Mwauwasa (Mwanza): Tunazalisha maji Lita Milioni 90 kwa siku, mahitaji ni Lita Milioni 160

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Mohamed Saif anafafanua:

"Kwanza sio kweli kwamba hatutoi taarifa kwa wateja wetu kuhusu mgao, mamlaka imekuwa ikitoa taarifa kupitia njia mbalimbali kupitia mitandao yetu, vyombo vya habari na kwa kuwatumia ujumbe wateja wetu kwa njia ya simu na kwa kutumia viongozi wa ngazi ya Serikali za Mtaa.

"Kuhusu suala la mgao wa maji, Kituo chetu cha Capri Point kinazalisha maji Lita Milioni 90 kwa siku wakati mahitaji ya maji kwa Jiji la Mwanza ni zaidi ya Lita Milioni 160, hali hiyo inasababisha kuwepo na mgao.

"Kutokana na hali hiyo tunachagua baadhi ya maeneo ambayo yanalazimika kuwa na mgao hasa yaliyopo pembezoni mwa Jiji na ambayo yana miinuko.

"Mwanza maeneo mengi yana miinuko na maji hayapandi mlima, hali ambayo inalazimika kuhitajika kwa nguvu ya ziada kupandisha maji juu.

"Malengo yaliyopo ili kupunguza changamoto hiyo, kuna Mradi wa Butimba ambao ukikamilika utazalisha maji Lita Milioni 160 kwa siku.

"Mradi huo una Hatua Mbili, Hatua ya Kwanza ambayo itazalisha mali Lita Milioni 48 kwa siku, imekamilika kwa wastani wa 92%, Mungu akijaalia mwezi mmoja kutoka leo (Agosti 16, 2023) au ndani ya mwaka huu maji yanatarajiwa kuanza kuzalishwa kutoka katika mradi huo.

"Baada ya hapo Hatua ya Pili itafuata, wakati huohuo mpango mwingine wa baadaye ni maboresho ya chanzo chetu cha Capri Point ambapo mambo yakienda swa tunatarajia kuzalisha maji Lita Milioni 100 kwa siku, baadaye pia Serikali imepanga kujenga chanzo kingine maeneo ya Igombe ambacho kitazalisha maji Lita Milioni 200 kwa siku, hiyo ni miaka ya baadaye."

Pia Soma:
 
Kumbe wanasikiliza...haya basi uo mgao uwe na usawa...huku cappripoint hamna mgao na ikifika jioni mara nyingi kituo chao cha kuzalisha maji huwa kinakua na maji mengi sana mpaka wanayarudisha ziwani kwa njia ya mfereji !! Pole nyingi ziende kwa watu wa Usagara, Nyamhongolo, Buswelu, Kisesa na Igoma.
 
Maji ni changamoto hata Dodoma! Inaonyesha tunazaliana sana bila kujua maji tutapata wapi!
 
HoD yuko busy kubambikia watu kesi uchwara badala ya ku deal na vitu muhimu
wacha tuone
 
Sawa, Lita mil 90 kwa wakati wakati mahitaji ni kita mil 160. Kwa hessbu hizo inamaana, watu wangekosa maji kwa siku moja na ya pili, wanapata. Lakini ni wiki ya tatu sasa, Mitaa ya Buhongwa, Maliza hadi Rwahima, hakuna maji kabisa. Mamlaka zichukue hatua
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Ni aibu mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na changamoto ya Maji pamoja na kuwa jirani na Ziwa Victoria na Tanganyika.

Wenzetu Misri hawana ziwa lakini wanasafirisha maji ya kunywa na shughuli nyingine za uzalishaji kutoka Ziwa Victoria.

Waswahili walisema kosa mali upate akili 🙌
 
Kumbe wanasikiliza...haya basi uo mgao uwe na usawa...huku cappripoint hamna mgao na ikifika jioni mara nyingi kituo chao cha kuzalisha maji huwa kinakua na maji mengi sana mpaka wanayarudisha ziwani kwa njia ya mfereji !! Pole nyingi ziende kwa watu wa Usagara, Nyamhongolo, Buswelu, Kisesa na Igoma.
Mimi nipo hapa Usagara mkuu hali ya maji sio mbaya sana
 
Matokeo oparesheni 255 na kurejesha bandari yameanza kuonekana ,zimeaza kutajwa mpaka lita
 
Ni aibu mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na changamoto ya Maji pamoja na kuwa jirani na Ziwa Victoria na Tanganyika.

Wenzetu Misri hawana ziwa lakini wanasafirisha maji ya kunywa na shughuli nyingine za uzalishaji kutoka Ziwa Victoria.

Waswahili walisema kosa mali upate akili
Uafrika hasa utanzania ni laana.
 
Back
Top Bottom