Mwigulu umedhalilisha Taaluma ya Ualimu

Mwigulu umedhalilisha Taaluma ya Ualimu

Nadhani Mhe Nchemba amekurupuka,anayopendekeza yalishawahi fanyika huko nyuma,ingekuwa vema kabla ya kuchangia akauliza kwanini serikali iliacha kuajili wahitimu wa fani zisizo za ualimu wa vyuo vikuu kuwa walimu.Mwalimu huwa amekamilika kufundisha somo husika,kama anazo elimu zifuatazo.
  1. Common Content Knowledge-ajue somo husika
  2. Specialized Content Knowledge-awe na mbinu za kuwasilisha somo kwa mwanafunzi
  3. Knowledge at Content Horizon-awe na elimu ya ziada ya somo husika,ajue mizizi ya kila mada
  4. Knowledge of Content and Student-awajue wanafunzi vyema,wanavyofikiri,wanavyokosea na namna ya kuwasaidia
  5. Knowledge of Content and Teaching-ajue taaluma ya ufundishaji akizingatia learners centres approach
  6. Knowledge of Content and Curricullum-aelewe vyema masuala yote yanayoihusu mitaala ya somo husika.
Rejea Prof Ball and Bass,(2009) Michigan University;Mathematical knowledge for teaching.Pamoja na utaalam huo unauhusu utaalamu wa uwasilishaji mitaala,mwalimu hufundishwa masomo mengine kama,psychology ya mwanadamu,sociology,philosophy na masuala ya uongozi na mipango.

Mtu asiyesomea ualimu atakuwa na Domain moja tu,COMMON CONTENT KNOWLEDGE basi.Atawaanda wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani na sio kupata elimu.Matokea ya kukariri badala ya kuelewa ndiyo yanayosababisha kupata wasomi uchwara kama Mhe Nchemba.Utafiti ulioendeshwa na wizara ya elimu wakati huo,ulionyesha mapungufu makubwa kwa wahitimu wa vyuo vikuu wasiosomea ualimu katika ufundishaji,ndio maana serikali ilisimamisha kabisa ajila kwa wahitimu wa vyuo wasio waalimu.Waliokuwa wameajiliwa walipelekwa vyuo vya ualimu wakasomee masomo ya ualimu.Serikali pia ilishauriwa kuongeza muda wa masomo ya shahada ya ualimu kuwa miaka 4 au 5 badala ya 3 iliyopo sasa.Kwa waliopo kazini ilipendekezwa mafunzo kazini yaendeswe mala kwa mala.Bahati mbaya serikali sikivu ya CCM haikufanya hivyo, ndio maana Mhe Sugu kasema serikali ya CCM ni ya wapumbavu.

Yapo mambo mengi yanayoporomosha elimu nchini,yamewekwa wazi kwenye riport ya 2010,kayasome Mhe,unachojaribu kupendekeza ni kitanzi kwa elimu nchini,labda ungeshauri watu hao wapelekwe vyuo vya ualimu kwanza ndipo waajiriwe.Kishauri chama chako cha CCM,kisiidharau elimu,itakuja kukiangamiza.NAWASILISHA
 
kwani shule za kata zina nini! Au unataka kujishaua, we changia mada hayo mengine kama huyajui achana nayo....kumbe kina mwigulu msiojua mambo mko wengi

waliosoma shule za kata zooote wana uelewa finyu sana wa kufikiri, hivi wengine wanadhani kila mwenye DEGREE wanaweza kuwa walimu......NO!! Ndio wanaokubali kufundishwa tuition na kila mtu ambae wanasikia kapitia chuo kikuu kumbe sio. lol
 
Wana jf tunaweka chuki tunapochambua hoja ya mwigulu. Hili wazo ni mhimu sana kwani amesema kuliko kusubiri walimu mpsks wamalize ndio waajiriwe ni bora kuwachukuwa wataalam ambao wapo tu hawana kazi. Lipi bora mwsnsfunzi kujisomea hesabu au kufundishwa na mhandisi. Acheni kuwaza kizamani na chuki ndani
Sawa Mwigulu Nchema Jr
 
Mwigulu Nchembe ni kichaa,zezeta na ana mtindio wa ubongo!

Hakuna mtu makini nanweza kuongea maneno ya kijinga na viteno anavyofanya huyu jamaa.

Atakiwa apelekwe Mirembe Hospital very fast!!!
 
we mburula kweli. unafikiri mwigulu ameongelea walimu wa primary? hao wenye shahada watashindwaje kuandaa lesson plan na scheme of work?

