Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,246
- 144,298
Baada ya kufikia ‘Unc’ status, nimejikuta tu napunguza mahudhurio ya hili jukwaa.
Hivyo msishangae sana kuniona humu leo. Mara moja moja si mbaya kujivinjari na kuwasabahi.
Twende kwenye mada….
Ni hivi, mimi nadhani ni mtu mmoja mvumilivu sana, hususan ikija kwenye mapungufu ya kiubinadamu.
Ila hata wavumilivu nao huwa wana kikomo chao.
Hivyo, nauliza……je, umeshawahi kuwa au unaye mwenza ambaye ni kilaza?
Yaani huyo mwenza wako unaona umemzidi akili lakini basi tu huna jinsi ya kumwambia.
Sasa, sidhani kama kuna kipimo sahihi cha ukilaza. Kama kipo basi mimi sikijui.
Kwa hiyo mtu unaposema flani ni kilaza unakuwa unatumia kipimo kupitia mtazamo wako.
Hiyo ni hatua ambayo inaweza kutoa matokeo yasiyo sahihi.
Mimi kuna mdada mmoja hivi ilibidi tu nimpotezee na kumfungia kioo mazima.
Si tu alikuwa ni kilaza, bali pia alikuwa naive [sikijui Kiswahili chake] sana.
Sikumbuki kabisa yeye kuwa na mtazamo wowote ule ambao ulikuwa ni sahihi, kwa jambo lolote lile.
Ilikuwa inamchukua muda mrefu sana kuja kuwa na mtazamo sahihi kuhusu jambo lolote lile.
Yaani hata umwelewesheje, alikuwa ni mzito sana kuelewa lakini baada ya muda mrefu ndo anakuja kuelewa.
Ukilaza wa namna hiyo ni mzigo sana na unakera.
Mpaka leo hii sijajutia kumtosa na wala hata simkumbuki kabisa.
Nyie mnaonaje, nilikosea kumtosa?
Na nyie mshawahi kuwa na wenza vilaza?