DOKEZO Mwanza: Mtoto wa mwaka mmoja aoza mkono kisa uzembe wa hospitalini, uchunguzi waanza

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mwanza. Mtoto Nassoro Rashid Nassoro (1) anapigania maisha yake katika wodi za Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza kutokana na madhara ya kiafya ambayo wazazi wake wanadai ni uzembe wa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Tanzanite Jijini Mwanza.

Matatizo ya mtoto Nassoro aliyelazwa katika wodi ya wahanga wa majanga baada ya kukaa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) ya Bugando kwa wiki moja, yalianza Agosti 15 alipofikishwa Hospitali ya Tanzanite na kugundulika kuugua malaria.

Akizungumza na Mwananchi akiwa Hospitali ya Bugando anakomuuguza mtoto wake, Neema Mohamed, mama mzazi wa mtoto huyo alisema baada ya kugundulika kuwa malaria, mtoto wake alitundikiwa dripu ya maji ambayo ndio kiini cha matatizo ya sasa.

Alisema licha ya maji ya dripu kuonekana kuingia mwilini kwa kasi, mkono wa kulia wa uliokuwa na sindano ya dripu ulianza kuvimba huku akipumua kwa shida.

“Nilitoa taarifa kwa madaktari, ndipo daktari mwingine tofauti na aliyetundika dripu alifika na kubaini maji yanaingia kwenye nyama badala ya mshipa kama inavyostahili. Alirekebisha kasoro hiyo kwa kuchomoa sindano ya dripu na kuuhamishia mkono wa kushoto, lakini ule mkono wa kulia ulishapata madhara ikiwemo kuendelea kuvumba,” alisema.

Alisema hali hiyo ilimtia hofu na kuomba rufaa kwenda Bugando, lakini uongozi wa hpsptali hiyo binafsi ulikataa kwa maelzo tatizo tayari limerekebishwa.

“Tuliendelea kushinikiza rufaa huku tukitishia kuwasilisha suala hilo polisi ndipo uongozi wa Hospitali ya Tanzanite ukatupatia rufaa kuja hapa Bugando,” alisema.

Johari Hamisi, nyanya wa mtoto Nassoro anayepokezana kazi ya kumuuguza mjukuu wake hospitalini hapo aliiomba Serikali kuinguilia kati suala hilo kwa kufanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki dhidi ya madaktari na wauguzi waliofanya uzembe huo.

“Si maisha ya mjukuu wangu pekee yako hatarini kutokana na uzembe wa madaktari na wauguzi, bali hata hali ya kiuchumi ya familia yetu pia imeathirika kutokana na kutumia gharama na muda mwingi hospitalini.

“Tunatumia zaidi ya Sh10,000 kwa siku kugharamia mahitaji muhimu ikiwemo chakula na nauli ya kuja hospitali na kurejea nyumbani kila siku,” alisema.

Aliulaumu uongozi wa Hospitali ya Tanzanite kwa kutoonyesha juhudi za kufuatilia na kujua maendeleo ya kiafya ya mjukuu wake, licha ya kutambua matatizo ya sasa yalitokana na uzembe wao.

Daktari Bingwa Bugando
Akizungumza kwa sharti la kutotojwa jina, mmoja wa madaktari bingwa wa upasuaji sanifu katika hospitali ya Bugando alisema hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri ukilinganisha na wiki mbili zilizopita, atafanyiwa upasuaji kurekebisha matatizo ya kiafya yaliyotokana na majeraha katika mkono wake wa kulia.

Alisema baada ya upasuaji mdogo uliolenga kusawazisha jeraha lililotokana na maji ya dripu kuingia kwenye nyama, mtoto Nassoro atafanyiwa upasuaji mwingine kupandikiza nyama kwenye maeneo ya mkono yaliyolika.

Hospitali ya Tanzanite
Kwa zaidi ya wiki moja, juhudi za kupata kauli kutoka uongozi wa Hospitali ya Tanzanite zimegonga mwamba baada ya simu ya kiganjani ya mkurugenzi wa hospitali hiyo, Derick Nyasebwa kuita bila kupokelewa huku ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na wa mtandao wa kijamii ya whatsapp pia haujajibiwa.

Hata hivyo, Mwananchi imefanikiwa kupata nakala ya fomu ya rufaa ya kumpeleka mtoto Nassoro Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando iliyoandikwa Agosti 18, 2022.

Pamoja na kukiri mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kubanika kuwa na malaria, daktari aliyesaini fomu hiyo ambaye hakuandika jina zaidi ya kutia saini anathibitisha mtoto huyo alibainika kuwa na tatizo la mkono wa kulia kuvimba na kubadilika rangi.

