Kuna ishara za wazi kabisa kuwa hukitambui vema unachokizungumza. Katiba ya chama iko wazi kabisa juu ya lini uchaguzi unapaswa kufanyika. Chama hakiwezi kufuata maoni ya misukule mnaokesha kukibomoa, chama kinaendeshwa kwa katiba. Katiba hii anayo pia msajili wa vyama vya siasa, na anatarajia chama kifuate taratibu zake ili kutembea ndani ya legal terms. Wanachama wana imani tele na viongozi wao na hawategemei kubadilishwa kifikra na misukule.
Juu ya Auditing, hilo si jipya kama unavyotaka kutuaminisha. Chama kinafahamu umuhimu wa auditing kwa ustawi wake na zaidi sana kwa ustawi wa taifa. Hesabu zote daima ziko wazi na ndio maana hata katika chaguzi, CHADEMA kimeendea kuwa wazi juu ya mapato na matumizi yake. Hili limekuja wakati muafaka kabisa, na baada ya ukaguzi, nadhani utakuwa wa kwanza kutuletea report safi, not because of cooking like what Chama Cha Mapinduzi always does, but because we are worthy it...