Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,603
Bukoba Vijijini | CCM Kura za Maoni Falis Athumani Buruhan amegoma kusaini matokeo ya kura za maoni baada ya kutoridhika na matokeo hayo yaliompa ushindi Dk. Jasson Samson Rweikiza, aliyeibuka mshindi baada ya kupata kura 6,485 kati ya kura halali 11,582 Falis Athumani Buruhan, alipata kura 4,619, huku wagombea wengine wakifuata nyuma kama ifuatavyo: 3. Fahami Mastawily Juma – 239 4. Asted William Mpita– 124 5. Edimund Emmanuel Rutaraka – 89 6. Philibert Francis Bagenda – 44
Buruhan aligonga vichwa vya habari zaidi Aprili 2024 baada ya kuibua mjadala alipotoa kauli hadharani akilitaka Jeshi la Polisi kutojihusisha na utafutaji wa watu wanaomkosoa Rais Samia na viongozi wengine mitandaoni endapo watapotea.