Mahakama ina vyumba vingi ambako kesi nyingine zinakuwa zinaendelea.Haiwi hiyo kesi yao tu.Wakiweka vipaza sauti watasumbua wengine.Pia ukumbuke kuna wafanyakazi wengine wa mahakama Kama mahakimu wakisoma ofisini mwao na kuandika maamuzi ya kesi mbali mbali pia kuna wanaokuwa kazini wakichapa hukumu,na kazi zingine za kiofisi.Huwezi kugezuza mahakama kwa kufunga maspika kama uko mkutano wa hadhara wa CHADEMA.Eneo la mahakama ni maofisi pia yenye watu wanaotakiwa kufanya kazi zao kwa utulivu bila kelele wakiwemo mawakili wa kujitegemea nk
Pia kuna sheria ya kuzuia kelele.Hizo kelele za maspika zitakuwa public nuisance kwa watu wengine na si kazi ya mahakama kuleta public nuisance kwa majirani,wapita njia nk
Na kuna sheria zinazotaka mahakama pawe mahali pa utulivu sio makelele kama kilabuni