Mwigulu Nchemba amcharukia Zitto Kabwe

Mwigulu Nchemba amcharukia Zitto Kabwe

Tatizo la Mwigulu ni nini wakati katiba ndiyo imetoa mwanya huo wa kujadili personality au afya ya kiongozi?, katiba imeyatamka hayo hadharani kwa kila atakayeisoma na tafsiri yake ni kwamba hali ya afya ya kiongozi nayo inapaswa kuwa hadharani .
Ukisha kuwa kiongozi tu tambua kwamba you are open to the public, kama hautaki kujianika au kuanikwa basi usiusogelee uongozi.
Huyu Mwigulu Nchemba akili zake hazipo sawa mahali tangu zamani ni wa kumpuuza tu.
Tuliowahi kusikia mambo ya Zitto enzi zile za yule mbunge mdada aliyefariki, pia tumekuwa na mashaka juu ya ubora wa afya yake siku zote. Nyanja nyingi imekuwa ni vigumu kuthibitisha afya ya mtu labda tu pale anaposhindwa kuinuka.
Je, Zitto afya yake iko sawa?
 
Ninyi hamjamuelewa mwigulu.

Kwa kifupi ni kuwa Mwigulu kafurahishwa na andiko la Zitto,ndio maana kanukuu kila kitu alichoandika ili hata aliepitwa bila kusoma basi apate andiko la Zitto.

Kwa kifupi amerepost ,anafanyia promo andiko la Zitto kijanja
 
Tuliowahi kusikia mambo ya Zitto enzi zile za yule mbunge mdada aliyefariki, pia tumekuwa na mashaka juu ya ubora wa afya yake siku zote. Nyanja nyingi imekuwa ni vigumu kuthibitisha afya ya mtu labda tu pale anaposhindwa kuinuka.
Je, Zitto afya yake iko sawa?
Unaweza ukawa sahihi ila tatizo ni mahali unapoibulia tuhuma zako.
 
Unaweza ukawa sahihi ila tatizo ni mahali unapoibulia tuhuma zako.
NI sahihi! Zitto anajipa uelewa uliozidi kipimo wakati hana uzoefu kiasi hicho. Maana yake kwa ibara hiyo aliyoitaja ilikuwa kuonyesha kwamba rais ana matatizo ya afya.hata kama kwa uhakika ana matatizo ya akili. Sawa je, yeye anayo afya inayomruhusu kuwa mbunge? Yeye ni nani atukumbushe afya ya rais nasi tusimkumbushe afya yake.
 
Ninyi hamjamuelewa mwigulu.

Kwa kifupi ni kuwa Mwigulu kafurahishwa na andiko la Zitto,ndio maana kanukuu kila kitu alichoandika ili hata aliepitwa bila kusoma basi apate andiko la Zitto.

Kwa kifupi amerepost ,anafanyia promo andiko la Zitto kijanja
You are talking something!

Hivi tukiacha ya Mwigula na Zito, afya ya kimwili na/au ya kiakili ya mheshimiwa iko sawa?
 
NI sahihi! Zitto anajipa uelewa uliozidi kipimo wakati hana uzoefu kiasi hicho. Maana yake kwa ibara hiyo aliyoitaja ilikuwa kuonyesha kwamba rais ana matatizo ya afya. kwa uhakika ana matatizo ya akili. Sawa je, yeye anayo afya inayomruhusu kuwa mbunge? Yeye ni nani atukumbushe afya ya rais nasi tusimkumbushe afya yake.
'kwa uhakika anayo matatizo ya kiakili'.

I didn't know but now I know!
 
