Mwigulu Nchemba amcharukia Zitto Kabwe

Mwigulu Nchemba amcharukia Zitto Kabwe

Safi sana Mh. kwa kuwapa jibu zuri

Hao walafi wa upinzani wao hawajali wananchi bali matumbo yao tu.
 
Kosa la Zitto ni Nini?
Ku resite katiba?
Naangalia TBC two hapa simuoni huyo unayesema msiba unamhusu, au macho yangu?
Ukweli mchungu ni kuwa, hili janga lililotokea haliwezi kuwatoa kisiasa pamoja na huyo Zitto. Yeye ndio kakwama zaidi kwasababu ya hulka yake ya usaliti(mfano alichoifanyia CDM uchaguzi wa Rais 2010). Kingine ni imani yake kuwa yeye ni mwerevu sana kuliko wenzake. Kisiasa kwake ni machweo.
Kilichobaki ni kutishia watu kuwaroga na “kuwafariji” wajane wa marafiki zake. Huo ni mtazamo wangu tu.
 
Kosa la Zitto ni Nini?
Ku resite katiba?
Naangalia TBC two hapa simuoni huyo unayesema msiba unamhusu, au macho yangu?
Hapo kwenye red mkuu, yuko huku tumemaliza kunywa naye chai alivyotoka kanisani!!
 
Akiwa waziri was mambo ya ndani,Tanzania imeshuhudia mauaji makubwa ya watanzania na kutupwa baharini kwenye mifuko
 
Zitto Kabwe, na wenzako mnaoendelea kusambaza thread hii, With due respect to you, let us debate on Agendas, National issues and NOT PERSONALITIES. My collegemate, my agemate, my felloweconomist, mwanadamu mwenzangu: Where is the limit?

Nimesoma thread yako, na nimesoma kipengele cha Katiba ulichokitaja. AMBAYO IKO KWENYE THREAD; "Ni muda mwafaka SASA Baraza la Mawaziri kutumia Ibara ya 37(2) ya Katiba. Kwenye Katiba, maudhui ya Ibara hiyo ni"
37(2), Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya Maradhi ya MWILI au AKILI, laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba kwa sababu ya Maradhi ya Mwili au ya Akili hawezi kumudu kazi zake. " .......
.......
Mwanzo nilidhani ID feki, pili nikadhani wamekulisha maneno, but sijaona ukikanusha. Well ukiwa na jazba unaweza kuandika hivyo na yeyote mwenye jazba anaweza kufurahia hicho. But let us get back to the sense of humanity;

1) Taifa linapita kwenye janga, limepoteza watu, watu wako kwenye majonzi, Kiongozi ambaye ndio anadhamana ya watu wote yuko kwenye kipindi cha kupoteza watu kwenye janga hilo, msiba huo ni wake, wewe badala ya kumpa pole, any word of hope, unaweka neno ambalo impliedly unataka kuaminisha watu kuwa Rais anaumwa, maradhi ya mwili au ya akili. The timing and allegation haina chembe ya ubinadamu.

2) Hata kama, kuna mapungufu kwenye kuruhusu watu kupanda au vyovyote, ustaarabu wetu unatuonesha TUWAHIFADHI KWANZA NDUGU ZETU, NDIO TUANZE KUGOMBANA, kama ni kusingiziana au mirathi, nk, SOTE TUTAKUFA SIKU MOJA, hata sasa, Hii sio sherehe, badala ya kuwafariji ndugu, jamaa na wote waliokutwa na janga hili, we feel tumepata mwanya wa kupenyeza maneno. Hatuwatendei haki wale walio kwenye deep pain ya janga hili.


3) Hata kama kwenye siasa kuna kusemana, hata kama kwenye siasa kuna kushambuliana, hata kama kwenye siasa kuna kuchukiana, Maneno yanayolenga personalities za aina hii, tena za maswala ya kiafya, kwa kiongozi, maneno yanayoweza kusababisha taharuki kwenye familia, kwa wananchi na maneno yanayojeruhi personalities, ni adui mkubwa wa uhuru wa kuongea na ustawi wa demokrasia unaopiganiwa.

