Mwigulu: Si kila mwenye miaka 18 atalipa kodi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
1655509170252.png

Picha> Waziri wa Fedha Mwigullu Nchemba akiwa ameshika kipaza sauti

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kodi haitotazwa kwa kila mtu mwenye umri wa miaka 18, bali atatozwa mtu mwenye kipato ambacho kinaangukia wigo unaotakiwa kutozwa kodi.

Waziri Mwigulu amezungumza hayo ili kuwaondoa hofu wananchi kufuatia kauli ya ulipaji kodi kwa wenye umri wa mika 18 iliyotolewa katika bajeti ya 2022/23 Juni 14 bungeni Dodoma.

“Kuhusu kodi haitozwi kila mtu, anatozwa mwenye kipato, kwa hiyo mtu mwenye kipato ndiye anayetozwa kodi sio mtu mwenye kitambulisho cha taifa. Kitambulisho cha taifa ni utambuzi lakini kodi anatozwa yule mwenye kipato, watu wasipate hofu sisi, tunawarahisishia,” amesisitiza Mwigulu Nchemba.

Aidha, amesema kuhusu namba ya utambulisho ya mlipa kodi kwa mtu ambaye anataka kuanzaisha biashara asisumbuliwe kuandikisha taarifa zake upya bali taarifa ziunganishwe kwenye kitambulisho chake cha taifa.

Pia soma:
1. Serikali: Kila Mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi
2. Zitto Kabwe: Waziri afafanue kodi aliyoitangaza, kodi hailipwi na mtu
 
Uongo Mtu Atajuaje Mwenye Kipato​

Mbona Walishindwa Kuunganisha Leseni Ya Udereva Na Kitambulisho Cha Kupigia Kura Wakakomaa Kutoa Nida. Hiyo Ni Janja Pia Hana Ubunifu Wowote
 
View attachment 2264277

Rebeca 83
 
Naona bado hajaeleweka, sasa atatofautisha vipi wa miaka 18 mwenye kipato na asiye na kipato provided wote wana namba ya NIDA?

Haya majibu nusu nusu yanaonesha vile alivyokurupuka kuja na huu mpango bila ya kuufanyia tathmini ya uhakika.

Nachoona hapo kuna dalili hiyo kodi watatozwa wote wenye miaka 18 wenye namba ya NIDA, bila kujali mtu ana kipato au hana.

Mwigulu hapa akubali tu, hii kodi yake ni unyonyaji uliopitiliza, kama tayari wanakata kodi kwenye bidhaa zinazonunuliwa na wananchi bila kujali umri wao, tozo kwenye miamala ya simu bila kujali umri, hii kodi ya kichwa ni kurudishana utumwani, aifute.
 
Kundi la watu wenye umri la vijana wenye miaka 18 hadi 21 limegawanyika katika makundi madogo yafuatayo;
a) Wanafunzi wa sekondari na vyuo
b) Wahitimu wa vyuo na shule wasiokuwa na vipato ama ajira
c) Waajiriwa katika sekta iliyo rasmi na isiyokuwa rasmi
d) Waliojiajiri wenyewe
e) Wenye ndoa ama kuishi na wenza

Kutokana na mapendekezo ya waziri, wote hao watapaswa kuwa na namba ya mlipa kodi (TIN) ambayo itaunganishwa katika kumbukumbu za kitambulisho cha taifa (NIDA). Isipokuwa makundi "a" na "b" hapo juu hayataguswa na ulipaji wa kodi mbalimbali mathalani VAT, Income tax, customs & excise duties kwa kuwa hawana shughuli halali zenye kutambulika na kuwapatia vipato.
 
Naona Mwigulu anazidi kujichanganya tu.
Kwa hiyo mtu mwenye kipato na akiwa na umri wa chini ya miaka 18 hatapaswa kulipa kodi?

Kiuhalisia karibu kitu mtu mzima ana kipato fulani, kiwe rasmi au sio rasmi, kiwe cha yeye kutafuta mwenyewe au kutafutiwa. Kula, kulala na kuvaa ni matumizi ya kipato.

Kiuhalisia kila mtu mwenye kipato indirect or direct ni mlipa kodi toka enzi na enzi. Kwa kuwa wakati anapata kipato chake huenda alikatwa kodi au wakati anatumia kipato chake (kulipia huduma au kufanya manunuzi) automatically atakatwa kodi.
 
Uongo Mtu Atajuaje Mwenye Kipato​

Mbona Walishindwa Kuunganisha Leseni Ya Udereva Na Kitambulisho Cha Kupigia Kura Wakakomaa Kutoa Nida. Hiyo Ni Janja Pia Hana Ubunifu Wowote
Mh walishindwa? Maana majuzi hapa nimempeleka mtu kutengeneza leseni bila NIDA inakuwa ngumu.
 
Naona bado hajaeleweka, sasa atatofautisha vipi wa miaka 18 mwenye kipato na asiye na kipato provided wote wana namba ya NIDA?

Haya majibu nusu nusu yanaonesha vile alivyokurupuka kuja na huu mpango bila ya kuufanyia tathmini ya uhakika.

Nachoona hapo kuna dalili hiyo kodi watatozwa wote wenye miaka 18 wenye namba ya NIDA, bila kujali mtu ana kipato au hana.

Mwigulu hapa akubali tu, hii kodi yake ni unyonyaji uliopitiliza, kama tayari wanakata kodi kwenye bidhaa zinazonunuliwa na wananchi bila kujali umri wao, tozo kwenye miamala ya simu bila kujali umri, hii kodi ya kichwa ni kurudishana utumwani, aifute.
Nakazia tu!
 
View attachment 2264277
Picha> Waziri wa Fedha Mwigullu Nchemba akiwa ameshika kipaza sauti

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kodi haitotazwa kwa kila mtu mwenye umri wa miaka 18, bali atatozwa mtu mwenye kipato ambacho kinaangukia wigo unaotakiwa kutozwa kodi.

Waziri Mwigulu amezungumza hayo ili kuwaondoa hofu wananchi kufuatia kauli ya ulipaji kodi kwa wenye umri wa mika 18 iliyotolewa katika bajeti ya 2022/23 Juni 14 bungeni Dodoma.

“Kuhusu kodi haitozwi kila mtu, anatozwa mwenye kipato, kwa hiyo mtu mwenye kipato ndiye anayetozwa kodi sio mtu mwenye kitambulisho cha taifa. Kitambulisho cha taifa ni utambuzi lakini kodi anatozwa yule mwenye kipato, watu wasipate hofu sisi, tunawarahisishia,” amesisitiza Mwigulu Nchemba.

Aidha, amesema kuhusu namba ya utambulisho ya mlipa kodi kwa mtu ambaye anataka kuanzaisha biashara asisumbuliwe kuandikisha taarifa zake upya bali taarifa ziunganishwe kwenye kitambulisho chake cha taifa.

Pia soma:
1. Serikali: Kila Mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi
2. Zitto Kabwe: Waziri afafanue kodi aliyoitangaza, kodi hailipwi na mtu
HUYU KIJANA MBAYA KULIKO SHETANI
 
Hi
Waziri sasa kaeleweka, yaani ana maana kuwa kodi itotazwa kwa kila mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 ambaye pia ni mwenye kipato.
Zo nigeresha tu likija swala la utekelezaji utasikia mabumu chuo kikuu yanakatwa kodi we subiri tu
 
Hilo ndio tatizo la wasomi njaa hawa
Yaani mpaka walete kelele zisizokuwa na faida
Kwani alishindwa nini kufafanua kabla ya kukurupuka?
 
Back
Top Bottom