Mwenzangu unamalizaje mwaka?

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,621
2,000
Juzi nilipokuwa napitia malengo niliyojiwekea mwaka huu nikagundua kuna vitu viwili nilitarajia kuvifanya mwaka huu. Nilitarajia kuwa na shamba la migomba, mpaka jioni ya juzi nilikuwa sijaweza.Nilitarajia kuwa na shamba la nyuki la kisasa, nimekosa location nzuri.

Ili kuondoa nuksi, leo nimewaomba vijana wangu waoteshe migomba minne mchana wa leo, na nimenunua mizinga mitano ya kisasa ili iwe chachu ya kutimiza ndoto zangu mwakani, kwa hiyo tayari nimeanza mwendo wa kutimiza ndoto zangu.

Zaidi sana namshukuru Mungu alivyonilinda na kunijalia afya kwa mwaka huu, niwashukuru wanajamvi wenzangu kwa kushirikiana vema. Tumshukuru Mungu kwa yote, tuwe tumefanikiwa au hatukufanikiwa, maadamu hatukulala, yote ni heri.
 
Mama Joe

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,504
1,225
Ili kuondoa nuksi.............
nimecheka peke yangu bado kuna dhana ya kuondoa nuksi? Ila ni kweli kuwa mjasiriamali inataka nidhamu. Kwakweli ninajifunza vitu hapa, lakini kikubwa tunamshukuru Mungu sana kwa upendo wenu na umoja kwani kupitia hapa tumeweza kujifunza, kujaribu kuwekeza na kupiga hatua zaidi ktk malengo yetu. Nawatakia wote baraka na heri ya mwaka mpya.
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,621
2,000
nimecheka peke yangu bado kuna dhana ya kuondoa nuksi? Ila ni kweli kuwa mjasiriamali inataka nidhamu. Kwakweli ninajifunza vitu hapa, lakini kikubwa tunamshukuru Mungu sana kwa upendo wenu na umoja kwani kupitia hapa tumeweza kujifunza, kujaribu kuwekeza na kupiga hatua zaidi ktk malengo yetu. Nawatakia wote baraka na heri ya mwaka mpya.

Dada hujambo,
Kiswahili tu hicho dada. Nilichofanya, ni kuhakikisha nazianza hizi projects hata kwa kiwango hicho kidogo, bila hivyo nitakuwa naahirisha kila siku.
 
goodmother

Senior Member
Jul 21, 2012
108
0
Yote tumshukuru, Mungu kwa uhai, na afya. Namaliza mwaka nikiwa na mawazo tele kichwani mwangu mengini pengine yanachangiwa na uoga. Lakini naamini Mungu ataniPa ujasiri ili niweze kusonga mbele. MUngu azidi kuwalinda ndugu Zangu wanaJF. Herini ya mwaka mpya 2014
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,621
2,000
Yote tumshukuru, Mungu kwa uhai, na afya. Namaliza mwaka nikiwa na mawazo tele kichwani mwangu mengini pengine yanachangiwa na uoga. Lakini naamini Mungu ataniPa ujasiri ili niweze kusonga mbele. MUngu azidi kuwalinda ndugu Zangu wanaJF. Herini ya mwaka mpya 2014

Naam vyote vyatoka kwake. Hata ujasiri wa kuthubutu huombwa kwake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom