Mbunge Furaha Matondo akabidhi viti mwendo 70 Wilaya zote Mkoa wa Mwanza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,891
939

MBUNGE MHE. FURAHA N. MATONDO AKABIDHI VITI MWENDO 70 KWA WALEMAVU KWA WILAYA ZOTE, MWANZA

Mbunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Mwanza Mhe. Furaha N. Matondo katika ziara yake aliyoifanya Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza amekabidhi Viti Mwendo 70 kwa watu wenye ulemavu Mkoa wa Mwanza.

Hafla ya ugawaji wa Viti Mwendo hivyo ilifanyika katika Ukumbi wa Gandhi Hall uliopo Wilaya ya Nyamagana ikihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Kighoma Malima, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa na Wilaya, Viongozi wa UWT Mkoa na Wilaya, Madiwani, Wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jiji la Mwanza.

"Nimefarijika sana kukutana na ndugu zangu ikiwa ni pamoja na kugawana kile nikipatacho nimepata Amani Kubwa sana na nitafanya hivi kwa wilaya zote za mkoa wa Mwanza" - Mhe. Furaha Matondo

"Nimepata wasaa wa kuendelea kujumuika na ndugu zangu wenye mahitaji maalum Wilaya ya Ilemela, ninamshukuru MUNGU sana kwa ajili ya Madaktari pia ambao wapo pamoja Nami kwa ajili ya huduma hii. Niwashukuru sana viongozi wa Chama pamoja na jumuiya ya UWT, UVCCM na Jumuiya ya Wazazi na wananchi wote wa Wilaya ya Ilemela, nasisitiza wahitaji ni watoto wetu ni Baba na mama zetu na ndugu zetu na Jamaa zetu tuwalinde tuwapende tuwajali" - Mhe. Furaha Matondo

"Viti Mwendo hivyo vitagaiwa kwa Wilaya zote saba za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum" - Mhe. Furaha Matondo

Aidha, Mhe. Furaha Matondo amempongeza Rais wa JMT Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza Miaka Miwili Madarakani kwa kishindo huku akianisha mambo ambayo yamefanyika katika Mkoa wa Mwanza.

#UWTImara
#JeshiLaMama
#KaziIendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-26 at 20.05.07(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-26 at 20.05.07(1).jpeg
    52.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-03-26 at 20.05.10.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-26 at 20.05.10.jpeg
    36.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-03-26 at 20.05.07(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-26 at 20.05.07(2).jpeg
    64.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-03-26 at 20.05.10(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-26 at 20.05.10(1).jpeg
    66.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom