Mwarabu mwingine apewa mkataba wa kufanya utafiti, kazi ambayo ingefanywa na wataalamu wetu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,240
103,917
IMG-20230710-WA0003.jpg

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni ya TAQA ya nchini Misri wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika kufanya utafiti na kuangalia masoko ya gesi asilia katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Biashara ya Mafuta na Gesi kutoka TPDC Bw. William Chiome amesema, matokeo ya utafiti huo yatasaidia kuwepo kwa mipango madhubuti ya kusambaza gesi asilia kwa matumizi tofauti.

“Utafiti huu utaenda kufanyika na kukamilika ndani ya mwaka mmoja, na matokeo yake yatawezesha TPDC na makampuni binafsi kujipanga kupeleka miundombinu ya gesi asilia kwa watumiaji mbalimbali sawa na uhitaji ulioonekan,” amesema Chiome.

Kwa sasa kampuni ya TAQA inaendelea na ujenzi wa vituo viwili vya kujazia gesi asilia kwenye magari mkoani Dar es Salaam, vituo vitakavyosaidia watumiaji wa nishati hiyo kuipata kwa urahisi zaidi.
 
Naona kama mwandika uzi umekurupuka hapa, kidogo uniue kwa "Pressure".

Hio ni project ndogo sana sio ya kuhitaji wataalamu wetu, tena ni ya mkoa wa dar es salaam tu. Ni project ya uwekezaji wa kibiashara (Investment) kama ilivyo Oryx Gas, Taifa Gas, Mihan Gas na nyingine. Ya kuuza na kusambaza mitungi ya gas za matumizi ya majumbani.

Sio swala la kulikuza kiasi hicho, angalieni uzito wa vichwa vyenu vya uzi, mtatuua kwa BP.... Sisi bado tupo kwa DP World na Wakili Mwabukusi!!!
 
View attachment 2683985

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni ya TAQA ya nchini Misri wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika kufanya utafiti na kuangalia masoko ya gesi asilia katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Biashara ya Mafuta na Gesi kutoka TPDC Bw. William Chiome amesema, matokeo ya utafiti huo yatasaidia kuwepo kwa mipango madhubuti ya kusambaza gesi asilia kwa matumizi tofauti.

“Utafiti huu utaenda kufanyika na kukamilika ndani ya mwaka mmoja, na matokeo yake yatawezesha TPDC na makampuni binafsi kujipanga kupeleka miundombinu ya gesi asilia kwa watumiaji mbalimbali sawa na uhitaji ulioonekan,” amesema Chiome.

Kwa sasa kampuni ya TAQA inaendelea na ujenzi wa vituo viwili vya kujazia gesi asilia kwenye magari mkoani Dar es Salaam, vituo vitakavyosaidia watumiaji wa nishati hiyo kuipata kwa urahisi zaidi.
Watusaidie kutafiti kama muungano wetu unafaa.
 
Tusipende lalamika kila kitu.

Hizo kuna tender hutangazwa na watu hujitokeza,mwenye vigezo ndo hupewa.

Sasa unasema kuwa Wazawa wanaweza kuna mzawa yeyote kajenga kituo cha kujaza gesi tofauti na hao, Dangote pale Mkuranga?

Tusipende lalamika kila kitu
 
Wataalamu wa vyuo vyetu aka jalalani ndio hao wanaotafuta uteuzi, kisha kutumwa kwenda na ndege ya Taifa kuchukua dawa za kienyeji Madagascar! Utafiti upi wataufanya na aina hii ya fikra? Wacha wawaze uteuzi!
 
Hawa wataalamu wetu ni wa kutandika viboko, sijuI wao wamesomea kitu gani, wao ni wakusaidiwa kila siku, kwenye kila kitu, kama walemavu wa ubongo, ilimradi kujipendekeza tu kwa mwarabu, kisa bosi wao alishahongwa na waarabu akatoa bandari zetu.
 
Yani Samia na team yake ni kutafuta kila penye fursa kuingia ubia,si aingie ubia na waarabu basi ktk kuendesha nchi,manake kashindwa,aombe wajomba zake waarabu wamsaidie kutawala.
 
Kushirikiana kwenye tafiti sio jambo baya, tena ni muhimu sana kwetu maana tutavuna ujuzi mwingi.
 
Back
Top Bottom