Mwezi wa Ramadhani: Mambo 6 yanayobatilisha swaum yako

JumaKilumbi

JF-Expert Member
Sep 7, 2022
432
506
(Ramadan Kareem 🌙)

Na, JumaKilumbi.

D49608FA-BB7F-4380-A0AD-4DA4C5E1E9E4.jpeg

1. KULA AU KUNYWA WAKATI WA FUNGA
Kitu chochote iwe kinywaji au chakula kikipita ktk koo la mfungaji huhesabiwa amefungua swaum. Hii haihusishi vile vinavyoishia kwenye ulimi bila kupita na kuteremka kooni.

2. KUFANYA MAPENZI WAKATI WA FUNGA, NA KUSISIMKA KIMAPENZI MPAKA KUFIKA KILELE CHA HISIA
Funga inahusu kujizuia tamaa zote za kimwili kwa ajili ya Allah, mfungaji akishiriki tendo la ndoa na mkewe/mumewe au mtu yoyote basi funga yake inabatilika na akifanya hivyo analazimika Kuendelea na funga, na Ramadhani itakapokwisha anatakiwa, ikiwa anaweza, afunge siku 60 mfululizo kama hawezi basi atoe sadaka ya chakula cha kuwalisha watu 60!

Mtu anaefanya punyeto ilhali kafunga, aidha kwa kumshika mkewe/mumewe, kufikiria mambo yanayomsisimua, na kujishika sehemu zake za siri mpaka akafika kilele cha hisia (manii kumtoka) basi funga yake itabadilika.

Kama manii hayakutoka ila yakatoka madhii (majimaji) basi funga yake ni halali na aendelee kufunga.

Kwa aliyetokwa manii ameharibu funga na inampasa kuilipia ile siku baada ya Ramadhan bila kutoa sadaka yoyote.

3. KUJITAPISHA
Mtu aliyefunga kisha kwa makusudi akajitapisha aidha kwa kunusa vitu vyenye kutia kinyaa kwa makusudi au kwa kuingiza kitu kooni mwake anabatilisha Swaum yake.

Ila kwa ambae kichefuchefu kimempata ghafla na wala hajajilazimishabasi asijizuie kutapika na akitapika Swaum yake inaswihi.
(Al Tirmidhiy: 720)

4. KUTOKWA DAMU NYINGI MWILINI
Aidha kwa kutoa damu kuchangia kwa mtu mwingine au kupata jeraha litakalopelekea mfungaji kutokwa na damu nyingi, nyingi kiasi kwamba ikamfanya awe dhaifu, hii hubatilisha swaum.

5. KUPATA HEDHI (kwa wanawake)
Mfungaji mwanamke hubatilika swaum yake pindi anapopata ada yake ya mwezi. Lakini anawajibika kulipia siku ambazo hakufunga baada ya Ramadhani.

6. KUCHOMWA SINDANO
Kuna makundi mawili ya Sindano:
a) Sindano yenye dawa inayoupa mwili nguvu (glucose n.k)
b) Sindano yenye dawa za kawaida (insulin, penicillin n.k)

Kundi (a) linabatilisha swaum na kundi (b) halibatilishi swaum

Inashauriwa kuwa kama itafaa ni vyema mtu achomwe sindano wakti ambao si wa kufunga, kama vile Usiku.

RAMADAN KAREEM ☪️
(E Mwenyezimungu tukubalie Funga zetu🤲)
 
Kwahiyo kama muislam yuko kwenye dozi ya mseto, inabd amumunye zile vidonge zote 4?
 
Mtoa mada naomba unisaidie kuyafahamu mavazi sahihi ya mwanamke wa kiislamu nitashukuru sana..huku mtaani hata sielewi kipi ni kipi.
 
Kwani ni adhabu? Kufunga si jambo la kiroho la mtu?
Si adhabu, kwa watu wenye afya njema ni faradhi kwao kufunga.

