Meli ya MV Mwanza kushushwa majini Februari 12

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Ni Magufuli tena.

Tukio hilo la kihistoria la kushushwa kwenye maji kwa meli hiyo inayojengwa katika Bandari ya Mwanza Kusini litaongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma ya Meli nchini (MSCL), Eric Hamissi amewaambia waandishi wa habari jijini Mwanza leo Alhamisi Februari 9, 2023 kuwa utekelezaji wa mradi huo ulioanza Januari, 2019 tayari umefikia asilimia 82. Mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti, mwaka huu.

“Kushushwa kwenye maji kwa meli hiyo haimaanishi kuwa ndio inaanza safari. Hii ni moja ya hatua muhimu katika ujenzi wa vyombo vya majini unaolenga kuhakiki ubora wa umbo ikiwemo uwezo wa kutopitisha maji,” amesema Hamissi.

Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 1, 200, tani 400 za mizigo na magari 20 yakiwemo makubwa matatu inajengwa na mkandarasi kutoka Kampuni ya Gas Entec Ship-Building Engineering na Kang Nam Corporation za Nchini Korea kwa kushirikiana na Suma Jkt.

Itakapokamilika, meli ya Mv Mwanza itafanya safari zake kati ya Bandari za Mwanza, Kemondo, Bukoba, Portbail nchini Uganda na Kisumu nchini Kenya.
 
unachanganya na Mv.Victoria ya mkoloni.
hii Mv.mwanza ni mpya.

279928005_3180934418837186_6711581067375154780_n.jpg
inatisha hii meli "mpya"
 
Katika ujenzi wa hii meli tuli danganywa eti kuna Gati lina jengwa. Billions zika tengwa. Walai na waambia hakuna cha gati pale. Tume pigwa
 
Back
Top Bottom