Mwenye neno lolote tupia hapa kuniponya

Mwenye neno lolote tupia hapa kuniponya

Ages11

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2024
Posts
285
Reaction score
379
Kwa mara ya kwanza tangu niifanamu jf ndio ninaandika post, samahani kwa uandishi mbaya.
Kilichonisukuma kuandika hii post ni kwamba nimepoteza pambona la maisha na hata nafasi yangu inanishuhudia hilo.

Nimepitia Mikasa Mingi sana hapa duniani tangu utoto wangu, nimepambana vya kutosha bila nafuu, katika ukuaji wangu nilikuwa na marafiki wengi tu lakini mpaka sasa Sina rafiki hata mmoja zaidi ya hapa jf. Niliwapoteza baada ya kupata tatizo la usikivu.

Ninamengi ya kusema lakini sikuja hapa kujieleza matatizo nitajaza saver za jf. Leo ndugu zangu ninauhitaji mkubwa wa neno lako la faraja hata likiwa na herufi nne.
 
Pole sana, mimi mwenyewe nina mild hearing loss na bado naishi.
Kikubwa jikubali tuh, hata uishi kwa namna gani dunia itakujaji tuuh.
 
Nimepitia Mikasa Mingi sana hapa duniani tangu utoto wangu, nimepambana vya kutosha bila nafuu, katika ukuaji wangu nilikuwa na marafiki wengi tu lakini mpaka sasa Sina rafiki hata mmoja zaidi ya hapa jf. Niliwapoteza baada ya kupata tatizo la usikivu.
Kupoteza marafiki sio tatizo la usikivu tu. Hao sio marafiki zako tokea mwanzo walikuwa kama kupe tu wamekosa kukutumia watakavyo wao ndio wameondoka wenyewe.

Rafiki wa kweli atabaki nawe hata uwe chizi atakuja jalalani mcheke kama wote machizi.
 
Kupoteza usikivu hakupotezi utu wako, ona hapa JF tunawasiliana kwa maandishi tu.
Ni kweli mawasiliano yangu mengi ni maandishi, changamoto ya usikivu lilizalizaa ukimya, kwakua marafiki wanapokaa kuzungumza naweza nisijue kwa mapana wanaongelea Nini, hili lilifanya nisiwe napendelea kukaa sehemu wanayozungumza kwasababu nilionekana msumbufu kwa kuuliza maswali Ili na Mimi nielewe. Nikawa mtu wa pekeyangu tu.
 
Ni kweli mawasiliano yangu mengi ni maandisha, changamoto ya usikivu lilizalizaa ukimya, kwakua marafiki wanapoka kuzungumza naweza nisijue kwa mapana wanaongelea Nini, hili lilifanya nisiwe napendelea kukaa sehemu wanayozungumza kwasababu nilionekana msumbufu kwa kuuliza maswali Ili na Mimi nielewe. Nikawa mtu wa pekeyangu tu.
Vipi kuhusu jamii za watu kama wewe? Hakuna uwezekano wa kuungana na kuwa na urafiki? Naamini wapo wengine kama wewe.

Unajua kutumia lugha ya ishara (sign language) ?

Umeangalia uwezekano wa kutumia hearing aids kama inawezekana?
 
Pole Sana ,

Unapitia changamoto gani kutokana na tatizo lako usikivu hafifu ?

Kukosa Kazi ?
Kutengwa na ndugu na marafiki?

Je , umewahi kufikiria kuanzisha WhatsApp groups then ukawatafuta watu wenye the same situation Kama yako mkawa mnabadilisha mawazo na kupeana mbinu za Ku-handle the situation/problem.

Tatizo la usikivu ni tatizo la kawaida Ila , linataonekana kubwa kubwa Kama ukifanyiwa bullying .

Nawaza Kama utaibadilisha hii changamoto iwe fursa .

Fanya hivi watafute watu wenye shida Kama yako

Then fungueni groups lenu muwe mnapeanza experience na njia mbalimbali za kuishi au kuishinda hii changamoto

HOV .
 
Hili tatizo lilianzaje mkuu kama hutojali kutolea maelezo.
Nilianza kwa kushindwa kuona vizuri mwaka 2012,nilipewa dawa mbalimbali sikumbuki kwa sasa ila zilikuwepo Prednisone pamoja vitamin B, kipindi natumia hizo dawa masikio yalikwa yanapiga sana kelele ,tatizo la uoni hafifu lilipoisha ndio likaja hili la usikivu.
 
Mimi na washkaji zangu kama watatu hivi hawaskii Wala kuongea lakini uwezo wa kuandika na kuwasiliana kwa ishara wanao.
Jamaa wana enjoy sana maisha hawana wasiwasi na muda mwingine wenyewe ndio huwa wananishauri mimi🙏.

Amini upo wakati wako utapata marafiki sahihi kwenye maisha yako usikate tamaa kabla hajaenda kuwatazana wagonjwa mahututi hospital..hao wamepoteza uwezo wa kufanya chochote kwenye milli Yao
 
Kwa mara ya kwanza tangu niifanamu jf ndio ninaandika post, samahani kwa uandishi mbaya.
Kilichonisukuma kuandika hii post ni kwamba nimepoteza pambona la maisha na hata nafasi yangu inanishuhudia hilo.

Nimepitia Mikasa Mingi sana hapa duniani tangu utoto wangu, nimepambana vya kutosha bila nafuu, katika ukuaji wangu nilikuwa na marafiki wengi tu lakini mpaka sasa Sina rafiki hata mmoja zaidi ya hapa jf. Niliwapoteza baada ya kupata tatizo la usikivu.

Ninamengi ya kusema lakini sikuja hapa kujieleza matatizo nitajaza saver za jf. Leo ndugu zangu ninauhitaji mkubwa wa neno lako la faraja hata likiwa na herufi nne.
Pole sana, umefika mpaka siku ya leo kwa kusudi, usikate tamaa, kila jambo lina mwisho wake, utaifikia siku ambayo mapito yako yataisha pia na labda tatizo lako la kusikia litapata ufumbuzi.

Sending you hugs 🫂🤗🫂
 
Kwa mara ya kwanza tangu niifanamu jf ndio ninaandika post, samahani kwa uandishi mbaya.
Kilichonisukuma kuandika hii post ni kwamba nimepoteza pambona la maisha na hata nafasi yangu inanishuhudia hilo.

Nimepitia Mikasa Mingi sana hapa duniani tangu utoto wangu, nimepambana vya kutosha bila nafuu, katika ukuaji wangu nilikuwa na marafiki wengi tu lakini mpaka sasa Sina rafiki hata mmoja zaidi ya hapa jf. Niliwapoteza baada ya kupata tatizo la usikivu.

Ninamengi ya kusema lakini sikuja hapa kujieleza matatizo nitajaza saver za jf. Leo ndugu zangu ninauhitaji mkubwa wa neno lako la faraja hata likiwa na herufi nne.
Shida yako sio usikivu Shida yako kubwa ni mindset yako

Change Ur attitude change that frequency maisha yako yatabadilika
 
Back
Top Bottom