Wakuu hii hoja haiwezi kupita bila ya kutendewa haki.
Kabla sijaanza naomba kama Mamlaka husika hasa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dk.Pombe Magufuli watapitia huku jukwaani tunaomba wafahamu barabara hii ni zaidi ya kero, tunaomba ifumuliwe upya na ijengwe kulingana na misingi ambayo inaeleweka n ahata Waziri wetu huyu anaifahamu.
Ni aibu kwa barabara kubwa kama hiii inayotumika na takribani vigogo wengi wa Nchi hii akiwemo Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina kasoro ambazo hata mimi ambaye sikusomea uhandisi wa barabara ninaziona wazi:
1. Inatakiwa gari inayopinda kuelekea kulia ama kushoto iwekewe diversion angle ambayo itawezesha gari hilo kupinda kona na kuliruhusu gari la nyuma yake kuendelea na safari kama ilivyo kwa barabara za Nyerere na nyinginezo.
Kama alivyosema mtoa hoja, kwa watu wanaongia barabara za pembezoni tukianzia eneo la Kwakomba, kuna barabara ya Zawadi inayoingia Mbezi juu kwa Mheshimiwa Mbunge Shekifu. Mtu anayetoka Mbezi juu kuelekea Mwenge amenyimwa juction inayomwezesha yeye kukata kulia kwake na kuingia barabara ya kuelekea mwenge mpaka kwanza akate kushoto nakuelekea Tegeta mpaka eneo la Tanki bovu ndipo apinde tena kulia na kurudi tena mpaka KwaKomba ndipo aendelee na safari yake ya Mwenge. Kwanini wasiweke sehemu ya kuingilia hapo hapo Zawadi Road? Kwanini wasifanye kama walivyofanya pale Makonde?
2. Kitu kingine cha hatari ni hizi sehemu za kugeuzia magarikutoka barabara moja kuingia nyingine ni finyu sana kiasi kwamba magari mawili yakikutana pale kuna uwezekano mkubwa wa kugongana hasa kwa kuwa kwanza hakuna ile diversion angle ambayo inamuelekeza mtumiaji kwamba sasa unaingia zone ya kupinda kulia au kushoto. Na ikitokea gari zimepigana pini tayari nyuma inakuwa foleni ndefu tayari imezaliwa.
3. Barabara ni finyu sana bila shaka watakuwa wametumia vipimo vya bajaji maana ukiangalia gari mbili kubwa zinapoeleka sehemu moja utaona uwazi unaoachwa katikati ni mdogo sana.
4. Barabara hata kukamilika haijakamilika tayari kutokea tanki bovu mpaka Tegeta tayari imetengeneza matuta utafikiri mkulima ameandaa shamba kwa ajili ya kupanda viazi.
Barabara hii ni majanga, mheshimiwa Magufuli tunaomba utumie na huku rungu lilelile ulilotumia barabara ya Kilwa kuponda wote waliozembea.
Kweli mdau umelonga,hii barabara mimi mwenyewe huwa najiuliza hawa wakandarasi wako field kama wanafunzi au ni wakandarasi weledi.Mfano mwingine wa udhaifu wa hii barabara ni kuanzia maeneo ya mbuyuni unapopandisha kwenda stendi tayari lami inatitia,achilia ilo njoo tegeta darajani foleni kubwa ni balaa.Mimi namshauri waziri kituo cha Tegeta kwa ndevu kipanuliwe kwa kuondoa maduka ya upande wa kushoto(walipwe fidia) ili daladala ziweze kuingia ndani ya kituo kama Ubungo tanesco pale,hii itasaidia kupunguza foleni ya Tegeta darajani.Na pia ushauri kwa watu wanaoishi kuanzia maeneo ya basihaya mpaka Bunju,hakuna ulazima wowote wa kupitia tegeta kwa ndevu,wapitie maeneo ya bahari Beach kuelekea ununio mpaka CCM then waunganishe mpaka Bunju kwa kuchepukia Mbuyuni ili kupisha watu wanaoelekea Wazo,Tegeta kibaoni n.k.Wakuu hii hoja haiwezi kupita bila ya kutendewa haki.
Kabla sijaanza naomba kama Mamlaka husika hasa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dk.Pombe Magufuli watapitia huku jukwaani tunaomba wafahamu barabara hii ni zaidi ya kero, tunaomba ifumuliwe upya na ijengwe kulingana na misingi ambayo inaeleweka n ahata Waziri wetu huyu anaifahamu.
Ni aibu kwa barabara kubwa kama hiii inayotumika na takribani vigogo wengi wa Nchi hii akiwemo Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina kasoro ambazo hata mimi ambaye sikusomea uhandisi wa barabara ninaziona wazi:
1. Inatakiwa gari inayopinda kuelekea kulia ama kushoto iwekewe diversion angle ambayo itawezesha gari hilo kupinda kona na kuliruhusu gari la nyuma yake kuendelea na safari kama ilivyo kwa barabara za Nyerere na nyinginezo.
Kama alivyosema mtoa hoja, kwa watu wanaongia barabara za pembezoni tukianzia eneo la Kwakomba, kuna barabara ya Zawadi inayoingia Mbezi juu kwa Mheshimiwa Mbunge Shekifu. Mtu anayetoka Mbezi juu kuelekea Mwenge amenyimwa juction inayomwezesha yeye kukata kulia kwake na kuingia barabara ya kuelekea mwenge mpaka kwanza akate kushoto nakuelekea Tegeta mpaka eneo la Tanki bovu ndipo apinde tena kulia na kurudi tena mpaka KwaKomba ndipo aendelee na safari yake ya Mwenge. Kwanini wasiweke sehemu ya kuingilia hapo hapo Zawadi Road? Kwanini wasifanye kama walivyofanya pale Makonde?
2. Kitu kingine cha hatari ni hizi sehemu za kugeuzia magarikutoka barabara moja kuingia nyingine ni finyu sana kiasi kwamba magari mawili yakikutana pale kuna uwezekano mkubwa wa kugongana hasa kwa kuwa kwanza hakuna ile diversion angle ambayo inamuelekeza mtumiaji kwamba sasa unaingia zone ya kupinda kulia au kushoto. Na ikitokea gari zimepigana pini tayari nyuma inakuwa foleni ndefu tayari imezaliwa.
3. Barabara ni finyu sana bila shaka watakuwa wametumia vipimo vya bajaji maana ukiangalia gari mbili kubwa zinapoeleka sehemu moja utaona uwazi unaoachwa katikati ni mdogo sana.
4. Barabara hata kukamilika haijakamilika tayari kutokea tanki bovu mpaka Tegeta tayari imetengeneza matuta utafikiri mkulima ameandaa shamba kwa ajili ya kupanda viazi.
Barabara hii ni majanga, mheshimiwa Magufuli tunaomba utumie na huku rungu lilelile ulilotumia barabara ya Kilwa kuponda wote waliozembea.
Kweli mdau umelonga,hii barabara mimi mwenyewe huwa najiuliza hawa wakandarasi wako field kama wanafunzi au ni wakandarasi weledi.Mfano mwingine wa udhaifu wa hii barabara ni kuanzia maeneo ya mbuyuni unapopandisha kwenda stendi tayari lami inatitia,achilia ilo njoo tegeta darajani foleni kubwa ni balaa.Mimi namshauri waziri kituo cha Tegeta kwa ndevu kipanuliwe kwa kuondoa maduka ya upande wa kushoto(walipwe fidia) ili daladala ziweze kuingia ndani ya kituo kama Ubungo tanesco pale,hii itasaidia kupunguza foleni ya Tegeta darajani.Na pia ushauri kwa watu wanaoishi kuanzia maeneo ya basihaya mpaka Bunju,hakuna ulazima wowote wa kupitia tegeta kwa ndevu,wapitie maeneo ya bahari Beach kuelekea ununio mpaka CCM then waunganishe mpaka Bunju kwa kuchepukia Mbuyuni ili kupisha watu wanaoelekea Wazo,Tegeta kibaoni n.k.
Dada yangu nashukuru kwa kuliona hilo, ahsante kwa kunikumbusha, hapo napo nikero mpaka wakati mwingine huwa najiuliza hivi hii nchi watu wanaitumia kufanyia majaribio wahandishi wanafunzi wao nini!!!Na kwa kuongezea hapo mtu anayetoka tegeta kwenda interchick inamlazimu aende mpaka makonde then arudi nyuma tena via samaki samaki ndipo afike interchick. hii barabara ni ya ajabu sana
Kumbe Kiswahili kinajitosheleza sana!Si walifanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina? Si mchakato ulijadiriwa? Hata kama hoja ni mtambuka nadhan wahusika wawajibishwe.
Kwa kweli inasikitisha sana kuhusu mtaalamu aliye chora na kupitisha ramani ya barabara inayoanzia mwenge mpaka Tegeta. Wengi wa watumiaji tunapata taabu sana tunapotaka kuingia barabara za pembezoni.
Mara nyingi tumejikuta tukiwa katika hatari ya kugongwa kwa nyuma ya magari yetu kwa ukosefu wa maeneo ya kuwapisha wenzetu wanaotakiwa kwenda moja kwa moja.
Mfano mzuri ni pale Tangi Bovu kama unatoka mjini na unataka kuingia upande wa kulia yaani Ally Sykes road au anayetoka barabara hiyo na kutaka kuelekea Tegeta wote hao wanakuwa katika hatari ya kupata ajali.
Tunaomba mamlaka husika kabla ya kuipokea barabara hii watoe ushauri na maagizo ya kufanyiwa marekebisho sehemu zote hizo ili ionekane tuna wataalamu wanaojenga barabara za karne hii.
Hii barabara ni majanga na aibu kubwa hao wahandisi wa TANROADS wamekalia ufisadi tu wanazunguka nchi za wezetu kuna barabara zenye design nzuri ajabu halafu wanakuja kuleta vioja yaani sehemu zote kungia upande wa pili ni majanga kuanzia hapo Tanki bovu, maenea ya karibu na engeni, kungia kunduchi na barabara inayochipukia salasala ni hatari tupu
Na kwa kuongezea hapo mtu anayetoka tegeta kwenda interchick inamlazimu aende mpaka makonde then arudi nyuma tena via samaki samaki ndipo afike interchick. hii barabara ni ya ajabu sana
Yaani ni hatari tupu, kama wao hawana ujanja basi si wangedesa hata kwenye bara ya "Sam Nujoma" ! wao ni wakosa kwa upande mmoja lakini hata monitors na mafundi wazalendo nao ni wakosa vile vile! kila anaepewa kazi anawaza "whether it pays or not" hakuna mtendaji anaewaza maslahi ya taifa...Kwa kweli inasikitisha sana kuhusu mtaalamu aliye chora na kupitisha ramani ya barabara inayoanzia mwenge mpaka Tegeta. Wengi wa watumiaji tunapata taabu sana tunapotaka kuingia barabara za pembezoni.