“Enyi mlioamini mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kuwa wachamungu.
(Surat Al-Baqarah 2:183)
 
Mtoa mada naomba unisaidie kuyafahamu mavazi sahihi ya mwanamke wa kiislamu nitashukuru sana..huku mtaani hata sielewi kipi ni kipi.
“Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika kawaida tu. na wakwe zao, na wana wao, na wana wao wa kambo, na ndugu zao, na wana wa ndugu zao, au wana wa dada zao, na wanawake wenzao, na watumwa wa kike katika milki zao, na watumwa wanaume wasio na tamaa, au watoto wasio na habari. wa uchi wa wanawake. Wala wasikanyage miguu yao kwa kujipamba kwa mapambo yao yaliyofichika. Tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufaulu.”

Quran 24:31

Kwenye Uislam mwili mzima wa mwanamke ni utupu isipokuwa viganja vyake vya mikono na uso wake, hivyo inampasa kuvalia nguo yenye kusitiri mwili wake wote isipokuwa viganja vya mikono na uso wake tu.
 
(Ramadan Kareem 🌙)

Na, JumaKilumbi.

1. KULA AU KUNYWA WAKATI WA FUNGA
Kitu chochote iwe kinywaji au chakula kikipita ktk koo la mfungaji huhesabiwa amefungua swaum. Hii haihusishi vile vinavyoishia kwenye ulimi bila kupita na kuteremka kooni.

2. KUFANYA MAPENZI WAKATI WA FUNGA, NA KUSISIMKA KIMAPENZI MPAKA KUFIKA KILELE CHA HISIA
Funga inahusu kujizuia tamaa zote za kimwili kwa ajili ya Allah, mfungaji akishiriki tendo la ndoa na mkewe/mumewe au mtu yoyote basi funga yake inabatilika na akifanya hivyo analazimika Kuendelea na funga, na Ramadhani itakapokwisha anatakiwa, ikiwa anaweza, afunge siku 60 mfululizo kama hawezi basi atoe sadaka ya chakula cha kuwalisha watu 60!

Mtu anaefanya punyeto ilhali kafunga, aidha kwa kumshika mkewe/mumewe, kufikiria mambo yanayomsisimua, na kujishika sehemu zake za siri mpaka akafika kilele cha hisia (manii kumtoka) basi funga yake itabadilika.

Kama manii hayakutoka ila yakatoka madhii (majimaji) basi funga yake ni halali na aendelee kufunga.

Kwa aliyetokwa manii ameharibu funga na inampasa kuilipia ile siku baada ya Ramadhan bila kutoa sadaka yoyote.

3. KUJITAPISHA
Mtu aliyefunga kisha kwa makusudi akajitapisha aidha kwa kunusa vitu vyenye kutia kinyaa kwa makusudi au kwa kuingiza kitu kooni mwake anabatilisha Swaum yake.

Ila kwa ambae kichefuchefu kimempata ghafla na wala hajajilazimishabasi asijizuie kutapika na akitapika Swaum yake inaswihi.
(Al Tirmidhiy: 720)

4. KUTOKWA DAMU NYINGI MWILINI
Aidha kwa kutoa damu kuchangia kwa mtu mwingine au kupata jeraha litakalopelekea mfungaji kutokwa na damu nyingi, nyingi kiasi kwamba ikamfanya awe dhaifu, hii hubatilisha swaum.

5. KUPATA HEDHI (kwa wanawake)
Mfungaji mwanamke hubatilika swaum yake pindi anapopata ada yake ya mwezi. Lakini anawajibika kulipia siku ambazo hakufunga baada ya Ramadhani.

6. KUCHOMWA SINDANO
Kuna makundi mawili ya Sindano:
a) Sindano yenye dawa inayoupa mwili nguvu (glucose n.k)
b) Sindano yenye dawa za kawaida (insulin, penicillin n.k)

Kundi (a) linabatilisha swaum na kundi (b) halibatilishi swaum

Inashauriwa kuwa kama itafaa ni vyema mtu achomwe sindano wakti ambao si wa kufunga, kama vile Usiku.

RAMADAN KAREEM ☪️
(E Mwenyezimungu tukubalie Funga zetu🤲)
MashaaAllah
Baaraka Llahu Fiikum
 
Back
Top Bottom