Kwa elimu yangu ya psychology naomba nijibu hivi...
1. Kuoa na kuolewa ni maamuzi yaliyo mema, haijalishi unamuoa nani au unaolewa na nani!!! Ata ukioa kichaa yote ni sawa.
2. Hapo ndo chanzo cha majanga yote kwa kweli... Mimi nadhani kuondoa migogoro kama mwanaume kazaa nje basi mawasiliano kuhusu mtoto yawe yanapitia kwa mke wa huyo mwanaume... Namaanisha mke/mume awe daraja kati ya wazazi hao wawili... Ashirikishwe 100% katika mawasiliano, kusiwe na usiri wowote.
3. Mtoto yeyote chini ya miaka 10 inapendeza akalelewa na mama yake mzazi. Si vyema akaanza kulelewa na mama wa kambo mapema kama mama yake yupo na ana akili timamu kabisa.
4. Kuhusu kumuona ni vizuri wajadili utaratibu utakavyokua na sio kushtukizana tu... Kama itawezekana mnaweza toka na kukutana kupata chakula cha mchana (mume, mke, mtoto na mama mtoto). Au likizo mtoto akakae na mama yake kwa mda.
5. Apo utaanzisha mtoto kuteswa!!! Hamna mwanamke/mwanaume atakaefurahia matunda ya usaliti kwa kweli... Ni bora umuache hukohuko au umpeleke kwa bibi... Kumleta ndani ni kumuumiza mtoto... Atachukiwa na kila mtu kasoro wewe.
6. Inategemea na maamuzi yenu... Na kama mwenzako kakusamehe kweli.
7. AM BLANK!