.....ccm akivaa jezi ya ccm, popote pale inakwaza jambo lolote lisifanyike !? Chadema walikuwa na magwanda yao kwenye msiba wa Capt. Komba. Mbowe anashinda kutwa nzima na magwanda. Dont occupy your head with minor issues !
ndiyo! Inakwaza, hawa watu wa vyama tofauti huwa ni wapinzani popote,pia kuna chuki kubwa miongoni mwa wanachama/viongozi wa vyama hivi,sasa wakikutana sehemu moja mccm na mchadema usitake kujifanya kuwa hujui kuwa hapo kila mmoja anamkwaza mwenzake! Hivyo ni sahihi kabisa kutovaa jezi za utambulisho wa itikadi sehemu za shughuli za kijamii zisizohusiana na vyama vyetu!
 
Yaani utaijuaje afya ya mtu bila kumfanyia vipimo? VIPIMO NDIO VITAJIBU MASWALI YAKO. Wakati mwingine kaa kimya ufiche. ZITTO yuko sahihi na ana haki ya kikatiba ya kujua afya ya akili na mwili ya kiongozi wake. Ni nini mnaficha hapa? Mbona watu wamekosa kujiamini?
Wamesahau enzi za Push up jukwaani na Kebehi kwa Lowassa ...........!!
 
Msumari unatokea ulipoingilia.. Kipindi mnapiga push up hamkujua haya..ibara iliyotajwa itumike kwa usahihi..
 
Kivuko ni kibovu,hamsikii.
Ya kutokea yametokea sasa mkiambiwa mnahamisha magoli.
Acha kila mtu aambiwe ukweli wake kwa sababu watu wamewachoka.

Mongela kapata maagizo toka juu kwamba waache uokoaji giza limeingia, wewe Mwigulu unaona hiyo ni akili ya mtu aliye timamu kweli?
msitusababishie majanga sisi.

Mmeshindwa kuishi in reality, mnategemea life ya kutoa kafara to survive, naomba tena ujinga wenu isiwe majanga kwetu.
Hili la kutoa kafara ni jambo zito sana. Yaani watanzania tungemgeukia Mungu kiuhalisia wasingeweza kututoa kafara kwa Lucifer kirahisi hivi.
 
ndiyo! Inakwaza, hawa watu wa vyama tofauti huwa ni wapinzani popote,pia kuna chuki kubwa miongoni mwa wanachama/viongozi wa vyama hivi,sasa wakikutana sehemu moja mccm na mchadema usitake kujifanya kuwa hujui kuwa hapo kila mmoja anamkwaza mwenzake! Hivyo ni sahihi kabisa kutovaa jezi za utambulisho wa itikadi sehemu za shughuli za kijamii zisizohusiana na vyama vyetu!
Hiyo ni shida yako, 'makwaziko' yako si sheria na wala huwezi mpangia mtu atakacho kuvaa !
 
Kumbe na wewe umegundua hila za hawa wanasiasa ...
Itakuwa kweli anachosema Zitto............

Ila Mwigulu mjanja, ameamua kukuza mgogoro ili aonekane anamtetea mkuu, kumbe lengo lake ni huu mjadala uendelee kukua ili mkuu aendelee kuzalilika....
 
Hiyo ni shida yako, 'makwaziko' yako si sheria na wala huwezi mpangia mtu atakacho kuvaa !
Ume oversimplify, we hujui kwa nini misikitini wanaume na wanawake wanawekwa tofauti? Au ni kwa ajili ya "shida zao"?
 
Zitto Kabwe, na wenzako mnaoendelea kusambaza thread hii, With due respect to you, let us debate on Agendas, National issues and NOT PERSONALITIES. My collegemate, my agemate, my felloweconomist, mwanadamu mwenzangu: Where is the limit?

Nimesoma thread yako, na nimesoma kipengele cha Katiba ulichokitaja. AMBAYO IKO KWENYE THREAD; "Ni muda mwafaka SASA Baraza la Mawaziri kutumia Ibara ya 37(2) ya Katiba. Kwenye Katiba, maudhui ya Ibara hiyo ni"
37(2), Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya Maradhi ya MWILI au AKILI, laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba kwa sababu ya Maradhi ya Mwili au ya Akili hawezi kumudu kazi zake. " .......
.......
Mwanzo nilidhani ID feki, pili nikadhani wamekulisha maneno, but sijaona ukikanusha. Well ukiwa na jazba unaweza kuandika hivyo na yeyote mwenye jazba anaweza kufurahia hicho. But let us get back to the sense of humanity;

1) Taifa linapita kwenye janga, limepoteza watu, watu wako kwenye majonzi, Kiongozi ambaye ndio anadhamana ya watu wote yuko kwenye kipindi cha kupoteza watu kwenye janga hilo, msiba huo ni wake, wewe badala ya kumpa pole, any word of hope, unaweka neno ambalo impliedly unataka kuaminisha watu kuwa Rais anaumwa, maradhi ya mwili au ya akili. The timing and allegation haina chembe ya ubinadamu.

2) Hata kama, kuna mapungufu kwenye kuruhusu watu kupanda au vyovyote, ustaarabu wetu unatuonesha TUWAHIFADHI KWANZA NDUGU ZETU, NDIO TUANZE KUGOMBANA, kama ni kusingiziana au mirathi, nk, SOTE TUTAKUFA SIKU MOJA, hata sasa, Hii sio sherehe, badala ya kuwafariji ndugu, jamaa na wote waliokutwa na janga hili, we feel tumepata mwanya wa kupenyeza maneno. Hatuwatendei haki wale walio kwenye deep pain ya janga hili.


3) Hata kama kwenye siasa kuna kusemana, hata kama kwenye siasa kuna kushambuliana, hata kama kwenye siasa kuna kuchukiana, Maneno yanayolenga personalities za aina hii, tena za maswala ya kiafya, kwa kiongozi, maneno yanayoweza kusababisha taharuki kwenye familia, kwa wananchi na maneno yanayojeruhi personalities, ni adui mkubwa wa uhuru wa kuongea na ustawi wa demokrasia unaopiganiwa.

4) Mimi najua status ya afya yangu, mke wangu na watoto wangu, Je nina haki ya kujua status ya afya yako Zitto? Ni haki ya kuifanya public na nije kuwashauri wapiga kura wako? Brothers and sisters lets observe humanity.

5) Nini tafsiri sahihi ya kipengele hicho cha Katiba,? Hujakielewa, au unatumia Katiba kutukana, kudhalilisha, kuaminisha kitu kisicho na ukweli.

"KITU NISICHOTAKA KUTENDEWA HUWA SITAKI NA MWINGINE ATENDEWE, Huyu ni Kiongozi wetu, Huyu ni Baba yetu kwa umri, Hii ni nembo yetu as a Nation, can you just say like that? can you just wish like that? Oooh No!

Dkt Mwigulu Nchemba, (MB) Iramba.
Dr.na Mh. Mwigulu Nchemba,ni kweli kabisa kwamba sense of humanity ni muhimu sana tunapokuwa kwenye majonzi,lakini hii "sense of humanity" ni kwa baadhi ya raia au ni kwa raia wote?
Alipofariki mwanafunzi mwenzetu Akwilina Akwilin,ulijitokeza na kuzungumza kwa dharau sana,kwamba Abdul Nondo aliposema waziri ajiuzulu kutokana na kifo cha Akwilina,eti ulidhani anamaanisha waziri wa UDSM ajiuzulu kwa kifo cha Akwilina,Kweliiiii!????

Aliposhambuliwa kaka yako wa huko kwenu,Tundu Lissu,uliendelea kutuonyesha jeuri ya kimadaraka,ndani ya bunge na nje ya bunge pia,wengine tukahisi na tumeendelea kuhisi kuwa Siri ya shambulio dhidi ya Tundu Lissu,"labda" wewe pia unaijua vizuri!

Hata kama Zitto Kabwe amekosea,au amekosa sense of humanity,WEWE HAUNA MORAL AUTHORITY ya kumnyooshea kidole,kwa sababu hiyo "sense of humanity" wewe hauna kabisa,sio tu kwa maneno yako lakini pia kwa matendo yako!!!!

Better you shut up your mouth,Hon.
 
Back
Top Bottom