Mwenyekiti Wafanyabiashara Kariakoo Aomba Msaada Kuwakamata Waliofunga Maduka

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana amesema mgomo unaoendelea leo unasababishwa na kikundi cha watu wachache wenye maslahi yao binafsi huku akiomba wachukuliwe hatua na kuahidi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 16, 2023 wakati akizungumza na Mwananchi kufuatia baadhi ya maduka kuendelea kufungwa, licha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana kuwataka wafanyabiashara hao kusitisha mgomo huku akiahidi kushughulikia kero zao kikao cha kesho Jumatano ya Mei 17, 2023.

Mbwana amesema kilio chao kama wafanyabiashara ilikuwa ni kusikilizwa na Rais Samia Suluhu Hassan, na katika kuonyesha kuwa amewasikia alimtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

"Alipokuja aliwaomba wafanyabiashara wafungue maduka na kuahidi kuwasiliza siku ya Jumatano. Nashangaa wafanyabiashara kuwa hawana imani na Waziri Mkuu," amesema

Amesema shida ni kikundi cha watu wachache wanaoonekana kuwa na manufaa na mgomo huo huku akieleza kuwa ameomba msaada kwa vyombo vya usalama kuwachukulia hatua na kusema yupo tayari kutoa ushirikiano.

Chanzo: Mwananchi
 
Chanzo:Mwananchi
Mwenyekiti my shoes
 
Mamlaka lazima yaheshimiwe, mimi nawatetea sana wafanya biashara sababu najuwa TRA kuna shida sana lakini pia kuna wafanya biashara wengi tu ujanja mwingi kukwepa kulipa kodi hili wala sio siri. Sasa nataka niongee kwa ufupi huwezi kumtaka Raisi aje aingile direct tatizo kama hili sasa je akija halafu azomewe na akataliwe ombi fungueni nini kitatokea? ni hatari sana Rais atatoa tamko kila kitu kikiwa kimewekwa sawa sio kujadiliana je baada ya Rais mtaenda wapi? fujo au? tusifanye mambo kwa mihemuko hata mimi ningekuwa Rais nisingekubali hili kesho likitokea Mwanza, Dodoma sijui Iringa Rais aende? tuwe serious katika mambo ya nchi ni kweli TRA ni shida sana na pia ukwepaji wa kodi uko sana tu hakuna ubishi. Hata waziri mkuu kwenda pale ilikuwa hatua ya haraka na sio sawa ina poteza nguvu za walio chini ndio maana RC kupoteza sababu alikataliwa hadharani ina maana power hana tena na ukimkatalia waziri mkuu unamfanya kuwa dhaifu kabaki Rais naye mkija kumzomea atapoteza kila kitu na nchi itakuwa haitawaliki. Serikali itoe tamko kali kwa watu wenye kutaka kuleta madhara ya kiuchumi dawa hapa cance all lincence na tuanze upya hapo hapo sheria za TRA ziwekwe sawa ila hili la store ni majanga na hili nasema na uhakika nalo kuna bidhaa dukani utakuta inauzwa Mil 1 lakini ukiwa na connection utapata kwa laki 3, kwanini? ziko mali zimewekwa huko hazijalipiwa usidhani sheria hii kuja wamekurupuka wanajuwa nini kipo.
 
TRA Pana vijana wahuni Sana
 
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana amesema mgomo unaoendelea leo unasababishwa na kikundi cha watu wachache wenye maslahi yao binafsi huku akiomba wachukuliwe hatua na kuahidi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 16, 2023 wakati akizungumza na Mwananchi kufuatia baadhi ya maduka kuendelea kufungwa, licha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana kuwataka wafanyabiashara hao kusitisha mgomo huku akiahidi kushughulikia kero zao kikao cha kesho Jumatano ya Mei 17, 2023.

Mbwana amesema kilio chao kama wafanyabiashara ilikuwa ni kusikilizwa na Rais Samia Suluhu Hassan, na katika kuonyesha kuwa amewasikia alimtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

"Alipokuja aliwaomba wafanyabiashara wafungue maduka na kuahidi kuwasiliza siku ya Jumatano. Nashangaa wafanyabiashara kuwa hawana imani na Waziri Mkuu," amesema

Amesema shida ni kikundi cha watu wachache wanaoonekana kuwa na manufaa na mgomo huo huku akieleza kuwa ameomba msaada kwa vyombo vya usalama kuwachukulia hatua na kusema yupo tayari kutoa ushirikiano.

Chanzo: Mwananchi
mimi nimemsikia Huyu Bwana Martin sijasikia sehemu ambayo hayo.... kuna uvumishaji wenye manufaa kwa wanaovumisha!
 
Back
Top Bottom