Mwenyekiti Wa Ukombozi Na Ufahari!

Hivi huyu mwanzisha mada ndiye yule yule aliyewahi kuanzisha thread ya Watu kumpinga JK Washngton DC?
 
ki.
Margaret__BourkeWhite__Portrait_of_Mahatma_Ghandi.jpg


Mwenyekiti wa Chama cha kuwakomboa wananchi, anapotumia magari kama ya watawala, inasema nini kuhusu huu ukombozi? VX8, tena sio moja, Wasaidizi, Dreva, MABENDERA, KUCHELEWA KUFIKA UWANJANI, bado hajashika nchi, je akishika tutegemee nini tofauti, maana haya si ndio ya kawaida kwa watawala? Kwenye kuvaa kombati sawa lakini mengine hayo mbona sawa na watawala?

- NAOMBA KUTOA HOJA, MAANA WAKOMBOZI KINA CASTRO, CHE GUEVARA, MAO, NA SAVIMBI HATUKUWAONA NA MA-VX8, AU WASAIDIZI AU NI UKOMBOZI TOFAUTI?

- KUONGOZA SI NI MFANO ZAIDI? MUNGU AIBARIKI TANZANIA!


William.
...was savimbi mkombozi too? kamanda, toka, toka uende ukafanye rejea ya historia, kisha rudi tena...
 
Willy umeulizwa swali zuri kwa kweli na umepoint kitu cha muhimu sana, labda tu umekosea kulinganisha CDM na Savimbi, CDM wanatakiwa kulifanyia kazi swala hili. CDM waanze kujitofautisha na CCM kwa kutuonyesha kwa mifano jinsi watakavyoweza kubana matumizi ya serikali pindi tukiwakabidhi hii nchi. Tofauti na hapo mwenyekiti anafanya kazi nzuri. Viva mwenyekiti!
.....marehemu, captain thomas sankara wa bukina faso anaweza kutoa somo zuri, namna kiongozi wa umma,anaeongoza umma, anavyoishi....
 
ki.
Margaret__BourkeWhite__Portrait_of_Mahatma_Ghandi.jpg


Mwenyekiti wa Chama cha kuwakomboa wananchi, anapotumia magari kama ya watawala, inasema nini kuhusu huu ukombozi? VX8, tena sio moja, Wasaidizi, Dreva, MABENDERA, KUCHELEWA KUFIKA UWANJANI, bado hajashika nchi, je akishika tutegemee nini tofauti, maana haya si ndio ya kawaida kwa watawala? Kwenye kuvaa kombati sawa lakini mengine hayo mbona sawa na watawala?

- NAOMBA KUTOA HOJA, MAANA WAKOMBOZI KINA CASTRO, CHE GUEVARA, MAO, NA SAVIMBI HATUKUWAONA NA MA-VX8, AU WASAIDIZI AU NI UKOMBOZI TOFAUTI?

- KUONGOZA SI NI MFANO ZAIDI? MUNGU AIBARIKI TANZANIA!


William.
Analogy zako zimekosa kabisa maana kama "GDNP per capiter". Hii ni cheap shot against Mbowe tu.
Kumlinganisha Mbowe na Gandhi, halafu baadaye unakimbilia kwa Savimbi wapi kwa wapi mkuu. Wee bozo kweli.
 
ki.

Mwenyekiti wa Chama cha kuwakomboa wananchi, anapotumia magari kama ya watawala, inasema nini kuhusu huu ukombozi? VX8, tena sio moja, Wasaidizi, Dreva, MABENDERA, KUCHELEWA KUFIKA UWANJANI, bado hajashika nchi, je akishika tutegemee nini tofauti, maana haya si ndio ya kawaida kwa watawala? Kwenye kuvaa kombati sawa lakini mengine hayo mbona sawa na watawala?

- NAOMBA KUTOA HOJA, MAANA WAKOMBOZI KINA CASTRO, CHE GUEVARA, MAO, NA SAVIMBI HATUKUWAONA NA MA-VX8, AU WASAIDIZI AU NI UKOMBOZI TOFAUTI?

- KUONGOZA SI NI MFANO ZAIDI? MUNGU AIBARIKI TANZANIA!


William.

William,
Umegusia kitu muhimu sana hapa. Mara kwa mara sikubaliani na wewe kwa hoja zako za kupigia debe CCM, lakini hapa nafikiri umejitahidi kuleta hoja ya kitaifa.

Binafsi sidhani kama CDM watamchagua Mbowe kuwa mgombea wao maana kwangu sioni kama ana sifa za kuwa raisi, lakini hapa inaonyesha wazi kabisa utawala wake ungekuwaje? Ni vema kwa CDM kuliangalia hili na mengine mengi ambayo yameiharibu CCM.

Kwa Wana JF, ni vema tukaacha kupiga tu makofi kwa CDM, Upinzani au kumtukana yeyote anayeikosoa CDM. Tukosoe yeyote yule tunayeona haitendei haki nchi yetu. Vyama vya siasa tunaweza kubadilisha vikienda mrama lakini nchi yetu ikiharibiwa hatuna pa kwenda. Wake up you Tanzanians.
 
Mkuu,nilishakushauri huko nyuma lakini nadhani umeamua kupuuza ushauri wangu.Ulipata wazo la kuwania kuwawakilisha Watanzaniakupitia ubunge wa EAC.Aidha kwa bahati mbaya au kwa maandalizi duni,ukashindwa.Lakini pamoja na kushindwa,umefanikiwa kutangaza jina lako,na laiti kama una malengo ya siasa huko mbeleni,hapo ulipoishia pangewezakukusaidia sana.

So far,nakuona kama mtu uliyechangayikiwa.Baadhi ya mambo unayoandika hayakusaidii hata chembe.Huun ulikuwa wakati mzuri wa kuongea na kufanya mambo ya busara ili Watanzania watambue kuwa angalau nawe ni miongoni mwa hazina za taifa (kikubwa ni matendo si maneno matupu-especially maneno yenyewe yakiwa hayana mantiki na yametawaliwa na chuki ya KWANINI HUYU NA SI MIE).

Umefanya wazo la maana kuanzisha blogu.Awali nilitarajia mambo kadhaa ya msingi bloguni hapo lakini so far imegeuka uwanja wa kuwatangaza mabinti na udaku.Sir,that's way too low kwa mtu wa calibre yako.Kama signature ya Invisible inavyosema ficha ujinga wako onyesha busara zako.Publicity ni kitu kizuri lakini ikiwa misused inaweza kukuodnoa kabisa hata pale kidogo ulipofikia.

Watanzania wanachohitaji ni ukombozi.Ukiletwa na mtembea kwa miguu,sawa.Ukiletwa kwa mtumia bajaji,sawa.Ukiletwa kwa mtumia kibito,sawa.Na kama mwendesha Vogue atatuletea ukombozi,tatizo lipo wapi?Mbona hukulalamika Nape alipoenda Bukoba kwa ndege?

Japo natambua utapuuza tena-na pengine kukasirika-bado narejea kukushauri ujitahidi kupata muda wa kutosha kupumzisha akili.Siasa za Bongo ni tofauti sana ukiziangalia kutoka nje na kuzilinganisha na hali halisi 'mtaani.' Taratibu zama za kujali "huyu mtoto wafulani"zinaanza kuyoyoma (na mfano wa karibuni sio wewe tu bali hata yalomkuta Sioi huko Arumeru Mashariki).

I hope you'll put common sense in front of emotions

- Unajua kuna wakati huwa ninafikiri nilikuonea kuku-delete kule FB, lakini kila ukiandika pumba zako hapa ninapata faraja sana kwamba sikukosea, kwamba huwa unedna kwenye blogu yangu ni maajbu sana kwa mtu ambaye kila wakati unadai sina uwezo mkuwa wa kufikiri! ha! ha! ha! ha!

- Akili yan gu ipo sawa sawa ndio maana niliamua kuondokana na utumwa wa hirai huko Ughaibuni na kuja nyumbani kujumuika na wananchi wenzangu kujenga taifa letu, badala ya kukaa huko na kulia lia kila siku, aliyechanganyikiwa ni yule anyedai mwingine amechanganyikiwa na bado anaenda kwenye blogu ya aliyechanganyikiwa na yeye ni mzima! ha! ha! ha! yale yale ya mwizi kuamini wengine wote ni wezi kama yeye! ha! ha! ha!

- The New Super blogu, nitakwambia siri behind the scene wanao ongoza kwa kuingia kule ni watu kutoka hapa JF, wakifuatiwa na Facebook, sasa tuna average 4100 peoples a day bado hatujaisha ni siku 10 mtupo hewani, so tupo vizuri na wananchi wanatupa feedback ahhhhhhh they love it, tunachanganya kila kitu, siasa, udaku, warembo, mamen, you name it utapata kule, Otheriwse pole sana naona leo nimewashika pazuri sana mkono kwenye kunde na kwenye nyama, ukombozi mnataka na VX8 mnataka, ha! ha! haviendi pamoja!

- Ngoja nikupe darasa kuhusu commonsense, ukiona mtu amevua nguo huvui nguo na kumkimbiza kama unavyofanya hapa unaachana naye, wengi hapa mmelia sana kwamba sina uwezo wa kufikiri! ha! ha! ha! page karibu 10 sasa kwa ajili ya thread iliyoanzishwa na mtu asiye na uwezo mkubwa wa kufikiri? ha! ha! ha! ha! ha!

- Hivi unajua baada ya Jangwani ilifanyika sherehe kubwa sana nyumbani kwa Mwenyekiti? Ulialikwa? Alilipia nani ile sherehe kubwa vile? Sherehe ya nini hasa kufurahia kuja kujionyesha na ma-VX8? Wewe amuka wewe!


William.
 
Hivi kweli Savimbi aliyewakata watu mikono na kuwaua, leo hii watu wanamwona role model? Kweli, tembea ujionee.
 
Hivi kweli Savimbi aliyewakata watu mikono na kuwaua, leo hii watu wanamwona role model? Kweli, tembea ujionee.

- Tunajali mazuri yake, aliweza kuishi kama mkombozi wa wananchi, sio kama mwenyekiti wenu na ma-vx8, Idd Amin hakuwa model lakini alinunua jengo la Uganda House New York mpaka leo ni fahari ya Uganda!!


William.
 
willy
nashindwa kukuelewa Kabisa, nahisi una issue binafsi na mwenyekiti wa CDM . Hivi ukiwa kiongozi unatakiwa uishi maisha gani? Jasho la Kweli linalipa na kazi hulipa sasa Kama Mbowe Kafanya sherehe Kubwa nyumbani kwake Hilo ni swala binafsi, Kama kachinja mbuzi Mia hilo ni maisha yake binafsi, Kama kaalika marafiki Zake wote Sioni kwa nini uwe na hasira kiasi hicho. Nahisi kuna jambo linakusumbua au una hasira na mafanikio binafsi ya Mbowe. JF ibaki JF bifu zitafutiwe sehemu nyingine.

Siamini kama Willy umefikia kiwango hicho cha kushindwa kuonanisha matumizi mabovu ya fedha za umma na maisha ya mtu binafsi. Hakuna mzazi anataka watoto wake waishi kimasikini awe wawe na mafanikio ya kimasikini. Kama una hoja ilete na uache majungu. Kama unaamini Mwenyekiti wa CDM hawezi kufanya sherehe nyumbani kwake kwa fedha zake tuambie.

Kama unaamini mwenyekiti wa CDM hana uwezo binafsi wa fedha tuambie, zaidi ya hapo ni majungu, wivu, fitina, na ukosefu wa kuanisha matatizo ya mtanzania na ufisadi unaofanywa na watawala wetu wanaokusanya kodi zetu. Vyuo vikuu tunavyojenga na shule tunazopeleka watoto wetu na uchumi tunaotaka kujenga sio wa kumfanya mtanzania mnyonge na omba omba au wa kushangaa watu wakila vizuri au wakiishi maisha bora , tunataka wawe washiriki wa maisha bora na miundu mbinu ya kisasa.
 
willy
nashindwa kukuelewa Kabila, nahisi una una issue binafsi na mwenyekiti wa CDM . Hivi ukiwa kiongozi unatakiwa uishi maisha gaini? Jasho la Kelli linalipa na kazi helipa sasanqua Kama Mbowe Katanga sherehe Kubwa nyumbani kwake Hilo in swala binafsi, Kama kachina mbuzi Mia halo in maisha yaks binafsi, Kama kaalika marafiki Zane wrote Sioni kwa nini use na hasira kiasi hicho. Nahisi kuna jambo linakusumbua au una hasira na mafanikio binafsi ya Mbowe. JF ibaki JF bifu zits futiwe sehemu nyingine.

- Mbowe is my good friend, ila kwenye taifa hatuna urafiki nazungumzia nasa na ufahari kwa wakombozi huwa ni mwiko, wewe unazungumzima nini sijakuelewa?

William
 
Wiliam baharia, hakika shabiki, mpenzi, mwanachama wa ccm, ambaye ni kijana kama wewe yahitaji awe na akili kama ya maiti! Umerogwa na kuambukizwa uccm na Babako{JUMANNE} jina la kusaka madaraka alopewa na waarabu kwa ufadhili wa pesa. Kuna mambo yakupasayo kuyafanya hufanyi, bali kila siku ni kujua chadema leo wanafanya nini, wamekula nini, au wamejamba ushuzi gani n.k. Una bichwa kubwa na umbille kubwa lililokosa square, ubongo wa shomolo. Unasipidi kubwa ya kuzeeka kuliko umri wako. Gharaghabhaho!
 
401706_390840007625030_100000971026600_1045118_779788496_n.jpg


Ndugu William Malecela, Mheshimiwa Mbowe alisharudisha Shangingi serikalini ambalo alikabidhiwa kama kiongozi wa kambi ya upinzani.

Gari unayoiona ni ya kununua kutoka pesa zake za mfukoni, hakuna pesa ya mlipa kodi iliyotumika, na hakuna pesa ya mlipa kodi inayotumika kwa ajili ya mafuta na matengenezo.

Mbowe ni kama Sabodo anayetumia utajiri wake kwa manufaa ya watanzania, tofauti na viongozi toka CCM wanaopora rasilimali za taifa, viwanja vya mipira vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi, majengo kadhaa yaliyokuwa mali ya umma kama umoja wa vijana, na kuiingiza serikali kwenye gharama kubwa kununua magari ghali kwa ajili ya kutembelea.

Hakuna siyejua kwamba Mbowe ni mfanyabiashara, na ana uwezo wa kuwa na gari kama hiyo. Hata magari yanayotumika kwenye kampeni alinunua kwa pesa zake kisha kuweka utaratibu wa kurudishiwa taratibu, na magari hayo yanasaidia sana katika mikutano hakuna kuhangaika kutengeneza majukwaa ya muda kwani majukwaa wanayo wanatembea nayo po pote waendapo.

Misafara ya viongozi wa Chadema hutumia mashangingi ambayo ni ya wabunge waliyopata kwa mkopo na wanayalipia yakiwa ni magari yao. Hapo umenipata?

Jaribu kujenga hoja kwa misingi yenye kuakisi ukweli, kwani kwa hili tukuambie dhahiri umechepuka na kugusa pasipo kweli, labda ungesema ni magari ya Chama, lakini Mbowe hutumia gari yake binafsi.
 
ki.
Margaret__BourkeWhite__Portrait_of_Mahatma_Ghandi.jpg


Mwenyekiti wa Chama cha kuwakomboa wananchi, anapotumia magari kama ya watawala, inasema nini kuhusu huu ukombozi? VX8, tena sio moja, Wasaidizi, Dreva, MABENDERA, KUCHELEWA KUFIKA UWANJANI, bado hajashika nchi, je akishika tutegemee nini tofauti, maana haya si ndio ya kawaida kwa watawala? Kwenye kuvaa kombati sawa lakini mengine hayo mbona sawa na watawala?

