Mwigulu Ndani Ya SCOAN Leo 28.12.14

Mwigulu Ndani Ya SCOAN Leo 28.12.14

Je! Tanzania hayupo Mungu wa Kweli na Haki mpaka watu wakatalii kwenye masinagogi ya Israeli na Nigeria ?!
{UFUNUO 3:9 }
 
Biblia inasema:mtawatambua kwa matunda yao!(Hupati embe kwenye mbilimbi) km ameenda kuongeza mapepo mwisho wa cku yatalipuka tu!!
km anataka kuwa nabii tutajua!!
 
This is precisely the point ya watu wengi kwa sababu anayo hiyo hela, sasa anawaambia nini waumini wengine ndani ya Tanzania.

Ni sawa kwenda kwenya hija za holy places kama Israel au huko vatican atleast annually, lakini habari za kwenda makanisa ya nchi nyengine hizo sasa ndio ngebe zenyewe za pesa sidhani ni sahihi kwa mwanasiasa ambae amekuwa akijivunia yeye ni mtoto wa mkulima.

Tabu zako na shida zako usidhani ni ya mwenzako, wewe saizi angaika na ada ya watoto maana ukipanda ndege kwenye South kutembea utafilisika.

Sasa tena unasema hapo kuwa safari kwenda Israel au Vatican mara moja kwa mwaka ni sawa?sawa tena?kwani Mungu yupo Israel na Vatican?unajicontradict tena.Na hiyo safari ya mara moja kinachokufanya useme mara moja kwa mwaka ni bajeti yako, mbona unaenda Kariakoo zaidi ya mara kumi kwa mwezi?ni kwa sababu kwa uwezo wako kariakoo ni karibu.Fahamu kwa wengine pia Nigeria ni karibu, Ukaribu na Umbali unalimitiwa na uwezo wako wa kipi unakimudu na bajeti yako.

Kwa dunia ya sasa Nigeria ni karibu sana, kwa wengine hapa ata Zanzibar ni mbali, so sitashangaa Nigeria kuwa ni mbali zaidi.

Huu ni uamuzi wa mtu binafsi, na bila shaka katumia pesa yake ambayo kwa nafasi yake ya Ubunge na Unaibu Waziri anaimudu kabisa.

Mwigulu alikuwa mtoto wa maskini, leo ni Mbunge na Naibu Waziri, kwa akili za kawaida tu yeye sio maskini leo.

Na kuwasaidia maskini sio kwa kuishi kimaskini bali kwa kuwa na uwezo na nia ya dhati ya kujenga nyenzo za kupunguza umaskini sehemu ulipo.
 
Kama ni imani aipaswi kukumbuka. Ukiwa nayo ni popote unamwomba mola na yupo.tunasumbukia ulimwengu
I la ni bure wanajichosha
 
Mungu anatumikiwa Nigeria tu?

Nani kasema Mungu yupo Nigeria tu?unasema mwenyewe na kujijibu mwenyewe.Tatizo kubwa hili.

Last time i checked Mwigulu uwa anaenda kanisani pia ata akiwa Iramba na naamini ata akiwa Marekani uwa unasali pia, sasa hiyo kauli umeitoa wapi?
 
Wanajamvi Salaam,

Katika Muda Na Saa Hii Mh. Mwigulu Yuko Katika Kanisa La Nabii TB Joshua Lagos Nigeria Akiabudu.

Katika Siku za Karibuni Mwenendo Na Tabia Za Mbunge Huyu Wa Iramba Na Naibu Wa Fedha Zimebadilika. Amekuwa Mstaarabu Katika Kauli Zake. Je, Ameamua Kuokoka Na Kubadilika Kweli Au Kuna jingine?

Napenda Sana Aendelee Kuwa Katika Njia Hii.

urais unatafutwa. sasa Joshua atawachanganya na Lowasa.

halafu hii kasumba ya kwenda nigeria ni ujinga tu maana Mungu ni omnipotent ya nn kuamini ya Nigeria kama sio uchawi?
 
Then tatizo lako nini?wewe unaenda kusali Ukonga au Kibamba au Yombo kwa sababu ndio karibu kwako, ndipo reference ya "karibu" kwako inapoishia maana ENEO KARIBU linategemeana na mtu na mtu, eneo karibu kwako sio eneo karibu kwangu.Tambua hilo litakusaidia.

Kwa wengine Marekani ni karibu sana sembuse Nigeria?ni kama wewe unavyopanga leo uwe Gongo la Mboto na kesho uende kwa Mtogole na ndivyo wengine wanavyopa tu leo wawe Zanzibar kesho wawe na Nigeria na keshokutwa wawe Uchina.

Sasa kuangalia hayo kwa kioo cha hali na shida yako ndiko kunakoleta hayo maneno...ooh ni mbali sana...mbali kwako sio kwa wengine.

Ishi kulingana na uwezo wako na usiifunge dunia kwenye tabu na shida zako, dunia haipo hivyo, vikwazo vyako sio vya wengine.

Sasa wewe uliniita mjinga coz sina nauli au?
Hizi showbiz za Mwigulu mngesema kaenda kutembea Nigeria siyo kusali.

Watu wanatumiaga dini kama njia yao ya kupitia/kuingia/kufanya wayatakayo.

Kwahiyo msitudanganye eti kaenda kusali/kutubu au aliuwa MTU?
 
Je! Tanzania hayupo Mungu wa Kweli na Haki mpaka watu wakatalii kwenye masinagogi ya Israeli na Nigeria ?!
{UFUNUO 3:9 }

Umeishasema kutalii, then tatizo nini tena?kutalii ni kwenda sehemu na kuangalia kulivyo.

Sasa unataka watu wakatalii sehemu walipozaliwa?utaona nini usichokijua?
 
Sasa wewe uliniita mjinga coz sina nauli au?
Hizi showbiz za Mwigulu mngesema kaenda kutembea Nigeria siyo kusali.

Watu wanatumiaga dini kama njia yao ya kupitia/kuingia/kufanya wayatakayo.

Kwahiyo msitudanganye eti kaenda kusali/kutubu au aliuwa MTU?

Ni wewe ndio ulisema kuhusu ujinga, nilikujibu kwa muktadha huo, kuwa kama wao wajinga kwenda kanisani ambako ni karibu kwao basi na wewe unayetoka kwako kwenda kanisani ambako ni karibu kwako nawe ni mjinga kama wao.

Naona umeanza kuelewa hilo, kuwa kama wewe unavyosali Ukonga na siku nyingine Gongo la Mboto ndivyo wengine wanavyoweza sali leo Lagos na siku nyingine Pretoria.

Hayo ya kusali kwake, je wewe ni mhudumu kwenye ikulu ya Mungu?kama wewe uwa unaenda kanisani kwa ajili ya kujionyesha na kufanya hizo unazoita showbiz basi usidhani kila mtu uwa anaenda kufanya hivyo, wengine wakienda kanisani au msikitini humaanisha na husali hasa.

Sasa kama wana dhambi au kama sala zinafika au hazifiki kwa Mungu na kama zinafika Mungu anazionaje hilo sio lako wala la mimi kulisemea, Mungu wao atawajudge mwenyewe, labda kama wewe mwenzetu ni katibu muktasi wa ikulu ya Mungu so umeishaona ripoti ya Mungu juu ya maombi yake.

Jifunze kufikiri ki-universal, na sio kufikiri kwa hali, shida, mawazo na matendo yako tu kwani wengine HAWAPO KAMA WEWE.
 
Fahamu kwa wengine pia Nigeria ni karibu, Ukaribu na Umbali unalimitiwa na uwezo wako wa kipi unakimudu na bajeti yako.

Kwa dunia ya sasa Nigeria ni karibu sana, kwa wengine hapa ata Zanzibar ni mbali, so sitashangaa Nigeria kuwa ni mbali zaidi.

Huu ni uamuzi wa mtu binafsi, na bila shaka katumia pesa yake ambayo kwa nafasi yake ya Ubunge na Unaibu Waziri anaimudu kabisa.

Mwigulu alikuwa mtoto wa maskini, leo ni Mbunge na Naibu Waziri, kwa akili za kawaida tu yeye sio maskini leo.

Na kuwasaidia maskini sio kwa kuishi kimaskini bali kwa kuwa ni uwezo wa kujenga nyenzo za kupunguza umaskini sehemu ulipo.
Tatizo lenu nyie wapambe njaa ndio zinazo watoa akili sasa nani asiyejua kwa nafasi ya Mwigulu posho anazochokuwa anauwezo wa kwenda kanisa lolote duniani kila jumapili akiamua?

Swala hapa yeye ni kiongozi kuwa kioo cha jamii angeenda kimya kama kweli anamfuata mungu kwa malengo yake nani angepiga kelele.

Lakini unapoanza kufanya publicity za wewe kwenda makanisa ya Nigeria linakuwa zaidi ya swala la imani bali kujionyesha ya kuwa wewe una option mbele ya jamii ambao wengi hawana huo uwezo isitoshe kuna watu wanaweza amini Nigeria kuna kanisa bora zaidi hadi waziri analifuata mara kwa mara ndio maana yake hiyo.

Kwani unadhani hao akina Sokoine au Nyerere wangeshindwa kuwajengea majumba watoto zao wakaya promote au kuchagua kuendeshwa na magari ya kifahari wakati wa uongozi wao, au unadhani wakati watanzania wanapanga foleni ya sukari na wao pia walikuwa na shida za sukari.

Issue hapa ni twasira anayoileta kwa jamii kutokana na uwezo wake na direct message anayowatumia waumini wengine wa dini. Unatakiwa uongoze kwa mfano anasa zako ziwe private, kama unaona kuna umuhimu kwa kwenda kwa TB Joshua nenda kimya basi sio kutuonyesha sie tusio na uwezo uongozi maana yake utajiri.
 
hamuamini mtu anapobadilika!! suala ni kuona uelekeo yake!!

kwa TB J kuna siku hatarudi kabisa kama LOWASA lazima kuna sehemu utatakiwa kukiri yote uliyoyafanya kumbuka LOWASA aliambiwa aseme yote aliyokuwa anafanya akashindwa kwa kuwa alijua DUNIA NZIMA ITASIKA akakataa na ndio mpaka leo hajarudi
 
Tatizo lenu nyie wapambe njaa ndio zinazo watoa akili sasa nani asiyejua kwa nafasi ya Mwigulu posho anazochokuwa anauwezo wa kwenda kanisa lolote duniani kila jumapili akiamua?

Swala hapa yeye ni kiongozi kuwa kioo cha jamii angeenda kimya kama kweli anamfuata mungu kwa malengo yake nani angepiga kelele.

Lakini unapoanza kufanya publicity za wewe kwenda makanisa ya Nigeria linakuwa zaidi ya swala la imani bali kujionyesha ya kuwa wewe una option mbele ya jamii ambao wengi hawana huo uwezo isitoshe kuna watu wanaweza amini Nigeria kuna kanisa bora zaidi hadi waziri analifuata mara kwa mara ndio maana yake hiyo.

Kwani unadhani hao akina Sokoine au Nyerere wangeshindwa kuwajengea majumba watoto zao wakaya promote au kuchagua kuendeshwa na magari ya kifahari wakati wa uonogzi.

Issue hapa ni twasira anayoileta kwa jamii kutokana na uwezo wake na direct message anayowatumia waumini wengine wa dini. Unatakiwa uongoze kwa mfano anasa zako ziwe private, kama unaona kuna umuhimu kwa kwenda kwa TB Joshua nenda kimya basi sio kutuonyesha sie tusio na uwezo uongozi maana yake utajiri.

Ndugu yangu, ndio tatizo lilelile la kuona hali yako ni hali ya wengine, unadhani kila mtu anaishi kwa upambe kwa ajili ya kufurahisha watu.Wengine tunajadili tu kutokana na tunavyoona hali ilivyo na uhalisia ulivyo.Na huyo Mwigulu hana uwezo wa kunilipa.

Hayo ya kwenda Nigeria ni anasa?yaleyale limitation zako ndio zinafanya uone anasa kwa sababu bajeti yako labda hilo la kujitangaza?sijaona press conference yoyote imeitishwa Mwigulu akiwataarifu watu kuwa anaenda Nigeria; huyu aliyeleta mada it just happened kuwa ameona kwenye TV na kuleta hapa, asingeona na wengine wasingeangalia huko TV basi tusingejua kuwa yupo huko maana naamini hiyo ibada haionyeshwi TBC wala Tv yoyote za Tanzania.

Bottom line ni kuwa hakuna cha ajabu na wala sio anasa kwa dunia hii ya leo mtu kutembelea Nigeria, umbali na ukaribu ni related term kutokana na uwezo wa mtu, kwa mshahara wa Ubunge anaweza kabisa na sio anasa.

Hayo ya Nyerere na Sokoine kuishi kimaskini, sioni inahusiana vip na hii topic maana kwenda Nigeria sio utajiri. Kama Mwigulu katumia mshahara wake na hajatumia ata senti ya serikali kwenye safari yake, kajilipia mwenyewe hotel na chakula huko Nigeria, yes hajavunja kanuni yoyote ya uadilifu tunaoutaka.

Kumbuka dunia inabadilika, walivyoishi mwaka 1980 sivyo tunavyoishi leo.Na KUWA MASKINI AU KUISHI KIMASKINI WAKATI UWEZO UNAO SIO SIFA.

WAtanzania hawahitaji kiongozi maskini bali wanahitaji kiongozi mwenye uwezo, nia ya dhati na uadilifu wa kusimamia rasilimali za nchi na kujenga mazingira ya kujenga uchumi unaonufaisha nchi na wananchi walio wengi.

Na kufanya hivyo, kiongozi huyo ni lazima asiwe na akili za kimaskini maana kipofu hawezi muongoza kipofu mwenzake.Muhimu hapa ni UWEZO WAKE, UADILIFU WAKE NA UCHU WA KUBADILISHA HALI KUWA BORA ZAIDI KULIKO ILIVYO SASA.
 
kuna watu wanaogopa kueleza ukweli!! binadamu yeyote ni dynamic and not static!!! akija atatueleza pamoja na kwamba viongozi wengi wana kiburi!! hawapendi kukosolewa watubu mbele ya watanzania !!
 
Anapata majinamizi kwa yale mabomu ya Arusha. He is dead spititually anatafuta sympathy. Shetani hawezi kuwa malaika.
 
Back
Top Bottom