Hata wewe unaweza kuwa mburara, unafikiri kila mwenye shahada ya kitu chochote anaweza kuandaa SCHEME OF WORK NA LESSON PLANS?
 
Mwigulu Nchembe ni kichaa,zezeta na ana mtindio wa ubongo!
Hakuna mtu makini nanweza kuongea maneno ya kijinga na viteno anavyofanya huyu jamaa.
Atakiwa apelekwe Mirembe Hospital very fast!!!
Chagueni watu wa kuja MIREMBE sio Mwigulu
kuna MTU aliyelalmika sana OO NIMEIBIWA KURA LORRY ZIMA LIPO MBEYA
KUNA MTOTO WA KIONGOZI WA JUU KAKAMATWA NA MADAWA

Mlianza na NAPE
 
Sio kila mwenye shahada anaweza kufundisha.
"kunguru pia ni ndege ila hapandishi abiria"
Amka wewe!!!
 
Hivi chuo cha Ma-lecturers kiko wapi vile?

Lu-ma-ga amekujibu vizuri. Hata hivyo, in many PhD programs in the US etc., students are trained as teachers and researchers because they are expected to take up jobs in the academia.
 
Hivi chuo cha Ma-lecturers kiko wapi vile?

Mheshimiwa Speaker lecturer sio mwalimu. Lecturer ni mhadhiri. Wana tofauti kubwa hao. Mleta uzi anaongelea taaluma ya ualimu.
 
Last edited by a moderator:
Mwigulu ni MR KNOW ALL, Bila shaka kuna siku atakwaa kisiki kwa wakubwa wenzie maana for the time being anaona wenzake wasiokuwa karibu na Kikwete si mali kitu.
Dah.. Nimepata shida sana kusoma hii font kwenye hii simu yangu. Asante kwa mawazo yako...
 
Kuna wajinga kama Mwigulu wanajua kazi ya mwalimu ni darasani tu! Mwalimu ni mlezi, mshauri, mpatanishi! Psychology and Philosophy havifundishwi bure. Mjinga sana Mwigulu Nchemba
 
Last edited by a moderator:
Hivi chuo cha Ma-lecturers kiko wapi vile?
Lecture ni kijisehemu tu katika namna za ufundishaji.Hata hivyo wataalamu wa elimu wanapiga vita matumizi ya lecture kwenye level za msingi na sekondari.
 
Walimu wliopo na wnye sifa wameshindwa kulipwa maslahi ya kukidhi kuendesha maisha yao hoa mainjinia watalipwa kwa kupewa matofali au mawe ya kuokotwa barabarani? mwigulu asamehewe na co kosa lake nahic kafundishwa na walimu wa UPE wa enzi izo
 
ELimu isiyo na mitaala ni fujo tupu.Hii ni kithibitisho kuwa hatuna hata sifa ya wanaofaa kufundisha watoto wetu.Mwigulu ni kansa kwa serikali ya CCM.Tiba yake ni mionzi.
 
Mwigulu Taaluma ya Ualimu ni Taaluma kama Taaluma zingine,Unaposema kila Mtu mwenye Shahada ana uwezo wa kufundisha unakosea tena sana.Kuna kitu kwenye ualimu kinaitwa Pedagogy of Teaching.

Kufundisha ni Taaluma unayotakiwa usomee,mtu kama injinia asiye jua hata moja kuhusu Preparation of Teaching,Teaching Aids,Leason Plan,Scheme of work atafundisha vipi?,we unafikiri kufundisha ni kujua tu kilichopo kwenye Vitabu?,We mbunge unamasiala sana wewe.
binafsi naona mwigulu yuko sahihi, kama unaibu waziri wa elimu anapewa mtu mwenye elimu ya kuungaunga na kufoji vyeti, kwa nini mtu yeyote asiweze kufundisha? Ccm ni janga kwa taifa letu!
 
Hayo ndio madhara ya kuiba vyeti na majina ya watu ktk elimu,mwigulu ni kilaza hasa
 
Mwigulu alisema kama temporary plan hakumaanisha ndiyo iwe hivyo!Halafu mimi nina rafiki yangu alimaliza chuo kikuu SUA shahada ya Kilimo katika kuhangaikia ajira akaajiriwa shule ya serikali, trust me katika mwaka wake wa pili wa kufundisha alikuwa ni miongoni mwa walimu Tanzania aliopewa zawadi na wizara kwa kutoa wanafunzi bora kwenye somo la Agriculture form six!!

Binafsi CCM siwapendi lakini wazo la Mwigulu limekwenda shule kwa upande wangu.
 
Back
Top Bottom