Mwenye nyumba yangu hataki nipike kitimoto

Mwenye nyumba yangu hataki nipike kitimoto

Ilikuwa na muonekamo Kama wa nyama ya ng'ombe?
miaka imepita,nilienda Kigoma nilifika mchana;nilikuwa na hamu ya kiti nikaenda eneo Fulani wameezeka kwa makuti nadhani Barbara ya airport au km3 kutoka stend

kwa uroho nikatengeneza kilo 2,nikala na nyingine nikaamua kubeba,nikafunga vizuri tena kwa nailoni ili isitoe harufu

wenyeji wangu ni akina masudi.!

kiti cha kwanza kufika wenyeji wangu wakapokea bag na mfuko uliokuwa na kiti moto pamoja na kuwakatalia,wakakimbiza chumbani kwao.!! Nikalala na mawazo


Asubuhi wakati wa chai nashangaa yanaletwa maandazi na chai,pamoja na ile kiti moto na ndizi zikiwa zimepashwa moto.!?!!

imagine... wote walikula.!! na sikuulizwa hii ni nyama gani.?

sema baadae mazahouse aliniambia " ilibidi mboga tuipashe moto ili isiharibike '' nikajikausha

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Comments za humu ndani Ni Kasheshe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Maadam upo unaishi katika nyumba ya mtu,Basi fwata anachotaka.
Kumkomoa kwa kuleta hiyo kitimoto hakujengi chochote zaidi Sana kutaleta uadui.
Kama unashindwa kabisa kufwata anachotaka Basi waweza kuhama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habri zenu wana JF,

Nimepanga maeneo fulani hapa Dar lakini mwenye nyumba wangu kamuuliza mke wangu kama tumewahi pika kitimoto akajibiwa hapana kumbe kashamuuliza na dada wa kazi sasa sijui kama daa alimjibu vipi japo yeye anasema dada naye alikatanisasa akasema tusipike kitimoto ndani maana yeye anajisikia vibaya na hapendi,

Swali langu ni atakuwa na matatizo gani maana nasikia kunawatu wanatumia nguruwe kutolea mapepo na madude mengineyo na je nikipika tena atajuaje?

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukipika CHAIRFIRE atajua kwani?
 
Dada mmoja mtaani kwetu alikuwa akiudhiwa na mpenzi wake ustaadhi utamsikia ngoja nikamlie kiti moto akome maana anapenda sana kunyonya ulimi wakati wa show!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom