OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,015
- 114,360
Habari mpasuko ni kwamba Mwanza imezizima, kesi ya kumpigania mbunge wa wanyonge Ezekiel Wenje.
Biashara zimesimama, mabomu yanarindima.
Wafuasi wa CHADEMA wanakatazwa kusikiliza kesi.
Yupo Kamanda Mbowe, Katibu Mkuu Msomi Dr. Mashinji na makamanda wengine.
Biashara zimesimama, mabomu yanarindima.
Wafuasi wa CHADEMA wanakatazwa kusikiliza kesi.
Yupo Kamanda Mbowe, Katibu Mkuu Msomi Dr. Mashinji na makamanda wengine.
Kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza
Kesi ya kupinga ushindi wa STANSLAUS MABULA iliyofunguliwa na Mh. E. Z. WENJE imeendelea leo.
Upande wa wajibu mashtaka waliweka pingamizi kwenye HATI YA KIAPO ya Shahidi namba Tatu ambaye ni Mh. E. Z. WENJE hivyo kuiomba Mahakama iwape masaa mawili ya kuitolea ufafanuzi.
Baada ya hilo kujitokeza Mahakama ilihairishwa kwa masaa mawili yaliyoombwa, saa Nane mchana Mahakama iliketi upya na kupokea hoja bishwaniwa juu ya HATI KIAPO.
Baada ya pande zote mbili kutoa hoja zake, Mh. Jaji alihairisha kesi hiyo mpaka trh 16 March, 2016 saa tatu asubuhi ambapo aliweka wazi Mahakama kuwa suala hilo haliondoi uhalali wa Mh. E. Z. WENJE kutoa ushahidi wake.
Hivyo inatarajiwa trh 16 March, 2016 Shahidi namba tatu Mh. E. Z. WENJE atatoa ushahidi wake.
Nje ya mahakama wafuasi na wapenzi wa CDM walikuwa wengi sana waliokuja kusikiliza kesi hiyo, hivyo kulazimika Mwanasheria ERICK MUTTA kutoa ufafanuzi wa kilochoendelea mahakamani na kuwaomba wafuasi na wapenzi hao wa CDM kutawanyika kwa AMANI.
Katika hali ya kushangaza Askari wa Jeshi la Polisi waliziba njia nakuanza kuwashambulia kwa virungu na mbwa hata kupelekea majeraha makubwa kwa baadhi ya wafuasi hao, Hali iliyopelekea Mh. E. Z. WENJE Kuingilia kati na mabishano makubwa kuzuka, ilikuwa ni dhahama kubwa na mpaka hivi sasa Mwanachama mmoja ambaye jina Lake halijapatikana amekimbizwa Hospitali kwa Gharama za Mh. E. Z. WENJE.
TUKUTANE TENA MAHAKAMANI JUMATANO trh 16 March, 2016 saa tatu asubuhi.
ERICK MUTTA.
MWANASHERIA,
Bavicha Nyamagana.
MWANZA
16 Marchi, 2016.