Mwigulu Ndani Ya SCOAN Leo 28.12.14

Mwigulu Ndani Ya SCOAN Leo 28.12.14

Ungetumia kichwa cha juu ungeelewa mantiki ya swali, ila kwa kuwa umetumia kichwa cha chini ndio maana umekurupuka hivi.

sina muda wa kushindana na mfu kama wewe
 
Ni akili ya kushikiwa tu hii, kama mungu anapatikana Nigeria basi wakristo wote twendeni tukaabudu Nigeria.
Idiot Migulu.
Assume angekuwa hana uwezo wa kwenda Nigeria angeenda kuabudu wapi?

Hii ni kutapatapa kwa kutojiamini na aliyoyafanya so nafsi inamshitaki.

Hata kesho akiambiwa Syria kuna mhubiri makini utasikia kaenda.
Hajiamini huyu.

Katika dunia ya utandawazi unazungumzia umbali?kama huna pesa kwako Nigeria ni mbali. Lakini kwa mtu asiye na shida na pesa sio Nigeria tu bali ata UChina ni karibu.

Hivi hujawahi sikia watu wanatoka Tanzania kwenda kuangalia mpira Uhispania?kwani hakuna Yanga na Simba Tanzania?wapo lakini anataka kwenda kuwaona Madrid.

Kushupalia hilo ni ulimbukeni tu, shida zako sio za wenzako.Kula na tembea kulingana na uwezo wako lakini usishupalie mfuko wa mwenzako.
 
Heri ya huyu aliyekwenda kanisani kuliko wale waliokwenda kugonga kikombe cha babu pande za Samunge Loliondo e.g Steven Wassira, Willium Lukuvi, John Magufuli, Jakaya Kikwete etl.

Babu alikuwa anatibu magonjwa sugu yaliyonayo waheshimiwa hao hapo juu. Joshua anatoa tiba ya kiroho kwa wale wliowahi kuwa wadhambi wakuu kama Mugulu.
 
Hapana hawapo tofauti, Mungu anawatumia watu kwa namna tofauti na kwa viwango tofauti. Labda nikuulize swali hivi Kikwete anapoteua watu wa kumsaidia kazi huwa wote wanakuwa mawaziri wakuu?
Acha kumfananisha Mungu anavotenda kazi na uteuzi wa kikwete!!plz take a break!!
 
Sioni tatizo kwa mwigulu kwenda SCOAN...kwani maisha ya mwigulu ni siasa tu hana mambo mengine ...hatakiwi kumtumikia mungu wake anaemuamini??????
Mungu anatumikiwa Nigeria tu?
 
amefunuliwa au alienda kutubu dhambi zake!!ni ushabiki wa kijuha kuamin kua mungu anafunua watu kuptia kwa mashabik wa mhuska!Bali ni usafi wa roho matendo mema ya mhusika bas!!
 
Si ajabu Mwigulu Nchemba kwenda kwa TB Joshua;kwani wenzake waenda kwa mufti na kwa wachawi ili wapate VYEO na utajiri !
 
Katika dunia ya utandawazi unazungumzia umbali?kama huna pesa kwako Nigeria ni mbali. Lakini kwa mtu asiye na shida na pesa sio Nigeria tu bali ata UChina ni karibu.

Hivi hujawahi sikia watu wanatoka Tanzania kwenda kuangalia mpira Uhispania?kwani hakuna Yanga na Simba Tanzania?wapo lakini anataka kwenda kuwaona Madrid.

Kushupalia hilo ni ulimbukeni tu, shida zako sio za wenzake.Kula na tembea kulingana na uwezo wako lakini usishupalie mfuko wa mwenzako.
This is precisely the point ya watu wengi kwa sababu anayo hiyo hela, sasa anawaambia nini waumini wengine ndani ya Tanzania.

Ni sawa kwenda kwenya hija za holy places kama Israel au huko vatican atleast annually, lakini habari za kwenda makanisa ya nchi nyengine hizo sasa ndio ngebe zenyewe za pesa sidhani ni sahihi kwa mwanasiasa ambae amekuwa akijivunia yeye ni mtoto wa mkulima.
 
Hao wanasiasa wanakimbilia kutubu Naija badala ya kutubu kwanza kwa wananchi!!Hata neno linasema,"Kabla hujatoa sadaka yako,patana kwanza na mwenzio..",sasa wanadhan kutubu kwa Mungu ukamwacha ulomkosea ni suluhisho!!na urahisi haupatikani ,kwa Joshua,bali kwa kura!!
 
Kwa kutomfuata mungu mwenye uwezo mkubwa pale Nigeria ndiyo nimekuwa mjinga au Mimi kukosa nauli na sadaka ndiyo nimekuwa mjinga?

Asante sana kwa ujinga wangu heri wewe uliye na mungu mwenye uwezo akakuondelea ujinga ukakupa uwezo wa kwenda huko.

Mimi nasali hapahapa coz mungu wangu kanipa ujinga wa kusali hapa nilipo.

Then tatizo lako nini?wewe unaenda kusali Ukonga au Kibamba au Yombo kwa sababu ndio karibu kwako, ndipo reference ya "karibu" kwako inapoishia maana ENEO KARIBU linategemeana na mtu na mtu, eneo karibu kwako sio eneo karibu kwangu.Tambua hilo litakusaidia.

Kwa wengine Marekani ni karibu sana sembuse Nigeria?ni kama wewe unavyopanga leo uwe Gongo la Mboto na kesho uende kwa Mtogole na ndivyo wengine wanavyopa tu leo wawe Zanzibar kesho wawe na Nigeria na keshokutwa wawe Uchina.

Sasa kuangalia hayo kwa kioo cha hali na shida yako ndiko kunakoleta hayo maneno...ooh ni mbali sana...mbali kwako sio kwa wengine.

Ishi kulingana na uwezo wako na usiifunge dunia kwenye tabu na shida zako, dunia haipo hivyo, vikwazo vyako sio vya wengine.
 
Back
Top Bottom