mcshonde
Member
- Jul 15, 2022
- 66
- 154
Wao pia wameungana na wenzao kutoa sababu kuwa ni urasimu, pamoja na kero wanayopata kutoka kwa watendaji wa mamlaka ya mapato TRA.
=======
Suala la wafanyabiashara wa Kariakoo kutangaza mgomo wa kufunga maduka limefika hadi maeneo ya Manzese ambapo baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya jumla na rejareja wameamua kutofungua biashara zao.

Wafanyabiashara hawa wameomba mchakato wa kusikilizwa ufanywe kama ilivyopangwa ili waweze kurudi kuendelea na shuguli zao kwani kuna mnyororo wa watu wengi wanaoathirika na hali hiyo.
Ifahamike kuwa tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshaazimia kukutana na kamati ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Mawaziri wa sekta husika na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA). Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Saa 8 Mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu MAGOGONI- ikulu Jumatano tarehe 17 Mei 2023.
MC Shonde