu hana lesson plan, anaweza kutoa mwelekezo tu alaf watu wakaenda kujiandalia maelezo/notisi...lectuer na mwalimu ni vitu tofauti unless tunataka kuingiza siasa.

Nchemba kama jina lake ana matatizo makubwa au ya kisiasa au kifamilia au kisaikologia. Kama nchemba aposipoangalia baadae atakuwa ndicho chanzo cha kufa kwa taifa la Tanzania. Wameshindwa kumlipa mwalimu hata milioni moja basic, leo wanataka mwanasheria ambaye kwa std ya kawaida iyo ni travelling allowance ya siku mbili na nusu, anataka injinia akafundishe secondary kwa masilahi yepi? Ukitaka mwanasheria akafundishe secondary basi tuache forces of demand and supply zifanye kazi in a way mwanasheria aamuke mwenyewe akaombe ila kulazimishana hatuendi popote..Nchemba na boss wake hawaelewani na walimu mpaka matokeo yanakuwa ya ajabu, wanangoa madaktari meno.............iweje wawatake wanasheria?wajaribu waone kama hapatachimbika.
 
Mwigulu machemba na wafuasi wake wamekuwa na fikra mgando. Sikushangazwa na kauli yake aliyoitoa mithili ya bata anapoharisha.😡
 
Mkuu, moja ya sababu ya kufeli kidato cha nne ni upuuzi kama huu wa kudhani kwamba kila mtu anaweza kufundisha. Unakumbuka walimu wa "voda fasta?" Kwa taarifa yako bado wapo mashuleni huko sekondari na wanafanya kazi nzuri tu ya kufelisha wanafunzi, kuwafundisha "u-check bob" na upuuzi mwingi tu kwa sababu hawana taaluma ya kufundisha (pedagogy). Afu serikali inaunda tume!
...mmekazana na pedagogy badala ya msingi wa kufundisha, kujua kwa umakini somo unalolifundisha, hapo ndipo kulipo na tatizo kuliko taaluma ya kufundisha, huwezi ukamtegemea mwalimu failure awatoe wanafunzi wazuri, hapa ndipo palipo na tatizo na wala sio abc za Ualimu......Enzi nasoma nimefundishwa na watu ambao hawajui hizo taaluma za ualimu lakini wapo deep kwenye masomo husika, na believe me, hawa wanasaidia sana huko mitaani kuliko walimu vilaza walioko mashuleni......Kwa lugha rahisi, ni heri mwanafunzi afundishwe mathematics na mtu mwenye uwezo wa A ya mathematics japo hana taaluma ya ualimu kuliko kuwa na Mwalimu mwenye taaluma ya Ualimu lakini mwenye uwezo wa E ya Mathematics....
 
ndugu, lecturer sio mwalimu, lecturer anaelekeza tu hana lesson plan, anaweza kutoa mwelekezo tu alaf watu wakaenda kujiandalia maelezo/notisi...lectuer na mwalimu ni vitu tofauti unless tunataka kuingiza siasa.

Nchemba kama jina lake ana matatizo makubwa au ya kisiasa au kifamilia au kisaikologia. Kama nchemba aposipoangalia baadae atakuwa ndicho chanzo cha kufa kwa taifa la Tanzania. Wameshindwa kumlipa mwalimu hata milioni moja basic, leo wanataka mwanasheria ambaye kwa std ya kawaida iyo ni travelling allowance ya siku mbili na nusu, anataka injinia akafundishe secondary kwa masilahi yepi? Ukitaka mwanasheria akafundishe secondary basi tuache forces of demand and supply zifanye kazi in a way mwanasheria aamuke mwenyewe akaombe ila kulazimishana hatuendi popote..Nchemba na boss wake hawaelewani na walimu mpaka matokeo yanakuwa ya ajabu, wanangoa madaktari meno.............iweje wawatake wanasheria?wajaribu waone kama hapatachimbika.
umesomeka mkuu
 
Mwigulu mimi hata aseme kibaya gani nitamsamehe tu kwa sababu najua ndio alivyo na hata ufanyeje hawezi kubadilika. Tukubali kuwa Mungu alimuumba akiwa kichwa maji basi.

A very Big No ! Maana Mwenyezi alimuumba kila binadamu kwa mfano wake , kumbe ni kwamba Mungu hakuumba Wajinga Maana si Mfano wa Mungu ! Huyu atanyooka tu , ni suala la muda tu , kuwa karibu na Rais hakumfanyi mtu yeyote kujivunjia tu sheria anavyotaka , time will tell , juzi nilimkumbusha huyu Mwigulu kwamba hebu amtupie jicho Seif al Islam , ambaye zaidi ya nusu ya uhai wake atanyea ndoo .
 
Unapowataka watu wasiosomea taaluma ya ualimu waingie darasani kufundisha hakuna tofauti sana na ile crash program iliyoshindwa na kwa kweli ndiyo inayozidi kuleta matokeo haya tunayoyaona leo.

Mwigulu Nchemba ametudhihirishia kwamba, jahazi la serikali yake (CCM) linazama, serikali imekuwa mfa maji, wanataka kujiokoa kwa kushikilia majani badala ya maboya au magogo.

Serikali ikiri, imekosa vision ya muda mrefu katika elimu, na kama ipo basi utashi wa kuifuata haupo.
 
Back
Top Bottom