4) Mimi najua status ya afya yangu, mke wangu na watoto wangu, Je nina haki ya kujua status ya afya yako Zitto? Ni haki ya kuifanya public na nije kuwashauri wapiga kura wako? Brothers and sisters lets observe humanity.

5) Nini tafsiri sahihi ya kipengele hicho cha Katiba,? Hujakielewa, au unatumia Katiba kutukana, kudhalilisha, kuaminisha kitu kisicho na ukweli.

"KITU NISICHOTAKA KUTENDEWA HUWA SITAKI NA MWINGINE ATENDEWE, Huyu ni Kiongozi wetu, Huyu ni Baba yetu kwa umri, Hii ni nembo yetu as a Nation, can you just say like that? can you just wish like that? Oooh No!

Dkt Mwigulu Nchemba, (MB) Iramba.
 
Tatizo nyie ndio mnalazimisha watu kupandikiza chuki. Serikali hii haiwapendi baadhi ya watu kwa tofauti za kiitikadi. Sasa ndio mapenzi yalazimishwe
 
Hmm! Kwa uandishi huo iko kazi, nina shaka kama aliyeandika hapo ni Dk. Mwigulu Nchemba (Ph.D)... Nasema tena siamini...
 
Zitto amekosea sana,lkn mweshimiwa mwigulu usiwe msahaulifu kiasi hicho,kumbuka mauaji ya Bomu Kule Arusha(Soweto) njinsi ulivyobwabwaja!kweli kwenye awamu hii kila mnafiki ataongea ili tu mkulu amuone.ccm oyeee
 
Mwigulu acha upumbavu wako, haya mambo yamesemwa since before

Kivuko ni kibovu,hamsikii.
Ya kutokea yametokea sasa mkiambiwa mnahamisha magoli.
Acha kila mtu aambiwe ukweli wake kwa sababu watu wamewachoka.

Mongela kapata maagizo toka juu kwamba waache uokoaji giza limeingia, wewe Mwigulu unaona hiyo ni akili ya mtu aliye timamu kweli?

Ujinga, upumbavu, ukicha wenu msitusababishie majanga sisi.

Mmeshindwa kuishi in reality, mnategemea life ya kutoa kafara to survive, naomba tena ujinga wenu isiwe majanga kwetu.

Kichaa aondolewe mapema kuepuka majanga zaidi.
File la kichaa pale Bugando lirudishwe na aendelee na matibabu ya akili kama kawaida

Tunasema, Think like there’s no Box at all....

Ame Bold kauli ya zito ama amepigilia Mstari....
 
Mods, naomba msiunganishe hii mada.

Brother Mwigulu, si sahihi kabisa kuhusisha tweet ya Zitto kuhusu ibara hiyo ya katiba na swala zima la ajali ya kivuko cha Mv.Nyerere.

Watu wengi hawaelewi kuwa ile tweet Zitto aliipost tarehe 20/09//2018 saa saba na dakika thelathini na mbili mchana (1:32 PM) wakati ajali ilitokea saa nane kamili mchana kwa mujibu wa RPC (someni uzi wa ajali ulioko hata hapa JF kuona kauli hiyo ya RPC) na hapo bado huja-consider muda wa taarifa kusaambaa na mpaka watu kuanza kujadili akiwemo huyo Zitto.

Binafsi ile tweet ya Zitto niliona siku moja kabla haijaletwa hata hapa JF na kwa mazingira ya siku ile, inaonyesha Zitto aliguswa na document fulani ambayo wengi iliwashitua na hata hapa JF iliibua mjadala mzito kuhusu maswala ya family planning.

Brother Mwigulu, kama ungeongelea ile tweet ya Zitto kuhoji kuhusu maswala ya kununua Dreamliner, maSGR huku tukishindwa kuoko watu, hapo ungekuwa unaongelea tweet sahihi iliyohusiana na maswala ya ajali lakini sio ile tweet yake kuhusu ibara ya 37 (2).

Tuweke kumbukumbu sawa na tuache kutafuta huruma kutoka kwenye jamii.
 
Mwigulu hushamwaga uwaziri hata useme vipi haurudishwi tena 😀😀😀😀😀😀😀.
 
Mwigulu ushamwaga uwaziri hata useme vipi haurudishwi tena 😀😀😀😀😀😀😀.
 
Back
Top Bottom