Mwenzi mwenye mtoto nje ya ndoa

Mwenzi mwenye mtoto nje ya ndoa

Sasa kwa nini na ninyi wanaume msijipange mnapojiandaa kwa sex? Kwanini usitumie kinga kama hutaki mtoto? Na kama mtoto amepatikana kwa nini usiwe na mpango mzuri wa malezi? Badala ya kujifanya kughafirika as if uliposex haukujua kama kuna product inaweza kutengenezwa
Mkuu, kuna sex zipo intended kwa starehe tu na si vinginevyo. Ukipata mimba tunashukuru ila tusigandane. Ila huduma utapata kama kwaida
 
Okay...naelewa ila tu najaribu kuwaza possibility nyingine za mazingira mazuri ya kumlea mtoto.

Sasa kwa namna unavyodhani, je ni heri mtoto alelewe na mama yake huko huko, na wewe unakula bata kwenye ndoa pengine? Je utaendelea kuwasiliana na kukutana na mama mtoto? Uko tayari kumshirikisha mkeo wa ndoa juu ya mawasiliano yako na mama mtoto? Je kwenye events muhimu za mtoto kama arobaini, kipaimara, ubarikio, ndoa, graduations,....je utahudhuria? Watoto na mke wako wa ndoa utawashirikisha?
Mama mzazi ndo mlezi mzuri zaidi wa mtoto kws hiyo ni heri akaendelea kishi na mama yake. Disavantage atakayopata huyo mtoto ni kutopata my full attention kwa sababu siwezi kujigawa. Mambo yake mengi sitahudhuria especially kama tunakaa mbali mbali.
Mke wangu mpya lazima ajue kila kitu ili kuwe na amani, akitaka kujihusisha sana na hayo mambo anakaribishwa.
Umeolewa?
 
Mmh hawajuagi kusema "NO", na pia they will never admit kuwa na wao walikosea pia kwa kutokuwa na misimamo. Muda wote wanataka kuonekana ni victims tu, walisukumwa. Wao huwa hawana choices ila huwa "wanajikuta" yameshatokea. Sipendi mtu who put blames others as if yeye hana ufahamu wa kufanya maamuzi sahihi, na since wanajua sana kujiendekeza wacha waendelee kusuffer consequences za choices za wengine. Mtoto wa kwanza walijikuta, na wa pili wamejikuta tu tena, bado mtu anamlaumu tu mwenzie, haoni kuwa na yeye ni reckless kufall into her traps all the time. Soon watajikuta wana mtoto wa watu. Namuonea tu huruma huyo mume
Wahenga walisema maji hufuata mkondo! Umesahau visingizio vyao vilianzia huko bustanini kwa babu Adam, so hakuna namna acha waendeleze libeneke.
 
Kuna demu mmoja mke Wa mtu ana watoto 5 kwenye ndoa yao.
mwaka 2014 tulianza mahusiano ya siri baadae akasema anafanya hivyo kisa mumewe mkali anampiga kila Mara zaidi zaidi hamridhishi kimapenzi
Baada ya wiki akapata mimba Na mtoto anafanana Na Mimi hadi naogopa.Kuja hapa nilipo anapanda basi mwendo Wa saa mbili,anakuja anashinda saa kumi anarudi
Siku moja akapaki kila kitu Na kuachana Na mume wake waliejenga nae nyumba 2 Na miradi kadhaa nikashangaa fuso inapaki nje ya ghetto langu vitu vingine ilibidi tuweke kwa mwenye nyumba maana Nina chumba Na sebule tu.
Watoto wote 5 wako kwa mume wake hapa kaja Na yule niliezaa nae
[emoji1] [emoji1] hatari!
 
Mama mzazi ndo mlezi mzuri zaidi wa mtoto kws hiyo ni heri akaendelea kishi na mama yake. Disavantage atakayopata huyo mtoto ni kutopata my full attention kwa sababu siwezi kujigawa. Mambo yake mengi sitahudhuria especially kama tunakaa mbali mbali.
Mke wangu mpya lazima ajue kila kitu ili kuwe na amani, akitaka kujihusisha sana na hayo mambo anakaribishwa.
Umeolewa?

Yeah ni vizuri kuweka wazi kila kitu ili huyo mtarajiwa ajue kama kusuka au kunyoa. Umenichekesha hapa "....akitaka kujihusisha anakaribishwa". Sijaolewa.
 
Wahenga walisema maji hufuata mkondo! Umesahau visingizio vyao vilianzia huko bustanini kwa babu Adam, so hakuna namna acha waendeleze libeneke.
Wanachosha hawa viumbe. Yani yeye kajiweka kwenye utakatifu afu makosa yote kambebesha baby momma wake. Sijui hana uchungu na watoto wake pia, naona kaamua kuwa tu kuwa sperm donor, mume mwenzie atalea
 
Yeah ni vizuri kuweka wazi kila kitu ili huyo mtarajiwa ajue kama kusuka au kunyoa. Umenichekesha hapa "....akitaka kujihusisha anakaribishwa". Sijaolewa.
Mtu akitangaza nia na akakuambia ana watoto utakuwa tayari?
 
Asante mkuu. Ni haki yake kwenda kumsalimu *****.
Quickly
Anakubip au kukupigia au atatoa lawama " jaman hata salam'... Hata humkumbuki mwanao? Mpe bas mwanao zawadi, mtt wako anataka aende shule mpatie bas hata pocket mny. Nk.... Ukimwambia ntakutumia atasema hapana, mi mwenyewe ntakuja kuchukua pia nataka nikuone nikuambie kitu... Akija tu km mazingira yanaruhusu lazima akupe mkumbushie enzi
 
Wanachosha hawa viumbe. Yani yeye kajiweka kwenye utakatifu afu makosa yote kambebesha baby momma wake. Sijui hana uchungu na watoto wake pia, naona kaamua kuwa tu kuwa sperm donor, mume mwenzie atalea
Hawa wanawake tuliowazalisha, they will always have a spot in our hearts. Sometimes kuwazuia wanapotuhitaji ni ngumu na sometimes tunatoa ushirikiano ili tusisemwe vibaya kwa watoto wetu.
 
Mtu akitangaza nia na akakuambia ana watoto utakuwa tayari?

Kusema ukweli nikiambiwa hivyo siwezi kukubali haraka, I will need sometime of thinking and re-thinking. Hii ni kwa sababu, unaweza kuolewa na mtu asiye na mtoto akaja kuzaa nje ya ndoa baadae. Na hiyo itakuwa ni kama usaliti, na itakuuma hasa, kwamba mume wangu ameni-cheat mpaka kuzaa nje ya ndoa.

Na unaweza kumpata aliyezaa kabla ya ndoa, ambaye unaingia kwenye ndoa ukiwa na mindset kwamba kuna mtoto yupo somewhere. Na ukaingia ukiwa umejiandaa kukabiliana na changamoto hiyo. Kwa hiyo yatakayotokea hautakuwa shocked.

On the other hand, unaweza kumkataa aliyekwambia ana mtoto, ukamkubali aliyekwambia hana mtoto, kumbe amekuficha. Baada ya ndoa ndo unakuja kugundua kuwa ana mtoto mkubwa tu. Hii itakuuma hakika.

Kwa hiyo hii ni changamoto na ndiyo maana nikaleta huu uzi, ili kupata mtazamo na uzoefu wa watu wengine.
 
Hawa wanawake tuliowazalisha, they will always have a spot in our hearts. Sometimes kuwazuia wanapotuhitaji ni ngumu na sometimes tunatoa ushirikiano ili tusisemwe vibaya kwa watoto wetu.
Aisee!
 
Haha vipi tena! Am trying to be honest here. Ila nikioa they will not be entertained
Hahahahaha usiogope be honest...yaani nawaza gharama ambayo mtu anaibeba kwa kuwa na mwenzi mwenye mtoto nje ya ndoa
 
Hawa wanawake tuliowazalisha, they will always have a spot in our hearts. Sometimes kuwazuia wanapotuhitaji ni ngumu na sometimes tunatoa ushirikiano ili tusisemwe vibaya kwa watoto wetu.
That's very understandable, hao sio your mere exs, ni wazazi wenzenu and no matter what wataendelea kuwa kwenye maisha yenu. Hata akiumwa /akiwa na tatizo lazima inacatch your attention. Huko kwenye kuonana wanapowahitaji na kutoa ushirikiano, have a limit please, kwa sababu hapo ndo kunapozaa changamoto nyingi zinazojadiliwa hapa. Kama mliona mmeshindwana basi kila mtu amove on, sio ndo mnatumia mtoto as excuse ya kupashana viporo na kuongeza watoto wengine. Au mmoja anatumia excuse ya mtoto kutaka kuvuruga ndoa ya mwenzake.

Sio kila anachodemand kitimizwe tu kwa sababu mna mtoto or sijui mtoto wangu atanionaje maana wengine wana demands hata hazihusiani na mtoto. Una mahusiano mengine na unaona demand ya mzazi mwenzio inaweza kuhatarisha mahusiano yako mapya au tu sio demand ya msingi, just don't it. Nafikiri cha msingi ni kuweka tu a clear line, kuwa hapa tunalea tu so tuwekeane tu mazingira mazuri ya kumlea mtoto. Tusiwekeane mitego au vikwazo
 
Kusema ukweli nikiambiwa hivyo siwezi kukubali haraka, I will need sometime of thinking and re-thinking. Hii ni kwa sababu, unaweza kuolewa na mtu asiye na mtoto akaja kuzaa nje ya ndoa baadae. Na hiyo itakuwa ni kama usaliti, na itakuuma hasa, kwamba mume wangu ameni-cheat mpaka kuzaa nje ya ndoa.

Na unaweza kumpata aliyezaa kabla ya ndoa, ambaye unaingia kwenye ndoa ukiwa na mindset kwamba kuna mtoto yupo somewhere. Na ukaingia ukiwa umejiandaa kukabiliana na changamoto hiyo. Kwa hiyo yatakayotokea hautakuwa shocked.

On the other hand, unaweza kumkataa aliyekwambia ana mtoto, ukamkubali aliyekwambia hana mtoto, kumbe amekuficha. Baada ya ndoa ndo unakuja kugundua kuwa ana mtoto mkubwa tu. Hii itakuuma hakika.

Kwa hiyo hii ni changamoto na ndiyo maana nikaleta huu uzi, ili kupata mtazamo na uzoefu wa watu wengine.
Umejibu vizuri sana. Am satisfied. Ningekuwa ndo nakutokea ukanijibu hivi, ningekupa all the time you need to think and rethink kwa sababu you seem to be reasonable
 
Hahahahaha usiogope be honest...yaani nawaza gharama ambayo mtu anaibeba kwa kuwa na mwenzi mwenye mtoto nje ya ndoa
Ni changamoto. Ila hakuna kinachoshindikana. Everybody wants a successfull marriage so they will do anything they can to keep it so. Huna haja ya kuogopa sana
 
Umejibu vizuri sana. Am satisfied. Ningekuwa ndo nakutokea ukanijibu hivi, ningekupa all the time you need to think and rethink kwa sababu you seem to be reasonable
Am humbled! Shukrani sana mkuu!
 
Back
Top Bottom