Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Nionavyo mimi kufa kwa chama nikukosa wanachama na chama kukataliwa na wananchi, jee ichara hizi nani mwenye nazo kati ya chadema na ccm?.

Realty nikuwa ccm ndio iko coma na sio leo hupata unafuu kwa kuokolewa na Zec na Vyombo vya Dola bila ya kutumia kilinge hicho tungrkuwa tayari tumesha ifanyia feneral.
 
Tunashauri serikali na chama tawala, shughulikieni matatizo ya wananchi badala ya kutumia muda mwingi na rasilimali nyingi kudhoofisha/kuua upinzani. Mnaacha rasilimali zetu na pesa zetu zinatoroshwa huku mkiwapa kinga MAFISADI wanaoifilisi nchi na kutuongezea ugumu wa maisha. Tunaomba mtubadilishie wimbo sasa, tumechoka kuwasikia kutwa kucha mnapambana na CHADEMA badala ya kupambana na UMASKINI, MARADHI na KUFUTA UJINGA.
 
namuunga mkono mh.mwigulu maana kwa ukabila,na ukaskazini wa chadema hawawezi fika 2015 wakiwa salama.ubaguzi,chuki na choyo ndo unaokiua chama na si mwigulu wala ccm.watanzania wanajua mission na vision ya ya chadema si kuwasaidia watanzania zaidi ya kulinda maslahi ya wakaskazini na familia zao.
 
Malumbano ya vyama hayatusaidii watanzania tumepigika kipindi kirefu tunahitaji mabadiliko
 
Malumbano ya vyama hayatusaidii watanzania tumepigika kipindi kirefu tunahitaji mabadiliko
 
nchemba.jpg

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba

CHAMA Cha Mapinduzi kimekitabiria kifo Chadema baada ya uchaguzi wa 2015 kikieleza kuwa CCM ikishinda, chama hicho kitakuwa hakina nguvu tena kwa kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa atakuwa amechoka.


Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba aliliambia gazeti hili jana kuwa chama hicho kinapoteza umaarufu kadri siku zinavyokwenda hasa kutokana na siasa zake za uchochezi na mwaka 2015 ndio itakuwa mwisho wa chama hicho.


Alisema kitakufa na kitasahaulika kabisa, akisema sasa hivi vijana wameshaanza kuwakimbia, na kwamba anaamini pia baada ya 2015 hakuna diwani ambaye atagombea kupitia chama hicho.


Alisema pia ni mwaka ambao Katibu wa Chadema Willibrod Slaa amestaafu kwa kuwa alishatangaza asiposhinda atastaafu na Chadema haiwezi kushinda hivyo mwisho wa Dk Slaa ndio utakuwa umefika kwa kuwa nyota yake haitang’aa tena.


“Nguvu ya Dk Slaa aliyokuwa nayo miaka miwili iliyopita sio aliyonayo sasa na mpaka mwaka 2015 atakuwa ameisha kabisa.” alisisitiza.


Pia Mwigulu aliyataka makundi yaliyojichomoza ndani ya CCM ikiwa ni harakati za kuwania urais mwaka 2015 kuheshimu ilani ya chama hicho kwa kuitekeleza na kuisimamia kwa kutoleta vurugu ndani ya chama wala kujenga chuki kwa wale ambao hawawaungi mkono.


|”CCM ina utaratibu wake wa kupata mgombea na hatumzuii mtu kugombea, sisi kama kamati ya utendaji tunatekeleza maagizo aliyotoa mwenyekiti tutayasimamia kwa nguvu zote anayetaka kugombea ahakikishe havurugi chama na asitengeneze chuki kwa ambao hawamuungi mkono.”


Wakati huohuo Naibu Katibu huyo wa CCM na Mbunge wa Iramba Mashariki aliwataka wakazi wa Mtwara kuachana na propaganda zinazoenezwa na wapinzani kuhusu rasilimali ya gesi na badala yake wafanye kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.


“Rasilimali iliyopo ni ya taifa na watafaidika, hakuna rasilimali ya wilaya fulani, bomba la gesi ni lazima lijengwe tutawaelimisha wakazi wa Mtwara, kwani hata Ziwa Victoria bomba lilijengwa kwenda Shinyanga badala ya Kwimba, kwa nini basi halikujengwa kwenda Kwimba wakati pale ni karibu zaidi.


