Lengo na maudhui ya Mwigulu ni kukitabiria CHADEMA mabaya kwani wengi wetu twamchukulia mbwa kama ishara ya ubaya. Kwahilo hata mwenyekiti wake, JK na CCM watamchukia kwa hofu kubwa ya revenge ya wanaCDM. Nasikitika nyota yake Mwigulu imeshaingia gizani kwa laana ya wanyama na watanzania wa leo wanaoamini ukombozi wao uko mikononi mwa CHADEMA. Pole ndugu Mwigulu, ungehamisisha wanakijiji kujenga japo chumba kimoja cha walimu kule kijijini kwetu ingelipa zaidi.
Kwa upande mwingine kiuwkeli Mbwa ndiye mnyama pekee anayeheshimika na kupewa malazi bora, lishe bora, elimu hususan ya ulinzi na maisha bora. Ndiye mnyama ambaye hapendi uchafu ukiwemo nguvu za giza n.k. Uchafu huo CDM haumo. Hivyo kwa walewa wa wanyama hususan mbwa na paka. Umekipaisha CDM kwasana.
Kwakuwa ulikuwa na lengo baya kwa mnyama huyo, tunakushukuru sana Mwigulu kwa kutuonyesha tena kuwa tulikuchagua kwa makosa, hukustahili hata kidogo kuwa hata balozi wa nyumba kumi na tunakuahidi kuwa hatutorudia makosa hayo 2015.