Mwenge-Tegeta Road: Poorly designed, poorly constructed! Nani awajibike?

Joined
Jul 20, 2013
Posts
7
Reaction score
17
Kwa kweli inasikitisha sana kuhusu mtaalamu aliye chora na kupitisha ramani ya barabara inayoanzia mwenge mpaka Tegeta. Wengi wa watumiaji tunapata taabu sana tunapotaka kuingia barabara za pembezoni.

Mara nyingi tumejikuta tukiwa katika hatari ya kugongwa kwa nyuma ya magari yetu kwa ukosefu wa maeneo ya kuwapisha wenzetu wanaotakiwa kwenda moja kwa moja.

Mfano mzuri ni pale Tangi Bovu kama unatoka mjini na unataka kuingia upande wa kulia yaani Ally Sykes road au anayetoka barabara hiyo na kutaka kuelekea Tegeta wote hao wanakuwa katika hatari ya kupata ajali.

Tunaomba mamlaka husika kabla ya kuipokea barabara hii watoe ushauri na maagizo ya kufanyiwa marekebisho sehemu zote hizo ili ionekane tuna wataalamu wanaojenga barabara za karne hii.
 
wenzio hawakuwa na muda huo wa kuangalia michoro maana mfadhili alishkubali kutoa pesa na akili yote ilikuwa kwenye 10%! Inakuwa aibu kwa miradi mikubwa na ya muda mrefu kama hii kujengwa kwa mawazo ya kutafutia umaarufu na kura za muda mfupi tu!
 
Si walifanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina? Si mchakato ulijadiriwa? Hata kama hoja ni mtambuka nadhan wahusika wawajibishwe.
 
Hata hapo Sams fenicha napo ukitaka kuingia upande wa Engen ni kasheshe, ajali zimetokea mara mbili. Kibaya zaidi hamna matuta yoyote magari sasa hivi yanakimbia ovyo hivyo mtu kwenye hizi junction ni hatari, hapo hujaongeza Bajaj na pikpik zinazochomekea tu bila tahadhari....
 
Wakuu hii hoja haiwezi kupita bila ya kutendewa haki.

Kabla sijaanza naomba kama Mamlaka husika hasa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dk.Pombe Magufuli watapitia huku jukwaani tunaomba wafahamu barabara hii ni zaidi ya kero, tunaomba ifumuliwe upya na ijengwe kulingana na misingi ambayo inaeleweka n ahata Waziri wetu huyu anaifahamu.

Ni aibu kwa barabara kubwa kama hiii inayotumika na takribani vigogo wengi wa Nchi hii akiwemo Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina kasoro ambazo hata mimi ambaye sikusomea uhandisi wa barabara ninaziona wazi:
1. Inatakiwa gari inayopinda kuelekea kulia ama kushoto iwekewe diversion angle ambayo itawezesha gari hilo kupinda kona na kuliruhusu gari la nyuma yake kuendelea na safari kama ilivyo kwa barabara za Nyerere na nyinginezo.

Kama alivyosema mtoa hoja, kwa watu wanaongia barabara za pembezoni tukianzia eneo la Kwakomba, kuna barabara ya Zawadi inayoingia Mbezi juu kwa Mheshimiwa Mbunge Shekifu. Mtu anayetoka Mbezi juu kuelekea Mwenge amenyimwa juction inayomwezesha yeye kukata kulia kwake na kuingia barabara ya kuelekea mwenge mpaka kwanza akate kushoto nakuelekea Tegeta mpaka eneo la Tanki bovu ndipo apinde tena kulia na kurudi tena mpaka KwaKomba ndipo aendelee na safari yake ya Mwenge. Kwanini wasiweke sehemu ya kuingilia hapo hapo Zawadi Road? Kwanini wasifanye kama walivyofanya pale Makonde?

2. Kitu kingine cha hatari ni hizi sehemu za kugeuzia magarikutoka barabara moja kuingia nyingine ni finyu sana kiasi kwamba magari mawili yakikutana pale kuna uwezekano mkubwa wa kugongana hasa kwa kuwa kwanza hakuna ile diversion angle ambayo inamuelekeza mtumiaji kwamba sasa unaingia zone ya kupinda kulia au kushoto. Na ikitokea gari zimepigana pini tayari nyuma inakuwa foleni ndefu tayari imezaliwa.

3. Barabara ni finyu sana bila shaka watakuwa wametumia vipimo vya bajaji maana ukiangalia gari mbili kubwa zinapoeleka sehemu moja utaona uwazi unaoachwa katikati ni mdogo sana.

4. Barabara hata kukamilika haijakamilika tayari kutokea tanki bovu mpaka Tegeta tayari imetengeneza matuta utafikiri mkulima ameandaa shamba kwa ajili ya kupanda viazi.

Barabara hii ni majanga, mheshimiwa Magufuli tunaomba utumie na huku rungu lilelile ulilotumia barabara ya Kilwa kuponda wote waliozembea.
 
Vipi kuhusu ukubwa/upana wa hilo"tuta" linalogawa barabara? Kero tupu!
 
Hii barabara ni majanga na aibu kubwa hao wahandisi wa TANROADS wamekalia ufisadi tu wanazunguka nchi za wezetu kuna barabara zenye design nzuri ajabu halafu wanakuja kuleta vioja yaani sehemu zote kungia upande wa pili ni majanga kuanzia hapo Tanki bovu, maenea ya karibu na engeni, kungia kunduchi na barabara inayochipukia salasala ni hatari tupu
 
Hivi kweli kwa hali kama hii tutasema tuna uongozi kweli, ina maana hawalioni hili. Na mbaya zaidi kila siku tunapigana nao vikumbo wakitumia barabara hiyo hiyo mbovu tena wakiwa kimya.
 
mnajua hata hii barabara ya mabasi yaendayo kasi imejengwa utadhani ipo mbugani. Barabara za kuchepuka sehemu nyingine wameziba kabsaa. Pale tanesco migomigo waliziba kabisa mpaka walipoambika kuwa kuna watu na ofisi pembeni ya barabara ndo wakabomoa. Hizi barabara ni za viwango duni mno
 
Jamani ndugu zangu watanzania,wakati mwengine tusilaumu kila kitu serikali,Je tujiulize pia madereva wengi Tanzania wanafahamu sheria za barabarani,maana hizo barabara zimejengwa kwa ufadhili wa nchi za nje na hao wafadhili wana watu wao pia uishi nchini ,na huko kwao unaweza kukuta kuna barabara ya 3km uruhusiwi ku..overtake..na wao kwa kuwa wanafahamu sheria za barabarani vizuri utii ,lakini kivumbi tanzania kila mtu mbabe barabarani,.kwa sababu hizo basi lazima nyinyi kama wapenda sifa barabarani muone tofauti..tiii sheria barabarani ujikinge au uaifanye ajali.
 
Kuna mtu humu ameongelea suala la kunyimwa kuovateki? Umesoma hoja mojamoja vizuri kweli? Unaifahamu vizuri hiyo barabara inayoongelewa hapa?
 
Sifahamu kabisa hiyo barabara inayoongelewa ,hila ulikuwa ni ushauri tuu,ni vizuri pia kuzingatia za barabarani,maana katika tembea tembea zetu huko kwa wenzetu ,utakuta katika barabara kuna mwingiliano au mchanganyiko wa treni,motokaa,baiskeli na na mabusi,katika njia moja..ambayo wewe kama dereva lazima ujue ni wakati gani muafaka wa wewe kukata kona na kuwapisha,au nani anayepaswa kuanza kukata kona,na hili kufahamu hivyo ni lazima kuudhuria shule ya udereva,ambayo gharama zake kwa kweli ni kubwa ,pia lazima katika mtihani wa udereva ufaulu vizuri ndio unapata leseni ,sasa kwa nyumbani sijui kuna taratibu gani ufanyika hili tuwe na madereva wazuri ambao wataweza kuheshimu sheria za barabarani,tupunguze hizo ajali.. ,,samahani lakini kwa hilo hila umuhimu wa kujua sheria za barabarani ni muhimu sana..,
 
wenzio hawakuwa na muda huo wa kuangalia michoro maana mfadhili alishkubali kutoa pesa na akili yote ilikuwa kwenye 10%! Inakuwa aibu kwa miradi mikubwa na ya muda mrefu kama hii kujengwa kwa mawazo ya kutafutia umaarufu na kura za muda mfupi tu!
PENYE WEZI WENGI haki ya mtu ni kufa kwake!
 
Back
Top Bottom