“Utajiri unategemea na jitihada, wasitegemee kwa vile tuna rasilimali ya gesi basi wakae wategemee watapata utajiri bila ya kufanya kazi haiwezekani, wasisubiri kupewa vya bure, ni kama mikoa yenye madini halafu wakazi wa pale wategemee Serikali itawapa vocha za kuweka kwenye simu kwa vile madini yao kwao, haiwezekani ni lazima wafanye kazi.

Source: Mwananchi

My take:

- Attention ya CCM ni Dr. Slaa.

Huko mbali sana chadema chali 2014
 
Mbona mnanichanganya, huyu ni Mwigulu Nchemba au Lameck Madelu Mkumbo?. Mbona Mwigulu Nchemba ni msukuma yupo igunga anachunga mifugo yake?,
 
Atakufa yeye na domo lake refu. Hana adabu kwa wazee huyo.
 
Mwigulu, kulikoni! Mbona unapingana na ule utabiri wa awali wa mnajimu mwenza aitwaye S.M. Wassira?

Hii inathihirisha wazi kuwa ni ukweli usiopingika kuwa PM-7/Msalia na akina Shibuda ulikuwa ni mpango-mkakati wa kutegemewa wa CCM kuivuruga CHADEMA. Maana kwanini sio tena ndani ya mwaka mmoja kama alivyodai kwa majigambo Waasira Mei 2012?

Tanzania sio mali yenu, na ratiba yake haiko mikononi mwenu tena!
 
aka mkosa chama tatizo la Watz tunashabikia tusilolijua kwani hamjua vita iliyopo cdm? kama hamjui hicho chama cha wachaga mtadanganyika mpaka lini fuatilieni mtaona au ni chama cha mzee Mtei

Na wewe tukuite Great Thinker? Kama CDM ni chama cha wachagga na CCM ni cha watu wa kabila gani? Naona wewe ni mchumia tumbo uliye kwenye 'paylist' ya kina Nnauye na Mchemba usiye na uchungu kabisa na nchi yako! Toa data za kusapoti allegations zako la sivyo watu watatilia shaka uwezo wako wa kufikiri.
Ufisadi, rushwa na tamaa ya kutawala milele imewapumbaza CCM na kuwafanya waweweseke mithili ya mtu aliyepata ile dawa ya usingizi inayoitwa Ketalar ambayo aliyepewa huweweseka na kusema maneno kibao yasiyokuwa na maana yoyote! Statements kama hizi zinakivunjia hadhi chama kikongwe na mashuhuri hiki chenye historia ya kuzalisha watu mashuhuri walioitikisa Afrika na dunia!
Hivi kweli CCM imeshindwa kabisa kujifunza chochote toka kwa waasisi wake ambao busara zao zinakumbukwa hadi leo au ni upofu uliosababishwa na kufakamia ufisadi? Mwasisi wa chama chao Hayati Nyerere (RIP) alifanya juhudi za kuwafunda dhidi ya ubepari ndiyo kwanza sasa wameukumbatia na kamwe hawataki kuuachia hata kama utawagharimu roho zao na za waatanzania wengi! Aliwaonya juu ya udini na ukabila na sasa ndiyo waumini wazuri kabisa wa siasa hizo! Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa.
Watanzania tuamke sasa mchawi wa chuki zinazojitokeza sasa katika jumuiya ya watanzania ya kuhujumiana kiimani na pengine kubaguana kwa misingi ya ukabila, udini na matabaka ya walio nacho na wasio nacho ni dude hili linaloitwa CCM na kamwe hatutapumua mpaka ling'olewe litupwe linakostahili - motoni.

 
kiwewe cha 2015,anajua jimboni kwake ni pachungu sasa hivi!!!Tundu Lissu amesha mwanga sumu!!!
 
Wazanzibar wamesema wamechoshwa na tabia ya CCM bara kuwapereka Dodoma na kuwachagulia Rais sasa wanataka wao kama CCM zanzibar watakuwa wanachagua wao Rais wamtakaye siyo kuburuzwa na CCM bara! Mimi naona sasa CCM imeishikwa pabaya sasa ndo mwanzo wakufa hiki chama! Na hawana ubavu wa kuwazuia ngoja tuone hii ngoma ninani ataicheza!
 

Wakati huohuo Naibu Katibu huyo wa CCM na Mbunge wa Iramba Mashariki aliwataka wakazi wa Mtwara kuachana na propaganda zinazoenezwa na wapinzani kuhusu rasilimali ya gesi na badala yake wafanye kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

“Rasilimali iliyopo ni ya taifa na watafaidika, hakuna rasilimali ya wilaya fulani, bomba la gesi ni lazima lijengwe tutawaelimisha wakazi wa Mtwara, kwani hata Ziwa Victoria bomba lilijengwa kwenda Shinyanga badala ya Kwimba, kwa nini basi halikujengwa kwenda Kwimba wakati pale ni karibu zaidi.
Utajiri unategemea na jitihada, wasitegemee kwa vile tuna rasilimali ya gesi basi wakae wategemee watapata utajiri bila ya kufanya kazi haiwezekani, wasisubiri kupewa vya bure, ni kama mikoa yenye madini halafu wakazi wa pale wategemee Serikali itawapa vocha za kuweka kwenye simu kwa vile madini yao kwao, haiwezekani ni lazima wafanye kazi."

Nasikia kwamba Mheshimiwa Mwigulu Mchemba ni mchumi mwenye shahada ya uzamili. Sitarajii mtu wa aina hiyo atoe kauli hii: "hakuna rasilimali ya wilaya fulani." Namshauri aliombe radhi taifa. Vinginevyo tutaiomba seneti ya chuo kikuu kumvua kofia ya uzamili. Rasilimali za nchi hii ni maslahi ya wote. Hivyo, kila rasilimali ni ya wilaya fulani, japo sio ya wilaya fulani pekee. Kwa mfano maji ya Victoria ni rasilimali ya wilaya fulani, japo sio rasilimali za wilaya fulani pekee. Ni vivyo hivyo kwa rasilimali zingine. Angeuelewa umantiki huu, nadhani hotuba yake ingekuwa yenye kujenga ukweli badala ya ghiliba. Nasubiri kusikia toka kwake.


 
Ndugu zanguni,

Kama mjuavyo ndani ya chadema kuna mgawanyiko wa kutosha na tayari tuna team tatu ambazo zimejigawa kikanda., Hii ni moja ya dalili kuwa Chadema itasambaratika mapema kuliko wengi tulivyofikiri

Sababu kuu ya kusema haya ni hili suala la mahesabu na uchaguzi ndani ya Chadema

Tayari tunajua kuwa Chadema wameingia kambini kuchakachua mahesabu ili wayawakilishe kwenye kamati ya bunge ya mahesabu huku yule aliyewaitisha mahesabu haya akiwa tayari ana data zote za haya mahesabu hivyo hata wakichakachua vipi wataishia kuumbuka tu.

Suala la uchaguzi litaibuka upya soon kwani vijana tayari wameishaanza kuwashitukia viongozi waliopo kuwa ni matapeli.

Nawashauri makamanda wasikubali kufanywa misukule na kudanganywa kitoto bali wasimame na kudai uchaguzi ili wachague viongozi wanaowataka.

TUSUBIRI MHESHIMIWA JEMBE ARUDI KUTOKA SAFARI ......

JITAMBUE

MIMI KAMA kijana mzalendo nawashauri CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CDM) kuwa makini kwani neno demokrasi linakuwa gumu kwa baadhi ya viongozi