Katika fomu hiyo, daktari huyo anasema baada ya kupokelewa, mtoto huyo alibainika kusumbuliwa na malaria na kulazwa kwa siku nne kabla ya kuruhusiwa.

“Siku moja baadaye, alirejeshwa mkono wake wa kulia ukiwa umevimba na kubadilika rangi kwa kuwa nyekundu, kung’aa na maumivu,” inasomeka sehemu ya fomu hiyo.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kuhusu suala hilo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RM0), Dk Thomas Rutachunzibwa alisema ofisi yake haijapokea taarifa za mgonjwa huyo huku akiahidi kufuatilia.

Wakati Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Shadrack Mwaibambe hakupokea simu wala kujibu ujumbe mfupi wa maandishi, Rais wa Chama cha Wauguzi na Wakunga Tanzania (TANNA), Jumanne Bulahya alisema chama hicho kinafualia suala hilo na ikithibitika kulikuwa na uzembe kitachukua hatua dhidi ya wanachama wake waliohusika. “Nawasiliana na viongozi wenzangu wa Mkoa wa Mwanza na tukijiridhisha kulikuwa na kosa la kiweledi tutachukua hatua kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kitaaluma,” alisema Bulahya.

Chanzo: Mwananchi
 
Kama kuna taaluma ambayo wakufunzi huko Vyuoni wanatakiwa kukaza na kuhakikisha hatoki mhitimu aliyeiva nusu ni hii ya Udaktari.

Taaluma nyingine zote wanaweza kuendelea kujifunzia huko makazini bila madhara makubwa ila sio hii ya Udaktari.
 
Sad
 
Vipi madereva wa mabasi ya abiria?
 
Kama kuna taaluma ambayo wakufunzi huko Vyuoni wanatakiwa kukaza na kuhakikisha hatoki mhitimu aliyeiva nusu ni hii ya Udaktari.

Taaluma nyingine zote wanaweza kuendelea kujifunzia huko makazini bila madhara makubwa ila sio hii ya Udaktari.
Tunataka mabadiriko kwenye kada za Afya pekee siyo? Wazazi si mnafurahia mtoto mwenye D 2 kwenda kusoma huo mnaouita utabibu na kozi zingine za Afya .. tuvumiliane sisi wote wa tz tukitaka kubadilika tuanzie chini kabisa ... Na hii kesi tuombee mtoto aendelee vizuri tuu hakuna kesi hapo kwa mlala hoi mwenzetu.
 
Kiutaratibu muuguzi au daktari akiweka ile sindano ya kupitishia dawa kwenye mshipa ni lazima aipime kuona kama itaingiza dawa.

Kitendo cha kuvimba ni kiashiria kuwa haifai kutumika kupitishia dawa. Lakini pia utaratibu unamtaka mtoa huduma kumtazama mgonjwa ndani dakika 5 baada ya kumpa dawa/drip kutazama kama kuna tatizo lolote litatokea.

Na kwa maelezo machache ya waathirika ni kuwa watoa huduma walidharau taarifa waliyopewa na ndugu wa mgonjwa hivyo kupelekea mtoto kuathirika.

Pole sana kwa familia na mtoto pia
 
Tunataka mabadiriko kwenye kada za Afya pekee siyo? Wazazi si mnafurahia mtoto mwenye D 2 kwenda kusoma huo mnaouita utabibu na kozi zingine za Afya .. tuvumiliane sisi wote wa tz tukitaka kubadilika tuanzie chini kabisa ... Na hii kesi tuombee mtoto aendelee vizuri tuu hakuna kesi hapo kwa mlala hoi mwenzetu.
Hakuna Daktari kwa level ya hospital mwenye ufaulu wa D2.
Naona mnawapa lawama madaktari badala nurses zoezi zima la kuweka drip ni swala la nurse na nurses ndio wanashinda na wagonjwa muda wote.
 
Hakuna Daktari kwa level ya hospital mwenye ufaulu wa D2.
Naona mnawapa lawama madaktari badala nurses zoezi zima la kuweka drip ni swala la nurse na nurses ndio wanashinda na wagonjwa muda wote.
Nyie mmeonaga manurses ni wa kulaumiwaga tuuuuuuuuu
 
 Hii hospital wanalinga Sana kwa sababu ndio hospital kubwa ya rufaa kanda ya ziwa muda mwingi wagonjwa wengi wanaumia Ila watumishi hawajali lakini hebu tukumbushane kidogo kipindi magu alikuja na kujenga hospital kubwa chato mlisema ana siasa za ukanda japokuwa inaumiza hilo tukio tujifunze kuwaunga mkono viongozi wapenda maendeleo, maendeleo hayana chama bugando ni jipu najua hamtachelewa kusema skm gang
 
Back
Top Bottom