Mwanza ikitengenezewa mazingira mazuri itakuwa sehemu nzuri ya kuishi hapa Afrika Mashariki

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Mwanza ni mji ambao unakua kwa kasi kiuchumi na maendeleo yake sio madogo pia, waliofika Mwanza miaka 10 iliyopita ukilinganisha na Leo ni vitu viwili tofauti kabisa na watakua pamoja na Mimi.

Dar es Salaam ni jiji la biashara, pia Kuna mzunguko mkubwa wa pesa lakini sio sehemu rafiki ya kuishi ukiwa na kipato kidogo Dar es Salam wewe ni muhangaikaji tu, imagine mtu ana familia lakini wanakaa chumba kimoja au viwili, kaka angu alienda kutafuta maisha Dar, mwaka wa 7 huu hakuna anachojivunia.

Ukiwa na kipato cha kawaida jiandae kununua kiwanja mkoa wa pwani, yaani unabangaiza daresalam unaenda kupumzisha fuvu chalinze au kisarawe.

20240102_180605.jpg


Joto la hapo ndio usipime, Tena ukiwa mbangaizaji jiandae kuloana mpaka mbupu huku ukiwa na matumaini uchwara, lakini kiukweli daresalam pesa hipo na atakaeenda kutafuta maisha serious lazima ayapate.

Turudi Mwanza, kwanza Hali ha hewa ni soft hakuna mvua Wala jua la kuunguza, Kuna vipindi vya baridi na vipindi vya vya joto kiasi lisilokera.

Mwanza ya Sasa sio kama Ile, nimeingia hapa juzi naona kuanzia usagara Barabara yoote mpaka buhongwa watu wanashusha mijumba tu, kuanzia pasiansi mpaka airport kayenze watu ni wanajenga mijumba mikubwa hatari, Barabara ya lami kutoka corner ya bwiru -buzuruga watu wamejenga haswaa na kupata viwanja hapo nyasaka huwezi pata kuanzia 10 million, buswelu zamani ilikua porini nje ya mji lakini sasahivi ndio pamechafuka Sana, ukitaka kiwanja Cha bei Chee uende kisesa kwa mbele au magu kabisa 😁.

Inabidi serikali iifanye Mwanza kua center ya kibiashara kwa kujenga bandari kavu kubwa, mipango miji wafanye kazi yao kuzuia ujengaji holela wa nyumba za hovyo.

Kwakweli Mwanza ni uswisi ya EA 😁😁
 
Back
Top Bottom