- NAOMBA KUTOA HOJA, MAANA WAKOMBOZI KINA CASTRO, CHE GUEVARA, MAO, NA SAVIMBI HATUKUWAONA NA MA-VX8, AU WASAIDIZI AU NI UKOMBOZI TOFAUTI?

- KUONGOZA SI NI MFANO ZAIDI? MUNGU AIBARIKI TANZANIA!


William.

Hata Hayati Nyerere aliyaona hayo mapema sana na ndio maana alipigana mpaka mwisho na akahakikisha bwana Jumanne S. Malecela haingii ikulu.

Endapo J4 angeruhusiwa kuingia ikulu basi ni wazi kuwa Taifa na rasilimali zake zoote kwa sasa zingekuwa chini ya mwarabu.
 
Mkuu haiondoi hoja yake, wala haijajibu hoja yake

kwa swalli hili utakuta wananchi wote wanyonge wanaodanganywa na kupumbazwa watamuunga mkono Willy! na wote utawapima akili!!

Matola changanya akili zako....Hoja ya willy ni ngumu na mbaya sana kwa washabiki wa mageuzi

dalili za mvua ni mawingu, unafikiri Mbowe akiwa rais au waziri mkuu ndio atapiga marufuku matumizi ya magari ya kifahari


Matola mchana wa saa sita tunaona jua! na kamwe hatusemi ule mwezi.....hoja ya willy in other words in ku-alert hata wewe kuwa CDM ina dalili zote za kirusi CCM!!! ikishika madaraka itafanya yale yale ya CCM sasa , na haitakuwa ukombozi bali substitution!!!!

Wabs,

Naomba nitofautiane na wewe mkuu,

Sijasoma vitabu ya Gadhi ila nimeangalia simema, kuna vitu vinaitwa priviledge, kila mmoja ana vyake kutokana na chaguo, wakati, mazingira na morals.... wakati ule penetration ya Gandhi ilikua "kuwa mmoja wao" katika namna ambayo india ilikua na ipo hadi leo, cultural.... tunachoona kwenye dress code ni ndivyo ilivyo hadi leo maeneo core kama Kerala (india)

Nyerere, alivaa kombat, au ngwabi au chon lai, alipanda magari ya kifahari sana kuliko wote wakati ule na hata ukiangalia documentaries za akina Che, Fidel, Lincoln na wengine, bado kuna choices za priviledges ambazo hata akina mfalme daudi, Selemani na hata wanazuoni wa kiislam walikua nazo (hapa namuondoa Osama)

Tukija hata kwenye kalcha yetu......... mswaihi marekani anaeza kununua "rim kabla hata ya gari, bongo pia ananunua gari kabla hata hajajua atalala wapi........ ni tamaduni, na tamaduni hizi zina-associate na power, na power ndio sumaku ya followers, kwahiyo hatuwezi kulinganisha yasiyolinganishika kutokana na themes na context ya mambo na wakati

Leo hii Yesu angekuwepo, si ajabu angeenda saluni kupunguza sharubu, angeenda kwa Maumba kushona Tuxedo na angekua na IPAD

Lets open our eyes na kuangalia what drove our historic leaders to power, respect and infulence

Ukimuangalia dalai Lama unajifunza mengi sana kuhusu priorities na priviledges to influence powers
 
Hata Hayati Nyerere aliyaona hayo mapema sana na ndio maana alipigana mpaka mwisho na akahakikisha bwana Jumanne S. Malecela haingii ikulu.

Endapo J4 angeruhusiwa kuingia ikulu basi ni wazi kuwa Taifa na rasilimali zake zoote kwa sasa zingekuwa chini ya mwarabu.

NI kweli GC

ila pamoja na hayo, JK alitumia Rolls Royce, BEnzi, Ngege nk za serikali, kirungu, suti nk vyake etc

Ila lazima tukubali pia kwamba William ni total reflection ya Jumanne............ ni wazee wa kukurupuka na kukosa vision
 
..kiungo kati ya mwanasiasa na wananchi/wapiga kura wake ni IMANI/TRUST, pamoja na ujumbe wa matumaini kwa wale anaowaongoza/anaotaka kuwaongoza.

..ukiona Mbowe anatembelea magari hayo na wanachama wake hawalalamiki ujue ni kwasababu wamemuamini kwamba anafanya na kusimamia yale waliyomtuma.

..CCM wanalalamikiwa na wananchi kuhusu matumizi ya magari ya kifahari kwasababu wananchi hawaridhiki na utendaji kazi wa CCM. hata sasa hivi CCM wakiamua kutumia bajaji bado wananchi wanaweza wasiridhike kutokana na rekodi ya miaka 30+ ya utawala mbovu.

..Mwalimu Nyerere alikuwa anaishi msasani kwenye beach house na wakati mwingine akiendeshwa kwenye benzi ya milango mitatu, Sokoine amefariki akiwa amepakiwa kwenye benzi high class ya wakati huo. wananchi hawakulalamikia matumizi ya Mwalimu na Sokoine kwasababu waliwaamini.

..pia siyo lazima kiongozi awe masikini ili aweze "ku-connect" na wananchi/wapiga kura masikini. JF Kennedy alizaliwa kwenye familia ya kitajiri lakini aliweza kukubaliwa na wapiga kura ambao wengi wao alikuwa amewazidi kiukwasi. Wananchi walimpa kura Kennedy kutokana na ujumbe wake wa matumaini kwa wananchi wote wa Marekani.

..labda unajiuliza kwanini CCM wanaumiwa wanapotanua na ma-VX wakati CDM r given a free pass. Jibu ni kwamba CCM wanachongewa na kuwepo kwao madarakani kwa muda mrefu bila kuwa na chochote cha maana cha kuonyesha, pamoja na masuala ya rushwa na ufisadi vilivyotamalaki ndani ya chama hicho.
 
...was
savimbi mkombozi
too? kamanda, toka, toka uende ukafanye rejea ya historia, kisha rudi
tena...

savimbi ni gaidi aliyeingia msituni baada ya kushindwa uchaguzi. CDM
wako kwenye jumuia wakihamasisha wanaouona ni ukombozi toka kwa wafujaji
wa mali za umma na mafisadi!
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Mkuu W J M kauliza swali zuri sana bahati mbaya hapewi majibu ana ambulia kejeli na viroja.Wanajamvi wenzangu tuitendee haki JF kama huna uwezo wa kujibu hoja kaa pembeni magauzi ya kweli yatafanikiwa ikiwa tutakubali kukosolewa na kujisahihisha.

CDM leo ni chama cha upinzani kesho kinaweza kuwa chama tawala mambo yanayotendwa na viongozi wake leo yanatoa mwanga wakipewa dola watatutendea nini !.

Tunapinga kwa nguvu zetu zetu serekali ya CCM iachane na matumizi ya magari ya kifahari bahati mbaya mbadala wa CCM naye anatumia magari ya kifahari ?.

hawezi kupewa majibu ya maana wakati yeye mwenyewe na baba yake wanaishi maisha hayo hayo...mzee wake anaumwa badala ya kutibiwa hapa anakwenda USA? William kama sio kuwa mkubwa humu jamvini nakuhakikishia kwa jinsi ulivonichefua ungeoga matusi leo na BAN nipewe tu..lakini ndo hivo kwa kuwa wewe mkubwa humu basi unakuwa kama Rooney yaani usiguswe unanyoosha mikono kwa refa....haya bana ...mungu yupo lakini
 
Back
Top Bottom