Baada ya kufikia ‘Unc’ status, nimejikuta tu napunguza mahudhurio ya hili jukwaa.
Hivyo msishangae sana kuniona humu leo. Mara moja moja si mbaya kujivinjari na kuwasabahi.
Twende kwenye mada….
Ni hivi, mimi nadhani ni mtu mmoja mvumilivu sana, hususan ikija kwenye mapungufu ya kiubinadamu.
Ila hata wavumilivu nao huwa wana kikomo chao.
Hivyo, nauliza……je, umeshawahi kuwa au unaye mwenza ambaye ni kilaza?
Yaani huyo mwenza wako unaona umemzidi akili lakini basi tu huna jinsi ya kumwambia.
Sasa, sidhani kama kuna kipimo sahihi cha ukilaza. Kama kipo basi mimi sikijui.
Kwa hiyo mtu unaposema flani ni kilaza unakuwa unatumia kipimo kupitia mtazamo wako.
Hiyo ni hatua ambayo inaweza kutoa matokeo yasiyo sahihi.
Mimi kuna mdada mmoja hivi ilibidi tu nimpotezee na kumfungia kioo mazima.
Si tu alikuwa ni kilaza, bali pia alikuwa naive [sikijui Kiswahili chake] sana.
Sikumbuki kabisa yeye kuwa na mtazamo wowote ule ambao ulikuwa ni sahihi, kwa jambo lolote lile.
Ilikuwa inamchukua muda mrefu sana kuja kuwa na mtazamo sahihi kuhusu jambo lolote lile.
Yaani hata umwelewesheje, alikuwa ni mzito sana kuelewa lakini baada ya muda mrefu ndo anakuja kuelewa.
Ukilaza wa namna hiyo ni mzigo sana na unakera.
Mpaka leo hii sijajutia kumtosa na wala hata simkumbuki kabisa.
Nyie mnaonaje, nilikosea kumtosa?
Na nyie mshawahi kuwa na wenza vilaza?
Binafsi naona hata ukiacha kabisa kutumi JF inaweza kua vizuri zaidi, licha ya kua ulijiunga kwa hiyari yako mwenyewe na nafikiri kujiondoa wewe mwenye bila mayowe inaweza kua jambo la busara zaidi, ili hatimae wadau wapya wa JF wasikutane na watu wa aina yako, wakujipiga kifua, na kujipa uerevu, utakatifu na ukamilifu kuliko binadamu wengine mpaka kwenye mahusiano yako.
In fact,
kwenye mahusiano imara na yenye furaha, kila moja anapaswa kukubali kubeba mapungufu na madhaifu ya kibinadamu ya mwenza wake na kuyasitiri kadiri iwezekanavyo.
Kujipa ukamilifu, utakatifu na uerevu zaidi ya mwenza wako ni kukaribisha mafarakano na pengine maafaa kwenye mahusiano au ndoa. Na sense of perfections kwenye mahusiano ni kitu nonsense sana aise.
Biblia imeandika Ishi nao kwa akili.
Ni wazi wewe umekosa maarifa ya kuishi katika mahususino yako na umeshindwa kutumia akili vizuri katika kuishi na mwenzi wako na badala yake unakuja kujiexpose jukwaani tena kwa uthibitisho kabisa kwamba wewe ndio changamoto na kilaza zaidi kwenye mahusiano yako, kwasababu umeshindwa kutumia akili kuishi na mwenzi wako. Umejipa utakatifu na ukamilifu useless kabisa kwenye mahususi na kuyatumbukiza kaburini kindezi sana aise.
Hata hivyo,
humu jukwaani ni mashuhuda kwamba,
wakati mwingine, wewe ni mtukanaji hodari na mporomosha matusi mkuu dhidi ya wenye maoni na mtazamo tofauti na wako. Kwa hali hiyo, ni wazi, hutaweza kuishi na mtu mwenye jinsia tofauti na yako. Maana yake hata ukianzisha mahusiano mengine, hawatadumu yatavunjika kwasababu ni wazi wewe ni addicts wa sense of perfections, kitu ambacho ni sumu kwenye mahusiano yoyote yale.
Labda ufanyiwe mpango na walioficha familia zao ng'ambo ili hatimae ukaanzishe familia kama zao huko ng'ambo 🐒