Mwanza kutamu asikwambie mtu

Nakadori

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,781
20,946
Dahh sijui nianzie wapi...ila naomba kwanza nianze kwa kuwasalimia.

Basi bwana ....
Nimegundua kwamba nilikuwa nakosa vingi kwa kutokupajua mwanza.....yani ukiondoa dar es salaam naweza kusema mkoa unaofwata kwa uzuri ni Mwanza...(ni maoni yangu). Najua mtasema Arusha. Arusha pia nimeishi ila kwakweli hapafikii Mwanza.

Kwanza ni pazuri...
Ni pasafi....
Pili hali ya hewa ni rafiki......
Starehe pia zipo kama zote...
Sema tu asee kama mfuko umetoboka usiende. Labda uwe na ndugu kwamba utaishi bure gharama yako iwe nauli tu na ugali wa shikamoo.

Wasukuma pia sio wachoyo sana.....ila nilichoshangaa mara nyingi nikipita mtaani naangaliwa sana(japo haikuwa mara zote).....halafu nilipokuwa naongea wananiita manka wakati me sio manka. Jamani wasukuma ina maana mtu ambaye anaongea tofauti na nyie ni manka?

Wadada na wamama wa kule wote wana shepu za maana na miguu ya bia...sikuona mwenye fito kule wala mwenye pasi ....so wale wazee wanaopenda ishu hizo patawafaa.

Nakushauri kama hupajui mwanza jitahidi ukatembee mwanza hutajutia pesa yako.
 
Kweli si kila ukipendacho duniani waweza kukipata.

Nikiwa mdogo nilikuwa nina ndoto sana za kuishi Zoo, Moro na A town, maajabu sasa ya dunia niko Dar, lakini napaona pa kawaida saaaana kama vile uswazi.

Sinza, Magomeni, Keko, ni pa kawaida sana na nyumba zimebanana, pia mvua inyeshe wala isinyeshe ni shida tupu.

Ila Masaki, Mwenge Mlalakuwa, Osterbay, Mbezi, Kimara, Goba pamekaa vizuri sana kuishi.
 
Wa Arusha niko hapa…
Nilikuwepo Mwanza zaidi ya 1 week!
Aisee ni patamu
Nikiokota hela nitarudi tena.
Hata wafanya biashara wao wana ukarimu kwa mteja. Hiki kitu Chuga sio sana, labda wapaka rangi wa Chuga ndio at least wako wakarimu kwa mteja.
Mmmmmmmh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom