Mwenge wa Uhuru Wazindua Miradi Jimbo la Momba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Ndugu Abdallah Shaibu tarehe 02 Septemba, 2023 amepongeza utekelezaji wa miradi ndani ya Wilaya ya Momba na kusisistiza kuendeleza utunzaji wa mazingira.

Mbunge wa Jimbo la Momba, Mhe. Condester Sichalwe amewasisitiza watu wa bonde (Game Reserves) kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kuongeza Utunzaji mzuri wa Maliasili na kuacha kuwanyanyanyasa wananchi kwa kuwapiga na kuwanyang'anya vitendea kazi vyao, hivyo elimu izidi kutolewa kwa wananchi.

Mhe. Condester Sichalwe akiwa Kata ya Kamsamba ameishukuru Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Ninapoomba fedha ninasikilizwa, miradi inakuaj. Ninapoainisha matatizo ya wananchi wa Momba Serikali ya CCM inasikia" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Kwa viongozi mlioaminiwa na Serikali kusimamia miradi, watu wanapokuja kuchezea fedha za Serikali, fedha ya wanyonge Mimi kama Mbunge sitanyamanza. Kazi yangu kubwa ni kutafuta fedha kwaajili ya wana Kamsamba na wana Momba lakini iko hatua ya usimamizi inakuja" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba.

Mwenge wa Uhuru umefika katika Kata ya Mkulwe Jimboni Momba na kuzindua mradi wa Maji wa Itelefya ili kutimiza adhma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama Ndoo kichwani.


 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-09-02 at 23.03.33.mp4
    3.2 MB
  • WhatsApp Video 2023-09-02 at 22.43.24.mp4
    18.4 MB
  • WhatsApp Video 2023-09-02 at 22.58.53.mp4
    23.4 MB
  • WhatsApp Image 2023-09-02 at 22.38.27.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-02 at 22.38.27.jpeg
    72.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-09-02 at 22.38.23.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-02 at 22.38.23.jpeg
    59.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-02 at 22.39.49.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-02 at 22.39.49.jpeg
    93.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom