Seriously wanaume msioe wanawake waliozaa kabla ya kuolewa. Miaka chache ilopita nilizaa na dada mmoja hivi, nikamhudumia vizuri. Baadae tukapotezana kwa mda kutokana na majukumu ya kazi, pia upande wangu nilitaka apate mda wa kuchumbiwa ili aolewe, hilo likatimia baada ya mwaka akaolewa. Akanitumia ujumbe kuwa ameolewa hivo siku nikirudi nisimtafute. Baadae nikamwuliza vp mtt wangu, akajibu kuwa nisihangaike tena kuhudumia coz mme wake amesema nisirudie kutoa hata senti kwa ajili ya mtt. Nikakubaliana na wazo la mume mwenzagu mpya, na nikakata mawasiliano kwa mda wa miaka miwili hivi, ingawa nilikuwa napenda nimfanyie kitu mwanangu... Mwaka wa 3 mdada akanibip nikampandia hewani akaomba tuonane. Nikafanya namna tuonane nae mahali, akanieleza mambo mengi ktk ndoa yake. Nikamwomba nirudishe huduma kwa mwanangu, na nimnunulie ardhi pamoja na kujenga, akakubali pia... Baadae tukajikuta urafiki wetu ukirudi km awali. Siku moja akaniambia tuzae, nikamgomea sana na akaacha na mi nikadhani ameachana na wazo hilo kumbe alipanga anitege kwa siri, na akafanikiwa mimba ikanasa. Aliponiambia baadae sana nikamkatalia akaniambia km ni huduma mme wake atakuwepo akimaanisha huyo mtt ni ndani ya ndoa hivo mi sintahusika kwa lolote ingawa baba wa kibailojia ni mimi. Nikaazimia nimwache kimya kimya. Niliweza lakini jasho sana, wanaume wanaelewa ilivokuwa ngumu kuachana na mwanamke anaekupenda sana. Lakini nilifanikiwa baada ya misuko suko ya mda mrefu... Seriously usioe mwanamke mwenye mtt, mtu na mzazi mwenzie hawaachanagi huwa wana pozi kwanza ndoa ipite afu wanarudiana baadae