Mwenye nyumba yangu hataki nipike kitimoto

Pelly

Senior Member
Mar 26, 2013
117
91
Habri zenu wana JF,

Nimepanga maeneo fulani hapa Dar lakini mwenye nyumba wangu kamuuliza mke wangu kama tumewahi pika kitimoto akajibiwa hapana kumbe kashamuuliza na dada wa kazi sasa sijui kama daa alimjibu vipi japo yeye anasema dada naye alikatanisasa akasema tusipike kitimoto ndani maana yeye anajisikia vibaya na hapendi,

Swali langu ni atakuwa na matatizo gani maana nasikia kunawatu wanatumia nguruwe kutolea mapepo na madude mengineyo na je nikipika tena atajuaje?

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mji mahali fulani kanda ya ziwa tulikuwa tumepanga na bro zamani sana ndo anajiliwa jeshini. Kutopika kiti moto lilikuwa shart mojawapo. Kuna siku tulinunua kiti moto tukapika mle ndani. Nyumba ilitetemeka yoyote kama vile kuna tetemeko, na kuna kitu kilitonoa bati upande wa chumba chetu kikatua ndani kama jiwe ila hatukukiona kilikuwa nini. Tuliombwa kuhama siku hiyo hiyo na kodi tukarudishiwa
 
Hama kwenye hiyo nyumba ya huyo baladhuli
20200103_175500.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mmmh!
Pole sana
Fanya uwe unatoka out na familia yako, mnakula huko huko mkija ni kuosha tu miguu mnalala
 
Kwakua umepanga ni vizuri kutii masharti ya mwenye nyumba na kuheshimu hisia zake, mwambie ukweli kua wewe huwezi kukaa bila kula kiti moto angalau mara tatu kwa wiki, muombe akurudishie kodi iliyobaki ukapange sehemu nyingine,kama sharti la Kitimoto halipo kwenye mkataba, kama lipo fanya utaratibu uhame, usiteseke wala usiitese familia kwa ajili ya sharti la mtu mmoja. Kingine jihimu uwe na kwako hapo hata kuchinja unaeza chinjia sebuleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom