Mwenye orodha watu waliohukumiwa na Mahakama ya Mafisadi ya Awamu ya 5 aniwekee hapa. Naona kama ilikuwa kamba

Nimejaribu kutafuta watu walioitwa mafisadi, wezi na wapiga Dili walioitwa mbaroni na kuhukumiwa na ile waliita Mahakama ya mafisadi sijaona hata mmja.

Mataga na waimba Pambio wa Mwendazake naomba mnitakie mafisadi mliowatia mbaroni awamu yenu kwa sababu naona kama tulipogwa na kudanganywa kama Watoto wadogo.

Naongea haya kwa sababu aoka awamu ya 6 imeingia madarakani mafisadi ambao imewahukimu walikuwa ni wale waliiba pesa awamu ya 5 ila waliachwa na Jiwe na wapambe wake.

Mifano ya hai ni aliyekuwa DED WA Arusha Dr Pima, Sabaya mdogo Watumishi mbalimbali na sasa Kigogo wa Udart.

===

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka 15 yakiwamo kuisababishia UDART hasara ya Sh. milioni 750, kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji fedha haramu, kuwasilisha nyaraka za uongo na kughushi.

Katika shtaka la kuongoza genge la uhalifu, washtakiwa wanadaiwa katika nyakati tofauti kati ya Mei 25 na Julai 10, 2016 katika maeneo tofauti Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu na kujipatia Sh. milioni 750 kutoka akaunti ya UDART, Benki ya NMB Tawi la Bank House.

Washtakiwa hao pia walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kughushi, mawili ya kuwasilisha nyaraka za uongo na mashtaka tisa ya utakatishaji fedha haramu.

Nipashe

====

My Take
Hongera sana Rais Samia Kwa kuwashughulikia mafisadi waliolelewa na awamu ya 5 Kwa vitendo.
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Alikuwa anashika mkasi wa mafile muulize
Usihamishe magoli nitajie orodha ya mafisadi maana mlikuwa mnasomba pesa huku mnamsifia Jiwe
Screenshot_20221119-094007.png
Screenshot_20221119-093841.png
 
Nimejaribu kutafuta watu walioitwa mafisadi, wezi na wapiga Dili walioitwa mbaroni na kuhukumiwa na ile waliita Mahakama ya mafisadi sijaona hata mmja.

Mataga na waimba Pambio wa Mwendazake naomba mnitakie mafisadi mliowatia mbaroni awamu yenu kwa sababu naona kama tulipogwa na kudanganywa kama Watoto wadogo.

Naongea haya kwa sababu aoka awamu ya 6 imeingia madarakani mafisadi ambao imewahukimu walikuwa ni wale waliiba pesa awamu ya 5 ila waliachwa na Jiwe na wapambe wake.

Mifano ya hai ni aliyekuwa DED WA Arusha Dr Pima, Sabaya mdogo Watumishi mbalimbali na sasa Kigogo wa Udart.

===

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka 15 yakiwamo kuisababishia UDART hasara ya Sh. milioni 750, kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji fedha haramu, kuwasilisha nyaraka za uongo na kughushi.

Katika shtaka la kuongoza genge la uhalifu, washtakiwa wanadaiwa katika nyakati tofauti kati ya Mei 25 na Julai 10, 2016 katika maeneo tofauti Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu na kujipatia Sh. milioni 750 kutoka akaunti ya UDART, Benki ya NMB Tawi la Bank House.

Washtakiwa hao pia walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kughushi, mawili ya kuwasilisha nyaraka za uongo na mashtaka tisa ya utakatishaji fedha haramu.

Nipashe

====

My Take
Hongera sana Rais Samia Kwa kuwashughulikia mafisadi waliolelewa na awamu ya 5 Kwa vitendo.
Lakini bado kamba zitaendelea tu isipokuwa kwa wale vidagaa ambavyo havina influence ya kutosha !!
Hii ilikuwepo kabla ya awamu ya Jiwe na itaendelea kuwepo kwa muda mrefu ujao !
Muarobaini utapatikana ikipatikana Katiba mpya bora !! Ambayo nayo upatikanaji wake mpaka sasa bado ni Songombingo !!
 
Bora hata mama tumesikia vigogo wakipanda kizimbani.Kwa Jiwe ukimsikia nani amehukumiwa?
 
Unajua Nashangaa Hawa Wahuni Wanapata Wapi Ujasiri Wakumsagia Kunguni Mzilankende Ili Anuke
Yule Baba Alitufaa Sana Tanzania Na Alifanya Kazi Chap Chap
Mkuu alikufaa wewe! Yule alikuwa Mbakaji, mporaji wa wake za watu, fisadi, muuaji na kichaa! Hana cha kusagiwa zaidi ya tabia yake mwenyewe!!!
 
kikwete
Nape
Ridhiwani
Rugemarilla
kinana mwizi wa meno ya tembo
Harbinger Seth
Yusufu Manji
yote haya majizi yanazima umeme yauze majenereta yalihukumiwa na mahakama ya wananchi na yalifulia Sana ngoja tena yaje tuyaadhibu 2025 yarudi utumwani
Kwahiyo waliojua dhalimu ni mshamba ndio nyie chawa wake mlisema ni mafisadi? Kwahiyo ile mahakama ya mafisadi iliyoanzishwa na dhalimu magu haikufanya kazi, Bali nyie sukuma gang ndio mkageuka mahakama?
 
Nenda pale jengo la shule ya sheria utakutana na takwimu za kutosha.

Wezi waliopiga fedha za wananchi hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua kwenye hii ripoti ya CAG.
 
Back
Top Bottom