1. kuna baadhi ya viongozi wa juu wanaamini wao ndio kila kitu ndani ya chama na wengine inawapasa wawasikilize bila hoja bali kwa hoja ya nguvu
2. mwenyekiti na katibu mkuu wameonekana wanatumia udikteta katika baadhi ya masuala ndani ya chama wao ndio walipaswa kutekeleza wigo mpana wa demokrasia
3.uhuru wa maoni ndani ya chama unatia shaka kubwa kwani mfano mzuri ni suala la mwigamba kutoa maoni yake na baadhi ya watu kumuona msaliti
4. chadema wanapaswa kujua demokrasia sio kupinga kila kitu kama kuna kiongozi au mbunge wa chama kingine amefanya jambo zuri anapaswa kupewa haki yake na kama kakosea anaakosolewa angalia MH shibuda kwakua yupo huru baadhi ya wananchama wanamwita yy ni ccm hii inaonyesha kuwa kuna poor tolerance ndn ya chadema
5. kuhoji suala la uchaguzi ndani ya chama inaonekana ni usaliti je udikteta hauanzi kama hivi angalia dikteta hitler alivokuwa anakubalika tazama baada ya kupata madaraka ilikuaje? huwezi kuwa na uwajibikjai wa kisiasa huku ukiahirisha uchaguzi kila wakati bila sababu za msingi
6.kuhoji kwann katibu mkuu alipwe kodi za wananchi mshahara kama mbunge wakati yy si mbunge je waliwauliza wanachama au referendum kupta uhalali kama huu si ufisadi wa maamuzi wa watu wachache
7.tabia mpya ya kusimamisha viongozi bila kufata katiba ya chama ni hatari kwa mustakabali wa demokrasia
8. kubadili vifungu vya katiba vya ukomo wa uongozi kinyemela huo ni uhaini ndani ya demokrasia

BILA SHAKA CHAMA KIKIENDELEA KUTAFUTA MCHAWI NI NANI HAPO NDIPO ANGUKO KUBWA LA CHADEMA LAJA KWANI MTAANZA KUFUKUZANA. TAMBUA CHADEMA HAKIUNDWI NA WATU WA KANDA MOJA TU BALI NCHI NZIMA

kwanza kabisa napenda kutoa rai mimi ni mtanzania ambaye naitaji mabadiliko kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii. mabadiliko ambayo ccm imeshindwa kuyafanya hivyo basi niliamini kuwa vyama vya upinzani vitakuwa chachu ya mabadiliko hayo lakini ni tofauti. kwan mwaka 1995 niliamini kuwa Nccr mageuzi chini ya Mhe Mlema nilijua ndio kitaleta mabadiliko lakini hali aikuwa hivyo na hatimae waliingia kwenye malumbana baina ya viongozi wenyewe kati ya Mhe Mlema na Mhe Marandu mwisho wa siku nccr mageuzi imekuwa ni sawa na bustani nzuri iliyopanda mawe badala ya nafaka.

Nikirejea mada yangu kwa mwenendo wa chadema kwa sasa ni sawa na nccr mageuzi kwani ndanj ya chadema awatakiwi watu ambao watahoji mwenendo wa chama pia awatakiwi kusema ukweli wala kukosoa chochote ndani ya chama kwa maslahi ya chama kwani viongozi waliopo wapo kwa maslahi binafsi na sio kwa wananchi wanyonge wa nchi hii. mfano mzuri mwaka 2006 kabla ya kifo cha Marehemu Chcha Wangwe kutokea alikuwa anaonekana msaliti kwa kuwa tu alikuwa anapinga mwenendo mbovu wa chama kwa kuwa wengi wenu humu ni wadau wazuri wa siasa za nchi hii mnajua nn kililmtokea Wangwe sina haja sana ya kuwarudisha huko, huyu ni mfano wa kwanza ila mwaka 2012's tumeshuudia tena vijana makini ndani ya chama wakifukuzwa kwa kuwa tu walisema ukweli wa mambo ndani ya chama na wengi wenu ni mashahidi juu ya hili vijana hao ni Mtela mwampamba na Jiluana Shonza ambao leo hii ni mwiba kwa chama chetu kwani wanatumia muda wao mwingi kutoa maovu ya chama na wana siri nyingi kwa kuwa wamefanya kazi makao makuu kwa muda usiopungua miaka minne ila kinachonishangaza mm kila anaye sema ukweli ndani ya chama anaonekana ni upande wa Zitto, hivi ni kwa nn? au Zitto pekee ndan ya chama ndio msema ukweli?

kwa upeo wangu nikajua ni porojo tu za Mtela na Shonza juu ya ukilitimba uliopo ndani ya chadema ila mwaka huu wiki tatu zilizopita tumeshuhudia Mwigamba akisimamishwa kwa kuwa alisema uhalisia ndani ya chadema ila kwa mhe Lema kumpiga kiongozi wake kwa kuwa ajagusa maslahi ya Katibu na Mwenyekit hakuna hatua ambayo imechukuliwa kwake. kwamba hiyo aitoshi lema amekuwa kuwa hakitoa tuhuma za kejeli zisizokuwa na ushahidi zidi ya Zitto ambaye ni kiongozi wake wa chama kitaifa hakuna chochote anachoongea katibu wala Mwenyekit wa chadema taifa hii ni kwa maana kwamba awajasema ukweli na kwa kuwa Zitto amekuwa akisema ukweli ndani ya chama ni sawa kuchafuriwa. kwa mwenendo huu wa kutotaka viongozi wa juu kuambiwa ukweli na kukoserewa na kila anayesema ukweli anaonekana ni msaliti wa chama huku ni kujichimbia kaburi mwenyewe na mwisho kuja kulia kilio cha samaki.

Taifa kwanza maslahi binafsi baadae.

[h=2]Tujiandae kuhudhuria mazishi ya CHADEMA[/h]
Leo nimekumbuka kauli ya Jk kuwa vyama vya upinzani ni vyama vya msimu.

Wale tuliokuwa tunategemea ukombozi kupitia CHADEMA tujue "imekula kwetu".

Tumesema na kuonya kuhusu viongozi kulumbana hadharani lakini ni wazi hakuna lililofanyika.

Viongozi wa chama wanaona ila kwa maslahi yao wamekaa kimya!

Alafu hii fukuza fukuza mbona imeshika kasi sana na hutokea pale mwenyekiti wa chama anapokuwepo??!!

Ina maana viongozi hawaoni hatari iliyo mbele kwa chama chetu?

Kama wanaona mbona hawachukui hatua na kwa kuwa hawachukui hatua ni kwa faifa ya nani??!!

Hivi kweli tatizo ni posho tu au kuna agenda ya siri??!!

Joshua Nassari nae kajiunga kwenye hii issuen ili kuleta picha gani na kwa faida ya nani?

Hakika nawaambia CHADEMA imeshakufa "kiroho" ila "kimwili" tuko nayo hivyo tusubiri mazishi siku si nyingi.

Nawatuhumu hawa kwa kuua chama nao ni

1.Mbowe

2.Dr.Slaa

3.Zitto.

Hao wengine wanatumka tu!

5.11.13

Chadema kinakufa huku kinacheka


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

NI dhahiri Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kinakufa huku kinacheka. Kuisema kauli hii kwa Tanzania ya leo, kunahitaji moyo wa chuma. Baadhi ya watu wasiopenda kukoselewa au kuelekezwa jambo wataanza kupayuka. Watapaza sauti zao juu kupinga kila wawezalo.

Ila mwisho wa siku ukweli utadhihiri, maana wahenga wana msemo wao kuwa siku zote majuto ni mjukuu. Kauli hii inatufundisha watu kujifunza vitu kabla ya kuingia kwenye mihangaiko ya moyo. Naitamka kauli hii kwa kuangalia jinsi watu wanavyotaka kuyumbisha mambo na kufikia kuogopa baadhi ya sura ndani ya Chadema.

Kuogopwa kwa watu hao ni kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wake Dk Willbroad Slaa, moja ya watu waliokuwa wakiheshimika na bado baadhi wanamuheshimu hapa nchini. Ukiwa wewe ni kiongozi mdogo upo ndani ya Chadema, utasumbuliwa au hata kuwekwa kando kama utajaribu kukosoa utendaji wa Mbowe na Slaa.

Haya ni matatizo makubwa. Yanahitaji kuangaliwa upya, ili kesho wasijitokeze wale wanaosema ushindi wao umechakachuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wafuasi hao, itabidi waamini kuwa wameshindwa kutokana na mipango na dhamira ya kweli ya kuwaongoza Watanzania.

Chadema sasa kumesheheni makundi. Tena makundi ambayo kwa kiasi kikubwa yanaathiri mfumo mzima wa kiutendaji. Japo wanasiasa wenyewe wanakubali kuwa makundi hayaepukiki, lakini kwa chama kama Chadema, kinahitaji makundi yenye kujenga kwanza.

