Mwigulu akaliwa kooni Ufisadi

Mwigulu akaliwa kooni Ufisadi

Mwigulu ni Waziri smart kuliko Mawaziri wote
Mkuu 'Econo', mimi siujui u-'smart' wa Mwigulu, lakini nimevutiwa sana na huo msemo chini ya jina lako.

"Agoal without a plan..." ukanifanya niyakumbuke mengi ya nchi yetu.

Nchi yetu inayo malengo, na wengi wa hao viongozi watakwambia 'plan' pia zipo kedekede.

Tulikuwa/tuna malengo ya 2025 tuliyojipangia toka 2020; na sasa yanatayarishwa mengine ya 2045(?), hata bila kujua haya tunayoyahitimisha tumeyatekeleza kwa ufanisi kiasi gani!

Bila kutaka kukuchosha, mkuu wangu, nadhani hayo maneno ya mstari huo chini ya jina lako hayatuhusu sisi. Sisi ni viumbe tofauti sana na hao wanaoweka malengo na kuainisha mipango ya kuyakamilisha hayo malengo.

Tatizo letu kubwa kama nchi linaanzia hapa, na natumaini kutakuwepo na siku utaleta mada hapa JF tuijadili kuhusu hayo maneno uliyoweka hapo.
 
Mzaha mzaha mwisho utunga usaha.

Kama ni kweli bunge litakuwa seriously safari hii namuona Mwigulu akirudi jimboni mapema.

Wabunge wengi waliochangia ripoti ya CAG wameelekeza lawama zote kwa waziri wa fedha wakisema kuwa yeye ndiye mlipaji mkuu wa serikali.

Sasa sijui kama huu moto ulioanza kukolea pale mjengoni kutamuwacha salama kaka yetu Maderu.View attachment 2578425
"Stupid" natamani sana "Prof. Mussa Assad" ateuliwe waziri wa fedha yule bwana anahofu ya Mungu.
 
Wanamsingizia tu mwigulu nchemba.mwenye makosa ni rais ambaye aliidhinisha matumizi mabaya ya pesa za umma.Ni bora rais ajiuzulu ili nchi inemeeke.
 
Kama imekuwa hivyo ni jambo la heri kuachia mwenyewe kwa sababu, mosi majority if not all ni wabunge wa chama chake sioni kama kuna kuoneana hapa pili he’s rich already hahaha…. Joke. He has to go.
 
Kama imekuwa hivyo ni jambo la heri kuachia mwenyewe kwa sababu, mosi majority if not all ni wabunge wa chama chake sioni kama kuna kuoneana hapa pili he’s rich already hahaha…. Joke. He has to go.
Wala siyo joke
 
Ndio maana ya kuwa na wateule na wasaidizi, Je wadhani rais anauwezo wa kusoma documents zote ndani ya nchi hii?...... Ndio azisahini?, nini maana ya kuwa nanwasidizi waaminifu WATEULE WA RAIS?
Ndio anatakiwa azisome. You cant just sign.
 
Haiwezi kufaulu maana waliopanga hakuna hata mmja anaweza thibitisha Mwigulu alipoiba pesa.

Sababu pekee waliyonayo ni kusema malipo yanachelewa Wizara ya Fedha na hivyo kuleta riba but hili nalo sio la Mwigulu Bali mlipaji Mkuu wa Serikali..

Wengi wanaomkomalia Mwigulu ni chuki binafsi ila hawana hoja, nadhani Rais asiwasikilize awapuuze tuu maana so far Mwigulu amefanya vizuri sana kwenye Uchumi kuliko Mawaziri wengi wa Fedha niliowahi kuwashuhudia.
Wee kipofu umelipwa shilingi ngapi? kwa nchi nyingine waziri wa fedha akianza kulalamikiwa hata kama ni mambo binafsi uchumi wa nchi uporomoka hasa sarafu, sijui kwetu hali ikoje.
 
Tanzania inabahati mbaya sana ni sawa na ng'ombe wa masikini! Kama ilivyo ada kwamba, ng'ombe wa masikini hazai, akizaa huzaa dume!

Tanzania Imekosa kuingo mhimu sana temu hii, hatuna Waziri wa Mapesa sisi!

Aliyepo ni bora liende, hawezi kumsaidia mama!

Ni sawa na mwanake anayemkataa mwanaume mwenye vision ila anataka mwanaume mwenye television, hajui kwamba huyo mwanaume mwenye vision itatokea amuone kwenye television ya mwaume wake!

Nahisi hata sisi kama nchi, tumewakataa watu wenye taaluma zao tukataka watu wenye mataaluma! Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa aisee
.....Aliyepo ni bora liende, hawezi kumsaidia..... (Msaada utoke wapi !!? Labda uwe na maslahi binafsi maana hili ndio kipaumbele !!!)
 
Wee kipofu umelipwa shilingi ngapi? kwa nchi nyingine waziri wa fedha akianza kulalamikiwa hata kama ni mambo binafsi uchumi wa nchi uporomoka hasa sarafu, sijui kwetu hali ikoje.
Mimi sio mjinga kama wewe Wala Huwa sijadili issue binafsi Wala silipwi, kwani wewe umelipwa bei gani?

Leta hoja inayoonesha Waziri wa Fedha amehusika na Ufisadi sio Kuzunguka zunguka,kupatuka bila ushahidi Kwa sababu za chuki binafsi.

Tanzania sio Nchi zingine ndio maana hakuna athari yeyote Kwa sababu za kizushi, na Kwa taarifa Yako hizo Nchi nyingine Huwa inategemeana na scenario na economic/market interdependence hasa stock markets ambayo Tanzania ni ya mwisho hapa EAC.
Nchi imejaa mbumbumbu kama nyie stock markets haiwezi kukua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom