Kama kuna watu wana njama za 2025, mbona wakati wenyewe ndio huu sasa!
Hao akina Mwigulu na wengine wote kama wapo, wenye kutafuta huo urais, kuwaondoa wakati huu kwenye nafasi wanazoshikilia ni kama kuwapa fursa nzuri ya kuutafuta urais bila ya mizengwe ya uwaziri.
Lakini ninajiuliza sana kuhusu hawa watu wengi wanaoigiza siku hizi.
Nikimkumbuka Profesa wa Jalalani alivyokuwa akivimba na "uzalendo" nyakati zile, ungedhani wakati huu ndiyo angekuwa moto kwelikweli kuuonyesha 'uzalendo' wake watu wauone, lakini wapi!
Watu wote ndani ya CCM nikama wategemea fadhira tu, hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kusema anaweza kusimamama na watu wampime.
Wote, hata akina Magufuli, walikuwa wa aina hiyo hiyo, hadi walipobahatisha tu kuopolewa ndipo wakawa moto unaounguza hovyo kila sehemu.