MWANZA: Machinga wameanza kurudi katika maeneo yao kufuatia agizo la Rais

Hapa Makoroboi jijini Mwanza machinga walioondolewa sasa wanarudi katika maeneo yao.

Wanasema ni tamko la Rais.

3011297d53f4663e1316f908e9fb2207.jpg
Duuuh hatari Machinga wa digitali.... wanakamuwa wasap hatari washaona tamko tayari
 
Sidhani kama kuna mtu mnafiki kama wewe humu Jf.
Bendera fuata upepo.
Nina uhakika 100% wakitimuliwa kwa mara nyingine utarudi hapa kusifia.

Huna kumbukumbu
Kuna mnafiki Tanzania zaidi ya Mbowe,lema,Msigwa na Tundu lisu!!!
 
Warudi tu maana hakuna namna

Kila mzawa wa nchi hii anayo haki ya kufanya Kazi zake kwa Uhuru bila kuvunja katiba........

Na nimeona kumbe hawakuvunja sheria yeyote kwa mujibu wa Ikulu wacha wafanye Kazi zao.......
Ila waziri husika wako wapi?? Kazi yao ni nini mpaka ikulu inatoa matamko??
 
Daah polisi wa Mwz sijui wanajisikia huko walipo kwa walichokifanya.
 
Dah! Watanzania ni wapole aisee!
Wanajichimbia vinguzo vyao,mambo yameisha!
Hasara waliyoipata wala hawatahangaika nayo.....Maskini!
Na kesho wakikutana na yule "mama mchochezi" watamwamkia "shikamoo mama"....
Only In TZ!
 
Kila kiongozi anakuja na tamko lake,,,hivi mbona siku za nyuma haikuwepo hii?
Mara kazi yenu kuzaa tu, alafu mwingine anakuja anakanusha eti ilikuwa utani
Mara machinga waondolewe , mara warudi,,,
Mara wahitimu wasivae majoho kabla ya degree, mara hiyo haipo watavaa tu,,,
Mara diploma huendi chuo kikuu, mara utaenda tu,,,,
Ziara za Makonda kule Dar ndo usiseme,,,,Makonda hivi na serikali za mitaa vile,,,
MENGINE YANA UCHANYA NDANI YAKE, ILA TUANGALIE NA UHASI pia,,,tusishangilie kwa kila kitu,.

SIJUI KESHO WATASEMAJE MMMH
 
Nijambo la maana alilo lifanya mh rais kwakutoa agizo la machinga kurudi katika maeneo yao
Kweli wewe ni rais wa wanyonge
 
Warudi tu maana hakuna namna

Kila mzawa wa nchi hii anayo haki ya kufanya Kazi zake kwa Uhuru bila kuvunja katiba........

Na nimeona kumbe hawakuvunja sheria yeyote kwa mujibu wa Ikulu wacha wafanye Kazi zao.......
Imekatazwa kazi ya siasa zingine ruksa
 
Mwenye kujua tofauti ya kile kilichofanywa na viongozi wa Dar kwa machinga na kile kilichofanywa na viongozi wa Mwanza kwa machinga anisaidie, akinisaidia hilo anisaidie pia kunielewesha kwanini wa Dar hakukuwa na tamko ila hawa wa Mwanza limetoka tamko. Kwanini wa Dar waliambiwa wana support ya mkuu kwa asilimia 100 na hawa wa Mwanza wamepewa onyo ilihali walichokifanya kinafanana. NISAIDIENI KUELEWA, MIMI KICHWA CHANGU KIZITO HIKI.
 
Hapana aisee..
Hapa kuna kitu hakipo sawa,kwa nini asingezuia kabla?watu wameshapata hasara na walishaenda huko walipopelekwa leo anasema warudi?
Taatifa za kuondoshwa zilikiwepo muda mrefu na hata kwenye vyombo vya habari tuliona wananchi wakilia wakiomba wasiondolewe hakuna aliyejitokeza kusitisha.
Hii ni kuchonganisha wananchi na watumishi wengine
sasa azuie kabla alijua kuwa itatokea? acha kuongea pumba
 
nampongeza sana Rais magufuli. walichofanya serikali ya mwanza na serikali zote zilizopita ni kupokea rushwa tu ya mtu fulani ili wengine wafukuzwe wao wapate maeneo ya biashara. rais ana mamlaka ya kuwaonea huruma watu wake hata kama sheria isemaje.. so hongera jpm waache wamachinga wafanye biashara popote mpka mtakapo wapa sehemu ya kufanyia kazi..long live jpm
 
Hapa Makoroboi jijini Mwanza machinga walioondolewa sasa wanarudi katika maeneo yao.

Wanasema ni tamko la Rais.

3011297d53f4663e1316f908e9fb2207.jpg
Kama ni kweli hii taarifa kuna mdau ameshare kwenye group la whatsapp
IMG-20161206-WA0001.jpg
IMG-20161206-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom