Uchaguzi 2020 Mwanza Huduma adaiwa kumwaga pesa kama Njugu Bunda Mjini akisindikizwa na Viongozi wa CCM Wilaya

Habari bila picha hainogi. Halafu hela ni za kwake kwann tuone ni ubaya? Acheni azigawe maana hata mwenye nchi alishagawa sana fedha hadharani tena nyingi sana. Tuwe wapole tu ukimuona mtu anamwaga hela ujue anazo za ziada anasambaza uchumi mzuri kwa wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkirindi, Mkuu Mkirindi, mimi ni realist na muumini wa free speech na freedom of expression, hivyo I always speak my mind freely and expresses my opinions truthfully.

Kama kuna watu wana pesa zinazo wawasha, wanagawa fedha hizo kama njugu kwa wananchi for whatever reasons, wafaidika na wanufaika wa fedha hizi ni wananchi wa maeneo hayo, kuna ubaya gani?.

Nachukia rushwa ambayo ni adui wa haki, lakini sina tatizo kabisa na takrima, as long as uwezo wa kutoa takrima, sio kigezo cha kupitishwa kuteuliwa kuwa mgombea. Huu mimi nauita ni uwezeshaji wananchi Kiuchumi. Acha wenye fedha wagawe fedha kwa wananchi ili wananchi wanufaike na fedha hizo. Kuna ubaya gani haoo?.
P
Kabendera karma inazidi kukutafuna na utavurugwa saaana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika hali ya kushangaza Zury Nanji maarufu kama Mwanza Huduma Mfanyabiashara wa Jijini Mwanza ameonekana Bunda Mjini akigawa pesa hadharani.

Huku akiwa na mabaunsa, wapambe na wanakwaya wakimsindikiza Mwanza Huduma amepita Vijiwe vya Kahawa na Maegesho ya Magari na kugawa kati ya shilingi Elfu 50 na laki moja kwa watu hadharani, Pia amepita kwa baadhi ya Mabalozi wa nyumba kumi na kumwaga laki mbili na laki tatu.

Akionekana kujiamini amekusanya baadhi ya wazee katika nyumba moja ya Balozi Semeni Kasuku na kutoa Laki NNE.

Wapambe wa karibu nae wamekabidhiwa shilingi Milioni Moja na kuanza kugawa Elfu kumi Au Elfu kumi na tano kwa Vijana wa Bodaboda na Wanakwaya maalum kwaajili ya kumpamba 'mgombea' huyo.

Kabla tukio hilo la kujitokeza hadharani, Baadhi ya Viongozi akiwemo Mwenezi wa CCM Wilaya Ndugu Bonavencha Makanga akiwa na wasaidizi wake walipita kwa Makatibu wa Kata na kuwapatia posho (rushwa) na baadhi ya Wenyeviti kama sehemu ya salam za Mhindi huyo ambae ameanza kampeni mapema kabla ya muda.

Leo walipoulizwa kwanini wanafanya mambo hayo hadharani bila kuogopa Mpambe wa karibu ajulikanae kama Masalu na Mwingine Selemani Nasoro walisema wamepata kibali kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya hivyo hawatishwi na mtu.

Hali hii isipodhibitiwa Bunda Mjini wagombea watatoana Taya maana Rushwa kwa viongozi wengi inatisha kama Corona.
hilo sio geni kwa CCM. Kipindi cha siasa za kistaarabu za vyama vingi hangetubutu kufanya hivyo maana chama kisingempitisha kwenda kushindana na mgombea wa upinzani. Sasa kwa vile CCM imeona vema kufuta upinzani basi ngoja wanyukane CCM kwa CCM na msemo wao wa enzi hizo wa mwenye kisu kikali ndiye atakula nyama unarudi kwa kasi. Kuua nguvu ya upinzani kutawatesa wanaCCM wasafi na wasio na fedha. Watu sasa watachaguliwa kwa misingi ya kuwa na fedha na kutoa rushwa.
 
Mkirindi, Mkuu Mkirindi, mimi ni realist na muumini wa free speech na freedom of expression, hivyo I always speak my mind freely and expresses my opinions truthfully.

Kama kuna watu wana pesa zinazo wawasha, wanagawa fedha hizo kama njugu kwa wananchi for whatever reasons, wafaidika na wanufaika wa fedha hizi ni wananchi wa maeneo hayo, kuna ubaya gani?.

Nachukia rushwa ambayo ni adui wa haki, lakini sina tatizo kabisa na takrima, as long as uwezo wa kutoa takrima, sio kigezo cha kupitishwa kuteuliwa kuwa mgombea. Huu mimi nauita ni uwezeshaji wananchi Kiuchumi. Acha wenye fedha wagawe fedha kwa wananchi ili wananchi wanufaike na fedha hizo. Kuna ubaya gani haoo?.
P
Tena mbona wananchi hao hao waliahidiwa kugawiwa 50M@ kijiji? Hizo mbona hamkulalamika? fedha ni fedha tu. Acha huyo jamaa naye agawe kwa wananchi.
 
Tena mbona wananchi hao hao waliahidiwa kugawiwa 50M@ kijiji? Hizo mbona hamkulalamika? fedha ni fedha tu. Acha huyo jamaa naye agawe kwa wananchi.
Hizo milioni 50 za kila kijiji, mbona ziliisha gawiwa kitambo kupitia huduma kwa jamii.
P
 
Nipo hapa madras india kwa mwezi wa tatu sijawahi kumuona mwafrika akiongoza hata kitongoji. Nashangaa huko kwetu wahindi ndiyo wameshika hatamu

In God we Trust
siungi mkono rushwa lakini Mwanza huduma, ni Mtanzania mwenye asili ya kihindi wengine ni wasukuma kabisa, acha ubaguzi wa rangi.
 
chuki, Mkuu Chuki, acha chuki.
Maadam wanufaika na fedha hizo ni wananchi, hakuna ubaya wowote kwa mwenye fedha yoyote kugawa fedha zozote kwa wananchi wahitaji kwa nia yoyote au bila nia yoyote, cha muhimu ni wananchi watapata pesa za bure bure.

Tena nitaishauri CCM ifungue fursa, kila mwana CCM yoyote mwenye fedha ya kumwaga, inayomuwashawasha, na angependa kuitumia hiyo fedha yake kama means ya kutangazia nia ya kugombea jimbo lolote, aruhusiwe, iwe rukhsa kujipitisha pitisha kumwaga fedha, wananchi wanufaike.

Kwavile mwisho wa siku, wanaopitisha majina ya wagombea ni vikao vya juu vya chama, na sifa za kupitishwa sio umegawa fedha kiasi gani, bali chama kitawapitisha wagombea bora, na ikitokea wewe mgawa fedha ndio umepitishwa, unakuwa umepitishwa kwa kukidhi vigezo na sio kwasababu iligawa fedha.
P
This is wrong P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom