JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza ‘Hapa Kazi Tu’ na kubaini ukiukwaji wa makubaliano ya kimkataba ya ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Korea ya Gas Entec Building Engineering iliyo na jukumu la kujenga meli hiyo kuuza sehemu ya jukumu la ujenzi kwa kampuni nyingine.
Hali hiyo imesababisha ujenzi kukomea katika kiwango cha 65% badala ya 95% kwa mujibu wa makubaliano ya muda wa kukamilisha ujenzi wa Meli.
Aidha, inadaiwa kampuni hiyo imepunguza Wafanyakazi kutoka 118 hadi kubakia 22 hali inayosababisha ujenzi wa Meli kutokamilika kwa wakati ambapo Serikali tayari imelipa fedha kwa asilimia 80 hadi sasa.
Waziri Mkuu baada ya kubaini mapungufu hayo ameagiza Uhamiaji Mkoa wa Mwanza kuzuia kwa muda hati za kusafiria za raia saba wa Korea Kusini wanaojenga Meli hiyo na kuagiza wasiondoke nchini hadi wakamilishe ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza.
Ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza ‘Hapa Kazi Tu’ utagharimu zaidi ya bilioni 97.5 za Kitanzania.