Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Kufuatia hoja mbili kuhusu kilichotokea katika Hospitali mbili za Mkoani Tanga, mamlaka zimetoa majibu.
Hoja zenyewe ni hizi hapa:
= Hospitali ya Bombo kuna uzembe mkubwa. Inaumiza sana watu kutothamini uhai wa wengine
= Uzembe wa Wauguzi wadaiwa kusababisha mtoto mchanga kuvunjika mkono wakati mama mtu akijifungua Hospitali ya Magunga - Tanga
Majibu ya Serikali kuhusu hoja hizo...
TAARIFA KWA UMMAHivi karibuni kumekuwa na taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kifo cha kuhuzunisha cha mwanafunzi mmoja kilichotokea kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo), na katika tukio jingine kuvunjika kwa mkono wa mtoto mchanga wakati mama mjamzito alipokuwa anasaidiwa kujifungua katika Hospitali ya Mji-Korogwe (Magunga).
Matukio yote haya mawili yanahusishwa na dhana ya uzembe na watoa huduma za afya katika maeneo hayo.
Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa haraka tayari imeshatuma timu za uchunguzi na Mganga Mkuu wa Mkoa kwenye maeneo hayo ili kubaini ukweli wa kina na hatua zinazostahili kuchukuliwa kulingana na matokeo ya uchunguzi huo, na hatutasita kuchukua hatua za adhabu kitaaluma au jinai pale itakapobidi kufanya hivo.
Tunawaomba wananchi waendelee kuwa watulivu wakati suala hili linafanyiwa kazi kwa uzito unaostahiki.
Hoja zenyewe ni hizi hapa:
= Hospitali ya Bombo kuna uzembe mkubwa. Inaumiza sana watu kutothamini uhai wa wengine
= Uzembe wa Wauguzi wadaiwa kusababisha mtoto mchanga kuvunjika mkono wakati mama mtu akijifungua Hospitali ya Magunga - Tanga
Majibu ya Serikali kuhusu hoja hizo...
TAARIFA KWA UMMA