JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,462
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana amesema mgomo unaoendelea leo unasababishwa na kikundi cha watu wachache wenye maslahi yao binafsi huku akiomba wachukuliwe hatua na kuahidi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.
Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 16, 2023 wakati akizungumza na Mwananchi kufuatia baadhi ya maduka kuendelea kufungwa, licha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana kuwataka wafanyabiashara hao kusitisha mgomo huku akiahidi kushughulikia kero zao kikao cha kesho Jumatano ya Mei 17, 2023.
Mbwana amesema kilio chao kama wafanyabiashara ilikuwa ni kusikilizwa na Rais Samia Suluhu Hassan, na katika kuonyesha kuwa amewasikia alimtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
"Alipokuja aliwaomba wafanyabiashara wafungue maduka na kuahidi kuwasiliza siku ya Jumatano. Nashangaa wafanyabiashara kuwa hawana imani na Waziru Mkuu," amesema
Amesema shida ni kikundi cha watu wachache wanaoonekana kuwa na manufaa na mgomo huo huku akieleza kuwa ameomba msaada kwa vyombo vya usalama kuwachukulia hatua na kusema yupo tayari kutoa ushirikiano.
POLISI WATOA TAMKO
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wapo tayari kuimarisha usalama kwa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo watakaofungua maduka yao huku akiwatahadharisha watakaoleta vurugu.
Muliro ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 16, 2023 alipotembelea wafanyabiashara wa Kariakoo.
“Tupo kuimarisha usalama watakaofunga wafunge nasema ole wake atakeyekwenda kumsumbua atakayefungua tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jana alitoa maagizo na maelekezo yake yameeleweka” amesema Muliro na kuongeza,
“Watu wanaofungua maduka tunawahakikishia usalama, tumeshaweka askari mbalimbali mtu anayetaka afunge lakini anayetaka kufungua afungue usalama upo.
“Mtu yeyote atakayefungua biashara wafanye na natoa onyo kali atakayekwenda kufanya fujo hatua kali zitachukuliwa.”
Chanzo: Mwananchi