Wasipojijenga, hata malengo ya kuongoza Dola ni mtihani mzito kwao. Licha ya Chadema kutembea na sera ya kupinga ufisadi, ila ni wazi ndani yao kumesheheni vitendo vya kidhalimu.

Na kwakuwa ufisadi ni jambo pana, basi hapana shaka nao wapo miongoni mwa mafisadi. Ufisadi si kula mali za umma. Ufisadi si kuiba fedha za serikali tu, ila mahala popote panapojumuisha watu wengi. Leo Chadema wapo watu wanaohitaji wakalie nafasi zao miaka kadhaa mbele. Si jambo baya, ila pia taratibu lazima zifuatwe.

Ni aibu kubwa Chadema ambacho ni Chama Kikuu cha Upinzani, kushindwa kujenga hata ofisi zao zinazokwenda sambamba na uhai wao, licha ya kupokea ruzuku zisizopungua Sh Bilioni 9.2 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi 2010.

Chadema ni chama kisichokuwa na mipango ya kujiwekea miradi ya kimaendeleo, badala yake inasubiria ruzuku, michango ya wanachama wake na bado inatumika ndivyo sivyo. Chama kinajiendesha kwa siri siri. Hakuna uwazi wala uwajibikaji. Uwanja wa kuhoji uhalali wa jambo moja hadi jingine ndani ya viongozi hao ni mtihani.

Chadema kwa sasa wanaishi kama samaki, mkubwa anammeza mdogo. Nyuma ya pazia, wao ndio wanaohubiri utawala bora, sera, mipango na kusimamia maendeleo ya serikali, wakati wao wenyewe wanashindwa kujiongoza.

Waliokuwa nje ya uongozi wa Chadema, wafuasi wao wanabaki kudanganywa tu. Tena watu hao wanaodanganya hujificha katika kivuli cha mageuzi, wakiamini kila mtu anataka kuona CCM kikiondoka madarakani.

Kwakuwa baadhi yao wanahitaji kuona CCM kinakuwa pembeni, basi wanaburuzwa mchana na usiku. Wakiambiwa lolote hupiga makofi. Wanainua vidole viwili juu. Wanaimba nyimbo mbaya zinazohusu utawala wa CCM na viongozi wao.

Anayejitokeza kuhoji, anaonekana juha, makuhani. Eti ni mamluki wa CCM. Anaitwa mwajiriwa wa CCM.

Vijana wa leo hasa katika mitandao ya kijamii wanasema buku 7000. Wakimaanisha wapo watu wanaolipwa ujira wa elfu saba kila wanapoipigania CCM.

Kweli? Kwa mwendo huu sidhani kama CCM inahitaji kuwalipa wafuasi elfu saba ili wahubiri mema yao. Si kweli hata kidogo.

Ingawa CCM imeasisiwa tangu mwaka 1977, lakini ina historia nzuri na Taifa letu. Imefanikiwa kuweka utawala bora kiasi cha kukuza vyama vya siasa vya upinzani, kama vile Chama Cha Wananchi (CUF), NCCR Mageuzi, TLP, Chadema, UDP, NRA na vinginevyo vyenye sera na mitazamo tofauti.

Watu walikuwa wakilala barabarani wanaposafiri umbali mrefu, kama vile Mwanza, Kagera, Tabora, Arusha, Mtwara na kwingineko. Leo hii mikoa karibia yote inaunganishwa na barabara za lami na kuna mifumo mizuri ya kiutendaji. Huduma ua umeme na maji inafanyiwa kazi kwa kasi kubwa mno na pia uhalali wa watu kuihoji serikali yao.

Ni tofauti na vyama vya upinzani kikiwamo Chadema, kinachoongozwa na Mbowe. Tangu kianzishwe mwaka 1992, chama hiki ni ngumu mtu kuinua kinywa chake kuhoji utawala wa Mbowe na maswahiba zake ndani ya Chadema. Na ndio maana wengi wanaoinua midomo yao, mara kadhaa huishia nje ya uongozi wa chama hicho, akiwamo Juliana Shonza, Mtela Mwampamba na juzi Samson Mwigamba.

Hii ni mifano iliyotokea ndani ya mwaka huu, hasa baada ya watu hao kuhoji nyendo za viongozi wao. Suala linapopigiwa kelele ni juu ya Mbowe kuiendesha chama kama chake. Wengine wanasema ni chama cha kindugu. Wengine wanasema bila kuwa mtu wa Kaskazini huwezi kuwa na nafasi Chadema.

Na ukiwa si wa Kaskazini, basi inakulazimu kubaki kimya ili usinyang'anywe tonge mdomoni. Ni tofauti na CCM. Japo mfumo huo wakati mwingine haukwepeki, ila bado Mzigua wa Handeni anaweza kuwania nafasi yoyote ndani ya chama hicho au akashauri nyendo zenye kujenga utawala bora bila kufanywa lolote.

Ni jambo la kujiuliza, kama serikali ya CCM na viongozi wake wangekuwa hawataki kusemwa au kushauriwa wangapi wangebaki mtaani?

John Mnyika, Mbunge wa Ubungo ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa Chadema aliibuka akisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ni dhaifu. Aliainisha vipengele vingi na kuzua maswali na wasiwasi dhidi ya nyendo za baadhi ya viongozi wa Chadema. Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi ‘Sugu' naye akaingia kwenye rekodi baada ya kumuita Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa ni '--------'.

Wabunge kama Godbless Lema, Mchungaji Peter Msigwa na wengineo ndani ya Chadema wamekuwa wakibadilishana kauli za ukakasi dhidi ya serikali ya CCM, chini ya Kikwete. Wanaachwa kama walivyo. Lakini maneno hay ohayo wayaseme kwa viongozi wao, Mbowe na Slaa uone watapewa adhabu gani.

Watavuliwa uongozi. Maana mkuki kwa nguruwe. Hii ni kwasababu hakuna utawala bora ndani ya vyama vya upinzani, wakiwamo Chadema. Wao wanaishia kuipigia kelele CCM lakini ndani ya mioyo yao wapo kifedha zaidi. Ni ajabu na kweli. Ndio hapo tunaposhuhudia msuguano wao ukiwa katika mshike mshike wa uenyekiti katika Uchaguzi ambao haueleweki utafanyika lini.

Uenyekiti ambao watu wanahoji jinsi chama cha siasa kisichokuwa na ukomo wa uongozi ndani ya Katiba yao. Kipengele hicho hakijajadiliwa? Kwanini? Ama hakuna anayeweza kuwa mwenyekiti zaidi ya Mbowe na Katibu wake Slaa? Kelele zote zinaelekea kwa Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, akiambiwa ndio anayeongoza kambi inayosumbua chama chake.

Inawezekana, ila kwa sasa hoja ni utawala bora ndani ya Chadema kuwa sifuri. Hoja ni matumizi mabaya ya ofisi na kodi za wananchi. Hoja ni kwa namna gani hakuna utaratibu mzuri wa manunuzi ya vitu vya chama chao?

Ndio maana nasema Chadema kinakufa huku kinacheka. Kifo hiki ni kibaya sana. Maana mtu hajui kama mtu wake anakufa.

Akiangalia kicheko kinavyopamba sura yake, anaona uhai upo. Akija kushtuka, mauti yamemkuta na wanabadilisha jina, kutoka fulani hadi marehemu fulani. Je, Chadema wenyewe wanalijua jambo hili? Je, wamejua kama wanakufa huku wanacheka? Nani atawakomboa kama wenyewe wanatoana roho? Yu wapi mwenye ujasili wa kumwambia Mbowe anaendesha chama ndivyo sivyo?

Thubutu? Hata leo, Lema ni swahiba mkubwa wa Mbowe, lakini akiamua kuhoji mwendo wao mbaya hakika kiti chake kitakuwa kwaheri. Hawezi kusema lolote. Ataendelea kukaa kwenye msimamo wa mwenyekiti wake akiamini maisha yake yanakwenda sawa.

Huu ni wakati wa Watanzania kuwa makini katika kuviangalia vyama hivi vya siasa, ambavyo baadhi yao havina malengo mazuri na Taifa lao. Wanachoweza kufanya ni kuwayumbisha Watanzania kwa kusimamia mambo yenye faida yao, kusimamia migogoro, maandamano kupinga utawala wa sheria wa serikali, wakati wao wenyewe wanashindwa kujiongoza na kusimamia ukweli.

Nakutakia Jumatano njema.
Mungu ibariki Tanzania.
kambimbwana@yahoo.com
+255712053949
 
Same as CCM... wakisha toa Majina ya waliolimbikiza MALI USWIS; Utaona jinsi gani watakavyoanza kugombana...
Na Pesa nyingi ni zile walizopewa na Mchina...

Mbona CUF haina Uchaguzi na Bado Inapendwa huko ILIKO? Ukiangalia VYAMA VINGI VYA KISIASA havina VIONGOZI wa kuchaguliwa kila baada ya miaka kadhaa... Ni hapa tu TANZANIA bado tuanafuata ile tabia ya KI-CUMMUNIST kama CHINA kubadilishana VIONGOZI kama MASHATI... kwani Rais KIKWETE alipita kwa kupendwa au kwa Mizengwe? Mkapa alipita kwa kupendwa au MIZENGWE??? all those are COMMUNIST IDEOLOGIES...

Nipe Chama Chochote Duniani kinachochagua Viongozi wake kwa Mihula kama CCM na CCCP ??? HAKUNA>>>

Mnajua ya kuwa CHADEMA wakichagua VIONGOZI hawatakuwa wa kubebwa kama wa CCM na wanaweza wakawa sio wenye NGUVU kama wa sasa hivyo RAHISI kukipindua...
 
View attachment 117860 4.jpeg
2.jpeg View attachment 117863

Wewe unazungumzia Kufa kwa CHADEMA wakati CCM imeishakufa kitambo kama picha zinacyoonyesha migogoro katika jumuia zake mbalimbali, je Unaweza kuufahamisha umma katika migogolo iliyotokea katika hizo picha kuna ufumbuzi wowote ulipatikana?
Kiuhalisia hizo picha zinaonyesha Misukule ya CCM ilivyo na uchu wa Madaraka.


View attachment 117864

Misukule ya CCM inataka kuuawana katika hizo picha hapo juu huku wenzao kicheko kwa kwenda mbele.
 
nani atatoa majina ya uswis?hakuna atayetoa majina ya uswiss ni sawa na kutoa majina ya wauza unga,Mheshimiwa hata juzi nilisikia anasema yatajeni majina ya wauza unga,wakati alishasema anayo,haki ya mungu hii nchi yetu sijui wananchi wake nao ni wendawazimu ama viongozi wanatuona wendawazimu,
 

Same as CCM... wakisha toa Majina ya waliolimbikiza MALI USWIS; Utaona jinsi gani watakavyoanza kugombana...
Na Pesa nyingi ni zile walizopewa na Mchina...

Mbona CUF haina Uchaguzi na Bado Inapendwa huko ILIKO? Ukiangalia VYAMA VINGI VYA KISIASA havina VIONGOZI wa kuchaguliwa kila baada ya miaka kadhaa... Ni hapa tu TANZANIA bado tuanafuata ile tabia ya KI-CUMMUNIST kama CHINA kubadilishana VIONGOZI kama MASHATI... kwani Rais KIKWETE alipita kwa kupendwa au kwa Mizengwe? Mkapa alipita kwa kupendwa au MIZENGWE??? all those are COMMUNIST IDEOLOGIES...

Nipe Chama Chochote Duniani kinachochagua Viongozi wake kwa Mihula kama CCM na CCCP ??? HAKUNA>>>

Mnajua ya kuwa CHADEMA wakichagua VIONGOZI hawatakuwa wa kubebwa kama wa CCM na wanaweza wakawa sio wenye NGUVU kama wa sasa hivyo RAHISI kukipindua...
Tatizo ni huyo mnayemuona mtakatifu Slaa wa karatu

Hivi wewe kweli na akili zako unakenda kuchangia mafuta ya chopa wakati hata baiskeli huna?

Hawa jamaa wanawachuna bila huruma lakini kwa sababu mko kwenye msukule mode inakuwa ni vigumu sana kushtuka, lakini naamini iko siku mtajitambua tu
 
Back
Top Bottom